Nataka kuanzisha Kabila jipya na la kisasa

yeah ni rahisi, lakini muanzisha kabila kasema tutakua hatupo chini ya taifa lolote…ndo nikahoji itawezekanaje
Hapo atujuze😀😀
Mimi siko sana kwenye utambulisho kwa maana hakuna faida zozote tukitambulika sasa. Cha msingi ni taratibu kujenga misingi imara ya kabila letu.

Utambulisho utakuwa na maana kwetu sisi ndani kwa ndani kujuana lakini si watu wa nje 😎
 
Ukiweza kuepusha kabila lako na uchawi, 50% ya mafanikio itakuwa mbeleni mwako
 
Ukiweza kuepusha kabila lako na uchawi, 50% ya mafanikio itakuwa mbeleni mwako
Hizo ndiyo moja ya sababu zinazonisukuma kufanya jambo hili. Hatutakuwa na makandokando kama hayo. Kitakuwa kizazi pure 😎
 
naomba niwe mmojawapo mkuu....jina langu liwe mojawapo ya koo za kabila letu jipya
 
Hii nchi kuendelea itakuwa ni ngum sana,yaani unawaza kujenga vitu kama kabila tena? Haya...sasa hilo kabila litaanza lini kujijenga mkuu?
 


Kabila halianzishwi na mtu bali linaanzishwa na Mungu mwenyewe na tayari makabila yalishaanzishwa na kamwe huwezi pata kabila jipya nje ya makabila yaliyokuwepo. kuanzisha kabila jipya ni sawa na mtu kuanzisha bahari mpya mbali na bahari hizi zilizokwishakuwepo.
 
Wewe hauna tofauti na Nimrod wa mnara wa Babeli, muulize kilichompata.

Nguvu iliyo nyuma ya wazo lako sio nzuri. Utapotea
 
Nipo tayari kua mmoja wa kabila jipya,
Kikubwa tu;
Kusiwe na mambo ya ushirikina,
Tusichanganye Kabila na Dini,
Kuwe na Usawa kwa kila Mtu,
Kuwe na demokrasia ya kweli,
Kabila liendane na mfumo wa Dunia wa Sasa kwa maana Sayansi na Teknolojia.
 
Zipo jumuiya (societies) zenye mrengo mmoja na utaratibu wa pekee pamoja na itikadi yao ya kipekee. Zipo brotherhoods mbalimbali kama Freemasonry, Illuminati, Sculls and Bones, Knight Templers, mashirika ya kitawa ndani ya Kanisa Katoliki yanayoishi kama familia ndogo ndogo na kubwa kubwa, n.k.

Kwa ujumla halitakuwa jambo nje ya hayo niliyotaja hapo. Kuliita kabila utaita hivyo lakini utaishia na mifumo kama niliyotaja hapo juu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…