Nataka kuappeal matokeo yangu ya A-Level ya zaidi ya miaka 10 iliyopita

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Ndugu wana jamii wa Jamii Forums, naombeni ushauri wenu katika hili.

Nilipokuwa A-Level nilikuwa nina matatizo fulani shuleni na matokeo ya form 6 yalipotoka sikupata matokeo mazuri na naamini mpaka leo kuwa kuna kamchezo kalifanyika. Hili jambo limekuwa linaniuma sana kwa sababu naona kama nilionewa.

Miaka zaidi ya 10 imepita, je naruhusiwa bado kwenda kuappeal ili mitihani yangu iangaliwe upya?
 
Mleta mada umri huo bado unalilia matokeo ya kidato cha sita ili iweje?
Unataka kwenda kukopea benki?
Wenzio hayo matokeo tumeshayasahau sasa hivi tunataka kujua benki kuna salio kiasi gani?
Tafuta pesa aiseee hakuna duka linalouliza matokeo yako ya kidato cha sita,wao wanataka pesa yako tu.
 
Kwa lugha ya kisheria ushakuwa TIME BARRED.
Ila kama unajiamini una kichwa unaweza kureseat Ili upate hizo A.
 
Kuna Watanzania toka mmeijua ladha ya pesa hamchoki kuonyesha ushamba wenu. Mnadhani pesa ndiyo kila kitu.
 
Na mim nisaidie kuuliza.

Naweza apil matokeo yangu ya darasa la saba ya mwaka 2002.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuache Kwanza tukamzike Bibi Malkia Mkuu wa Jumuiya pendwa
 
Hizo karatasi zenyewe za mitihani iliyofanyika miaka 10 iliyopita zitakuwepo? Nina hakika zitakuwa zilishapigwa kiberiti siku nyingi . Tafuta pesa ndugu achana na hayo makaratasi ya mitihani ya zilipendwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…