Nataka kufungua kijiwe cha kitimoto pembezoni mwa barabara. Je, wazo hili ni sahihi?

Nataka kufungua kijiwe cha kitimoto pembezoni mwa barabara. Je, wazo hili ni sahihi?

Hyrax

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2023
Posts
1,458
Reaction score
4,409
Wakuu nimenunua eneo la biashara mji X na lipo pembezoni mwa barabara nzuri tu, moja ya biashara nayotaka kufanya eneo hilo ni kuweka kibanda cha kisasa cha nyama ya kitimoto.

Sasa najiuliza Je, nitakuwa nimevunja sheria yoyote kwa kufanya hivyo ikiwa watakaokuwa wanapita eneo hilo ni ndugu zangu waislam na wale wakristu wenye misimamo mikali?

NAOMBA MNISAIDIE MAWAZO kama kuna utaratibu wowote wa kufuata kama nataka kuweka kijiwe cha kitimoto sehemu ya wazi.

Ntashukuru kwa michango yenu.
 
Wakuu nimenunua eneo la biashara mji X na lipo pembezoni mwa barabara nzuri tu, moja ya biashara nayotaka kufanya eneo hilo ni kuweka kibanda cha kisasa cha nyama ya kitimoto, Sasa najiuliza Je ntakuwa nimevunja sheria yoyote kwa kufanya hivyo ikiwa watakaokuwa wanapita eneo hilo ni ndugu zangu waislam na wale wakristu wenye misimamo mikali? NAOMBA MNISAIDIE MAWAZO kama kuna utaratibu wowote wa kufuata kama nataka kuweka kijiwe cha kitimoto sehemu ya wazi.

Ntashukuru kwa michango yenu.
fungua haina shida mkuu,tupate ulaji
20250816_221131.jpg
 
Wakuu nimenunua eneo la biashara mji X na lipo pembezoni mwa barabara nzuri tu, moja ya biashara nayotaka kufanya eneo hilo ni kuweka kibanda cha kisasa cha nyama ya kitimoto, Sasa najiuliza Je ntakuwa nimevunja sheria yoyote kwa kufanya hivyo ikiwa watakaokuwa wanapita eneo hilo ni ndugu zangu waislam na wale wakristu wenye misimamo mikali? NAOMBA MNISAIDIE MAWAZO kama kuna utaratibu wowote wa kufuata kama nataka kuweka kijiwe cha kitimoto sehemu ya wazi.

Ntashukuru kwa michango yenu.
Utakuwa haujavunja sheria kama eneo hilo linaruhusiwa na mamlaka ujenge kibanda.Pili,utakuwa unatufundisha uvumilivu na kuyachukulia mambo kwa wepesi sisi tusiokula kitimoto.Nakuombea dua njema katika biashara yako mpya.
 
Kitendo cha kuuliza tu inaonesha nawe una mashaka. Hivyo sikushauri.
 
Fungua kijiwe cha kitimoto hata roundabout au stendi kuu ya mabasi. Utakuwa hujavunja sheria yoyote
 
Back
Top Bottom