Nataka kughairi kufunga ndoa, zimebaki week 3. Nifanye nini kutimiza azma yangu?

Nataka kughairi kufunga ndoa, zimebaki week 3. Nifanye nini kutimiza azma yangu?

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Wakuu, kama heading inavyosomeka, Nina tarajia kufunga ndoa week tatu zijazo ( tar sitaweka ili kuepusha mambo mengi) lakini ni mwezi huu wa nane.

Kimsingi sidaiwi, taratibu zote nimefuata, mahali nimelipa na kilichobaki Ni siku ya tukio tu kuidhinisha Jambo!

Lakini kwa sasa najisikia mzito sana kwenye hili swala, Yan kifup sielewielewi, nahitaji niterminate mchakato huu, ila nikifikiria maandalizi ya sherehe husika kwa maana ya nyumbani, kanisan na jamii yote kwa ujumla najiuliza nijinasuaje ili nitimize adhma yangu!

Naombeni ushauri wenu katika suala hili.
 
Yaani ughailishe Kwa sababu unajisikia mzito au Kuna sababu ingine?

Kama sababu ni hiyo Wala usiwaze sana, achana na kuhangaika na watoto wa watu hadi ukue, ukishakuwa tayari kuwa baba wa familia then utaoa. Sasa hivi endelea na ujana au utoto wako kwanza
 
Wakuu, kama heading inavyosomeka, Nina tarajia kufunga ndoa week tatu zijazo ( tar sitaweka ili kuepusha mambo mengi) lakini ni mwezi huu wa nane.
Ndoa ni jambo kubwa sana katika maisha hasa kwa wakristu, hutakiwi kuingia ukiwa mzito nafsini mwako. Mshirikishe kiongozi wako wa kiroho, atakusaidia bila kukuabisha.
 
Back
Top Bottom