munisijo
JF-Expert Member
- Apr 10, 2012
- 1,126
- 942
NDOA sio lelemama na si kwa wenye roho nyepesi; NDOA ni tamu lakini pia sio rahisiWakuu, kama heading inavyosomeka, Nina tarajia kufunga ndoa week tatu zijazo ( tar sitaweka ili kuepusha mambo mengi) lakini ni mwezi huu wa nane.
Kimsingi sidaiwi, taratibu zote nimefuata, mahali nimelipa na kilichobaki Ni siku ya tukio tu kuidhinisha Jambo!
Lakini kwa sasa najisikia mzito sana kwenye hili swala, Yan kifup sielewielewi, nahitaji niterminate mchakato huu, ila nikifikiria maandalizi ya sherehe husika kwa maana ya nyumbani, kanisan na jamii yote kwa ujumla najiuliza nijinasuaje ili nitimize adhma yangu!
Naombeni ushauri wenu katika suala hili.
Binafsi naamini kigezo cha kwanza cha kufunga ndoa ni kuwa tayari kiakili hii itakusaidia sana kwenye vipindi vigumu vijavyo ambavyo siku zote na kwenye NDOA zote huwa vipo, kama moyo wako unakataa kabisa usikilize kwani majuto ni mjukuu. NDOA sio ya jamii yote kwa ujumla, NDOA ni yako wao yao ni harusi tu.
Nahisi pengine hali yako inasababishwa na kiburi cha mwezako, usiende nalo hilo kwenye NDOA ni hatari.
Ujinasueje?
- Ongea na mwenzako kwamba unataka ''kujinasua''
- Ongea na wazazi wako, wao ni watu wazima na wanaweza kukusaidia on the way forward
Kila la kheri