Nataka kughairi kufunga ndoa, zimebaki week 3. Nifanye nini kutimiza azma yangu?

Nataka kughairi kufunga ndoa, zimebaki week 3. Nifanye nini kutimiza azma yangu?

Sikiliza mkuu; Ndugu yangu mwaka 2020 alighaili kuoa, tena ndoa ya kikristo na ulibaki muda mchache km wewe. Alipata lawama kiasi kwamba lawama zingekuwa mfuko angekuwa na matobo kuzidi tenga

Ndugu wa mwanamke wakamfanya adui kuanzia siku hiyo Hadi leo.Hawataki hata kumuona

Sababu ilikuwa hivi;Huyu binti ni mrembo kweli kweli kutoka ugogoni Dodoma.Ana kalio unaweza kuweka kikombe juu kisianguke,mguu ndy balaa,lkn sasa mzee baba alikuwa kila akiomba mzigo hataki kumpa anamwambia anavunja Sheria na yeye ni binti mlokole wasubiri harusi ipite mzigo atapata.jamaa akamjibu siwezi kuuziwa mbuzi kwenye gunia Mimi,nataka tupeane mambo kwani shida iko wapi na taratibu za mahali zote nimetimiza bado ndoa Tu

Binti Alipoona jamaa amekuwa mbabe na kumtishia kwamba hawezi kuuziwa mbuzi kwenye gunia ikabidi siku moja aje kumpa (aliongopa anaenda kuimba kwenye mkesha akaja kwa bro kulala) .
Alichokutana nacho akaishia kuwalaaani wazazi wa Yule binti kuanzia Ile siku maana wamemfanyia kitu cha kijinga na ukatili sn mtoto wao..Wamemkeketa

Akaterminate maswala ya kuoa na ulibaki muda mchache tu harusi kufanyika
 
Upo ktk wakati ambao MUNGU anapaswa awe msaada wako kujua ni nn kilicho mbele , maamuzi ni wewe Wala hamna yeyote anayeweza kukuambia ufanye Nini lkn Mungu aweza kukujulisha kinachoweza kukupata mbeleni ila wewe ndiyo mwamuzi.

Unatazamia kufanyia wapi ndoa Yako?
 
Namna ya kuahirisha ni kutoweka nyumbani na Kwenda unakojua wewe tu hadi pale tarehe ya harusi ipite. Ili kutowaweka wazazi kwenye presha kubwa acha ujumbe juu ya kile unataka kukifanya ila hakikisha simu yako iwie hewani. Unaweza kusajili laini mpya ambayo utakua unatumia kununulia bando ili usiwe mpweke.
Na kama moyo wako unasita, nikuambie acha tu Mkuu.
Kwanza sikai home, nipo mkoa X kikazi, home ni mkoa Z, na mwenza ni mkoa Y yupo kikazi!

Kwa hiyo mambo yanayoendelea kule nayadaka kwa simu tu, na mahitaji yote natuma note! Ila Sasa naishiwa nguvu , na nakosa raha na Jambo langu
 
Nisikilize homie
Hapo ilo swala sio rahisi hata kidogo maana unaweza timiza adhima yako kwakulazimisha lakini matokeo yake ni makubwa sana na yataathiri wengi kwa namna mbalimbali ,
Nakushauri kutafuta chanzo Cha huwo uzito wako na ujue utawezaje kurekebisha,
Kama haujamlizia mwali tafuta namna yakua mkweli bila kuumiza roho za watu
Kikubwa fikiri kabla ya kutenda
 
Ahirisha kwa miezi 6 au mwaka mmoja. Nina shuhuda moja nzito ila siwezi kuiandika kwa sasa.

Waombe wazazi wakupe mwaka mmoja zaidi.

Learn to trust your intuition

Lakini Mungu wetu ni Mungu wa miujiza hata kwenye hiyo shida bado atatoa na mlango wa kutokea.

But trust your intuition
 
Ailisha mkuu

AILISHA = AHIRISHA
Wakuu, kama heading inavyosomeka, Nina tarajia kufunga ndoa week tatu zijazo ( tar sitaweka ili kuepusha mambo mengi) lakini ni mwezi huu wa nane.

Kimsingi sidaiwi, taratibu zote nimefuata, mahali nimelipa na kilichobaki Ni siku ya tukio tu kuidhinisha Jambo!

Lakini kwa sasa najisikia mzito sana kwenye hili swala, Yan kifup sielewielewi, nahitaji niterminate mchakato huu, ila nikifikiria maandalizi ya sherehe husika kwa maana ya nyumbani, kanisan na jamii yote kwa ujumla najiuliza nijinasuaje ili nitimize adhma yangu!

Naombeni ushauri wenu katika suala hili!
MAHALI= MAHARI
 
Wakuu, kama heading inavyosomeka, Nina tarajia kufunga ndoa week tatu zijazo ( tar sitaweka ili kuepusha mambo mengi) lakini ni mwezi huu wa nane.

Kimsingi sidaiwi, taratibu zote nimefuata, mahali nimelipa na kilichobaki Ni siku ya tukio tu kuidhinisha Jambo!

Lakini kwa sasa najisikia mzito sana kwenye hili swala, Yan kifup sielewielewi, nahitaji niterminate mchakato huu, ila nikifikiria maandalizi ya sherehe husika kwa maana ya nyumbani, kanisan na jamii yote kwa ujumla najiuliza nijinasuaje ili nitimize adhma yangu!

Naombeni ushauri wenu katika suala hili!
Najitolea kufunga ndoa na huyo dada maadam ushagharamia niende naye honey moon afu sku ukijisikia kuwa nae unamchukua usinidissapoint tafadhal✍
 
Oya skia jatutaki mauaji.
Wewe unajua kuna sababu hutaki kuisema. Sema sababu. Ongea kiume. Kama unawasiwasi tafuta msaada hapa. Kama unahisi au umepenyezewa mchumba ako ana tabia za KI INJINIA uliza toa code anayemfahamu aje PM upate uhakika ujiridhishe ufanye maamuzi. Kuliko kukaa na kusubiri tufanyr ubashiri wa tatizo lako wakati wengine huwa EXCITED na kuoa regardless na HOFU lakini hupenda tukio lao liwe perfect.

## SPEAK OUT SAVE A SOUL
 
Wakati mwingine huwa ni hofu tu , mkuu labda au kuna jambo la bi dada unalifahamu toka kitambo umeliweka moyoni !!!
Sio lazima iwe kucheat , hata kwenye maumbile na tabia na hujamwambia ila vinakupa uzito !!
Ila asee utakachokifanya ni kibaya sana !! Ni mkosi kwa dada , pia itamwathiri kisaikolojia !!! Atahitaji waangalizi wa karibu anaweza hata kujiua kama alikua amekolea sana !!!

Mimi nawaza endelea na harusi , fungeni ndoa ikitokea hicho kinachokupa uzito piga chini itaeleweka zaidi kuliko ukiondoka ghafla !!

Pia huenda ni hofu tu za kawaida !! Kama wale wengine kabla ya mtihani mtu anaumwa kabisa !! Au kwa kuwa ni mara ya kwanza !! Au wale wanaoenda kwenye interview mtu anatetemeka kama ana homa akishaingia swali tu la mwanzo , ujasiri unarudi vizuri tu !!! Unaijua Gamophobia mkuu ?

Gamophobia
is a fear of marriage and commitment.1 It is characterized by feelings of excessive and persistent fear of being in a relationship, making a commitment, or getting married.
 
Back
Top Bottom