Nataka kughairi kufunga ndoa, zimebaki week 3. Nifanye nini kutimiza azma yangu?

Hapana mkuu, naomba niseme both of us ( wahusika wa ndoa ) tuko okay financially
Duh Kwanini sasa mkuu

Nadhan kuna kitu kinasababisha...
Chaweza kua personally au physically
Ila kipo
Ni vema uki share
 
Shetani yupo kazini kama kuna uliyempa ahadi kisha ukamtosa shauri yako! Nenda kwa Padre/Mchungaji wako atakupa mongozo achana na hizo habari zakuwa mzito, wanawake wengi huwa wanaumwa kabisa.
 
Sikiliza sauti ya ndani. Huo uzito ni ishara tosha, kaa mbali na huo upupu Jombaa.
 
Hii ipo hata kwenye masuala ya ujenzi.ukianza ujenzi wa msingi wa nyumba aje mchungaji kuombea na kuweka kinga au aje mganga kufukia kinga.
Vinginevyo watu wasotea usiku

Wakishaweka mauchawi,basi unashangaa kila ukitaka kwenda sait unakuwa mzito,kisha unapuuza,miaka inakwenda sait hakuna maendeleo, na sio kwamba hela hupati, ni kwamba umepofushwa.

Sasa hapo kwenye kufunga ndoa yako umeshafanyiwa namna. Ili ukwame.. mueleze mchungaji wako au kiongozi wako wa kiroho akusaidie.
Kama nawe ni mlozi wende ukasafishwe kwa mganga.
 
Binafsi sijafunga ndoa kwaiyo sina uzoefu na hali unayokutana nayo ila nahisi inaweza kuwa ile excitement tu anayokua nayo mtu kabla ya tukio kubwa mfano muda mfupi kabla ya kuingia kufanya mtihani wa taifa, siku ya kwanza kufanya mapenzi n.k, kama una uhakika hujakoea kuchagua mke we jikaze funga ndoa mkuu.. mwisho kabisa kama una connection ya kazi yoyote mkuu tupeane shavu mtaani sio poa
 
Hiki ni kichaa tuu cha harusi, ukifanikiwa kufinga ndoa huwa kinaondoka chenyewe.
 
Bro huyo ni shetani anakushawishi,mshinde ee endelea na ndoa
 
Mmh kwahio mwanamke huyo kua amekeketwa ndo kukafanya asimuoe?
 
Mi nilipata situation kama hiyo,na nilivyoforce ndoa mwaka 1 Chali....na ndani ya mwaka huo ilikuwa ni uvumilivu tu😥
Ndo hivyo, ule mlio wa alarm ya kwenye uchumba hulia kwa sauti ndogo lakini ukiingia kwenye ndoa sauti hiyo hiyo inakuwa kubwa isiyovumilika
 
Jitahidi uishinde hio hali siku uje na mrejesho umetoka honeymoon na una enjoy maisha ya ndoa.
 
Unataka kuoa singo maza unategemea nini imekula kwako mjuba
 
Kama Tatizo halipo kwa upande wa Bibi harusi Hilo wazo lako lifute Mara moja.

Pengine ni kauoga tu maana inawezekana ni wale watu waoga wa umati.

Jitie ujasiri na hakika utajipongeza shughuli ikishaisha.

NB:Hii ni kama bado unaona Bibi harusi ni chaguo sahihi kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…