Nataka kukaa mbali na mtoto

Nataka kukaa mbali na mtoto

Aaliyyah

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2022
Posts
19,041
Reaction score
46,239
Natumain wazima kama kichwa Cha habari kinavojieleza.

Nilikuwa kwenye mahusiano na mtu lakini nilikuta tayari anamtoto wa miaka 5 mwenzangu hakuwai Kuishi na mzazi mwenzio na mtoto analelewa Kwa bibi yake, baada ya kunitambulisha yule mtoto kiukweli nilikuwa nampenda sana na mtoto alikuwa Yuko karibu sana na Mimi ni mpole anaadabu sana.

Baada ya muda nikahama mkoa x ila mtoto Kila akiwa na babaake anasema msalimie mama na simu anaomba anipigie niongee nae now nimetengana na baba Kwa sabbu tulizoshindwa kuzitatua na mtoto sahiz anamiaka 8 lakini nikirudi haipiti siku lazima Aje kunisalimia na ananiita mama lakin sioni tatizo najua ni upendo tu.

Kubwa kuliko Wana mahafali madrasa akaja kunipa taarifa na kilasiku huwa anakuja kunikumbusha nisisahau kwenda kutokana na ubusy na kwakuwa ni mtoto Kuna details hakunipa yaani muda wa sherehe na mahitaji mengine nikaamua kumpigia simu babaake kumuuliza aniambie muda Cha ajabu baba Hana taarifa na hakupewa na mtoto na huwa wanaonana sana.

Nimejisikia vibaya nahisi huu ukaribu Sasa utaleta tafrani nataka nikae mbali na huyu mtoto bila kumuonyesha kuwa sipo kbisa na babaake namnagan nimuweke mbali na isimuathiri huyu mtoto?

Na kma sio uamuz mzuri mnaweza kunisahihisha
 
Maskini wala usikae nae mbali,pengine ni vile ulivyokua unampenda amejisikia faraja sana,sio watu wengi wanaweza kuonyesha upendo kwa mtoto au ,watu huhisi kulipa ada na kununua nguo imetosha kumbe kuna zaidi especially kwa hao watoto!

Wewe endelea tu kuwa nae usimtenge gafla atapata sonono,siku zinavyozidi kwenda i hope atakuja kuelewa tu kuwa hauko na baba yake so yeye mwenyewe atajitenga!
 
Back
Top Bottom