Nataka kukopa Shilingi milioni 5 nianze biashara

Nataka kukopa Shilingi milioni 5 nianze biashara

Mkuu,
akizingatia huu ushauri atakuja kukushukuru some time to come,

Ila tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana.
Tatizo vijana wengi wanaamini wanaweza kutoboa kwa kutegemea Mshahara wa Mkewe.

Ila kiuhalisia,
kuipigia hesabu ya Mshahara wa mke msomi ni kujitafutia Kiharusi,presha na mkanda wa JESHI.
 
Kwanza umejiandaa na Side effect za mkopo biashara sio faida tu kuna kuchelewa kupata faida au kufa kabisa nakuishi na take-home ya 100K mwaka mmoja hutaweza himiri.

Minakushauri weka kwenye biashara pesayako mwenyewe ya savingi...save kwelikweli hadi kufikia 4M kwa mwaka unaweza kama huna mke then fanya reserch hasaa biashara isiyohitaji usimamizi mkubwa na iliyo na uwezo wa kukua mfano Carwash wekeza 4M yako mpaka utakapo jirizisha unapata faida yamaana kopa hata 10M wekeza kwelikweli ongeza mtaji kwenye biashara ya kwanza mtaji mwengine wekeza kwenye biashara ya pili hutajuta ukitumia njia hiyo.

Uzuri wa hii hata biashara ikizingua ni pesa yako haiasiri mshahara na ikifanikiwa hata mshahara take-home ikiwa 10,000/= wewe utaishi safi tu.
Kias kwa sababu nilikuwa na mkopo mwingine ambao umeisha, niliwekeza kwenye kilimo na kununua mazao ila sasa mtaji nimeupeleka kwenye ujenz, nataka nikope tena
 
Nataman kuwa na mke ambae sio mtumish, mungu akijalia ntapata awe ananisadia kwenye shughuli zang hizo coz bado sijaoa
Kama una Mke asiye mtumishi muweke kwenye hyo biashara kisha na wewe uwe unaifuatilia kwa karibu. Tofauti na hapo ifanye wewe mwenyewe. Ukiajiri mtu anaweza akakutia hasara halafu ukachanganyikiwa bure! NB: haya yote tuyasemayo kuhusu hasara si lazima yatokee hivyo ila kuna uwezekano Mkubwa kutokea hayo!
 
Nashukuru kwa ushauri kiongoz
Biashara ya duka ni kati ya biashara nzuri sana kama ukifuata misingi yake
1. Hakikisha location ni NZURI
2. Hakikisha bidhaa ZOTE ulizonazo zipo kwenye daftari.
3. Hakikisha duka lisiwe sehem ya utatuzi wa madeni yako kwa maana kutoa pesa hovyohovyo
4. Hakikisha unakagua mwenendo wa biashara angalau kila wiki kwa kupiga mahesabu ya mauzo na bidhaa.
5. USIRUHUSU mchumba wako awe anaingia dukani kuuza.
6. Hakikisha mtoa huduma awe muaminifu na wewe umuamini, tena inatakiwa wewe uwe ni msaidizi na mkaguzi tu, usiruhusu awe na muda wa kutoka bila sababu ya msingi.
7. KUKOPESHA NI KUFUKUZA WATEJA.
Hayo ni yangu mengine jiongeze
 
Well detailed advice, nimeipenda kaka nitaifanyia kaz depply
Inaitwa " a stepping stone business" yaani wafanyabiashara wengi kabla ya kuingia kwenye biashara nyingine walizonazo walianza kwenye hiyo biashara. Vitu vya msingi kuvijua kwenye biashara hiyo

1. Uaminifu na Weledi wa Kijana ni kitu cha kwanza ili ufanikiwe ktk biashara hii tumeshuhudia wafanyabiashara wengi wakianguka na wengine wakiamka tokana na Wasaidizi ktk biashara hizo

2. Faida ni ya uhakika ingawa ni ndogo inayokuwa kwa muda mrefu inabidi uwe mvumilivu sana ili duka likae sawa na mwanzoni uwe na ufuatiliaji wa karibu sana

3. Uchaguzi wa eneo la kufanya biashara nalo ni muhimu. Kwa mfano kuna eneo ambalo hakuna Muajiriwa hata mmoja, sehemu nyingine unakuta Waajiriwa wa kumwaga

4. Ukaguzi, Uchunguzi na Utunzaji kumbukumbu wa mara kwa mara ni muhimu sana itakusaidia kujua maendeleo ya biashara, itakusaidia kubaini mbinu za kibiashara, ville vile itasaidia kujua kama msaidizi ana mapungufu au laa
Unaweza mchunguza hata huyo kijana wako kama ana kauli njema kwa wateja au laa, yuko aggressive au laa kwa kutumia watu wengine ambao wataenda dukani kama wateja

5. Mahusiano mazuri toka kwa Suppliers na upande mwingine Customers ni kitu cha muhimu sana ili ufanikiwe bila kusahau mahusiano na taasisi za fedha Ukiwa na mahusiano mazuri na Suppliers ni rahisi kupata bidhaa nyingi kwa mali kauli upande wa Customers utajua mahitaji halisi ya wateja na wachache utaowakopesha watakulipa timely

6. Teknolojia ni muhimu katika utunzaji kumbukumbu vile vile hivi sasa kuna App maalum za kufanya Manunuzi directly kutoka kwa Manufacturer au Dealer na Software saidizi ktk Stock Traxking na Sales Tracking

7. Mahitaji ya Kisheria, hakikisha huna ugomvi na Serikali na Mamlaka zake kwa kulipa kodi na tozo zote zinazohitaji

8. Wekeza ktk kujifunza na kutaka ushauri. Tafuta Business Consultant akupe ushauri at least kila baada ya miezi 3 fanya nae kikao. Wekeza ktk kujifunza toka kwa wafanyabiashara wenzio. Nilishaona mtu anadaiwa kodi na TRA Tshs 60m lakini baada ya kutafuta Tax Consultant na kuziweka report zake vizuri alilipa Tshs 2.5m

9. Jitofautishe wewe na biashara yako, sio kwa sababu biashara ni yako basi kuwe hakuna mpangilio Baba, Mama, Watoto, Mjomba wanaingia na kutoka dukani kadri watakavyo. Kukiwa na hali kama hiyo wasaidizi dukani hufurahia sana kwani chochote kitakachotokea dukani hawatawajibika. Uhusiano.wako wewe na duka ni faida tuu, hivyo basi chochote utachochukua dukani lazima kiorodheshwe hatimae kilipwe au kikatwe kwenye faida
 
Ushauri kukopa na kwenda kuanzisha biashara ni ufara sana....

Iko hivi biashara ili ufanikiwe inatakiwa uwe umeianza na umeshajua namna ya kuiendesha na umeshajua soko au wateja wako na jinsi gn ya kupambana na changamoto...

Unapokopa itakuwa kama unaongezea mtaji pale unapohic pamepungua hapo ndipo utapojua biashara uiendeshaje na kupata faida..

Lkn usikope na kuanza kununua vifaranga elfu moja wkt hujawahi ata kufuga KUKU mmoja utalia na kusaga meno
 
makato ya mwez ni laki mbili that means utakua anabakia na laki na nusu kwa miezi 30! so kwa akil ya kawaida utategemea zaid biashara mpya kukuendeshea maisha yako plus mshahara wa mfnyakaz na kodi na wakt huo huo biashara kujiendesha! hii itkua ngumu sana (tho its possble)..ushaur wangu fikria fursa ya biashara nyngne kutokana na eneo ulipo(nguo za kiume,kuuza chakula au pub) coz duka la rejareja sidhan kma ni idea nzur kwa situation uliyonayo! then uombe likizo ule mwez wa kwnza wa biashara wote ukae dukan na mfnyakaz wako ili ujue rotation ya biashara yakl! atleast hi itkupa experiance nzur ya kusimamia biashara yako.
 
Mm ni mwalimu npo mbeya mjini na mshahara wang kwa sasa take hom ni kama 350 iv, nataka kukopoa NMB kiasi tajwa kwa ajili ya kufungua kibanda cha mahitaji ya kawaida ya majumbani, location nimepata nzur ila bado najiuliza kama ntatoboa.
NB: nategemea kuajiri mfanyakaz kwa sababu muda mwing wa mchana nakuwa Mazini na jion ndio ntakuwa na muda wa kuwa Kubandani

Naombeni kuwasilisha
View attachment 1226709
wazo lako n zuri ila ur in wrong truck
sikushauri uchukue mkopo wa KUANZIA BIASHARA.... nashauri chukua mkopo kwa ajili ya KUKUZA BIASHARA ....biashara ya duka sio rahs kukurudishia hyo pesa ndan ya miaka 2 na nusu ambapo utatakiwa kulipa milion 6 na zaid......kkumbka duka lina faida za 200,100,50 lakn kuna kodi za TRA,MANSPAA n.k
 
Mtaji nilio nao na fridge na mizani, pamoja na kama 1mil ila biashara ina hitaji kama 7mil hivi, ko naona sina namna nyingine, na kwa kusema niweke mshahara mpaka ufike hata 3mil duu haijawah tokea
Ushauri kukopa na kwenda kuanzisha biashara ni ufara sana....

Iko hivi biashara ili ufanikiwe inatakiwa uwe umeianza na umeshajua namna ya kuiendesha na umeshajua soko au wateja wako na jinsi gn ya kupambana na changamoto...

Unapokopa itakuwa kama unaongezea mtaji pale unapohic pamepungua hapo ndipo utapojua biashara uiendeshaje na kupata faida..

Lkn usikope na kuanza kununua vifaranga elfu moja wkt hujawahi ata kufuga KUKU mmoja utalia na kusaga meno
 
Nalichua wazo lako nilifanyie kaz, niliweke , miongon mwa mapendekezo yang
makato ya mwez ni laki mbili that means utakua anabakia na laki na nusu kwa miezi 30! so kwa akil ya kawaida utategemea zaid biashara mpya kukuendeshea maisha yako plus mshahara wa mfnyakaz na kodi na wakt huo huo biashara kujiendesha! hii itkua ngumu sana (tho its possble)..ushaur wangu fikria fursa ya biashara nyngne kutokana na eneo ulipo(nguo za kiume,kuuza chakula au pub) coz duka la rejareja sidhan kma ni idea nzur kwa situation uliyonayo! then uombe likizo ule mwez wa kwnza wa biashara wote ukae dukan na mfnyakaz wako ili ujue rotation ya biashara yakl! atleast hi itkupa experiance nzur ya kusimamia biashara yako.
 
wazo lako n zuri ila ur in wrong truck
sikushauri uchukue mkopo wa KUANZIA BIASHARA.... nashauri chukua mkopo kwa ajili ya KUKUZA BIASHARA ....biashara ya duka sio rahs kukurudishia hyo pesa ndan ya miaka 2 na nusu ambapo utatakiwa kulipa milion 6 na zaid......kkumbka duka lina faida za 200,100,50 lakn kuna kodi za TRA,MANSPAA n.k
Duu niliwaza kama nategemea mauzo ya 200 to 250k nitakuwa natengeneza walau elfu 15 faida kwa siku ukitoa matumiz
 
Duu kumbe hakunaga kaz rahis, hata wazo tu la biashara ni mbinde namna hii
na hii n hatua ngumu sana katka biashara....haya assume ungekua tayar ushakopa pesa afu ndo unaanza kutafta wazo la biashara .....si ungekua ushaanza kuzitafuna?
 
Back
Top Bottom