Nataka kumiliki Scania R450. Je, pesa itarudi baada ya muda gani?

Nataka kumiliki Scania R450. Je, pesa itarudi baada ya muda gani?

Tabutupu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Posts
13,206
Reaction score
18,549
Nimepata kama mil 100 baada ya kuvuna vanila huko Bukoba. Sasa nahitaji nijiingize kwenye biashara ya usafirishaji na wazo langu ni kununua scania kama kwenye picha

Nimepanga kuanza na moja kutokana na kiasi nilichonacho

Naomba wenye uzoefu, kama biashara ikienda vizuri, kwa mwezi naweza ingiza kiasi gani?
FB_IMG_1592652503708.jpeg

Swali la nyongeza 24 June 2020
Vipi biashara ya kusafirisha
Mafuta vs Mizigo
 
Kwa pesa ya kwanza nakushauri tafuta 113, 124 na kisha zifanyie matengenezo ya kutosha ndipo uweke barabarani.

Tatizo la R420, R440 zinahitaji uwe na akiba walau isiyo pungua 30 millions just for emergency. Pia spare zake ni ghali sana pale SubScania, na hata sisi mafundi tunawachinja sana wamiliki wa R.

Mwisho nikukumbushe tu usisahau kukata bima kubwa yasije yakakutokea kama yule mama.

Pia biashara ya usafirishaji unapoianza ni vyema ukaisimamia mwenyewe kwa ukamilifu na kila hatua, hii itakusaidia kupata uzoefu wa magonjwa ya magari pia jinsi ya upataji mizigo pasipo kupitia madalali.
 
Kwa pesa ya kwanza nakushauri tafuta 113, 124 na kisha zifanyie maengenezo ya kutosha ndipo uweke barabarani. Tatizo la R420, R440 zinahitaji uwe na akiba walau isiyo pungua 30millions just for emergency. Pia spare zake ni ghali sana pale SubScania, na hata sisi mafundi tunawachinja sana wamiliki wa R.

Mwisho nikukumbushe tu usisahau kukata bima kubwa yasije yakajutokea kama yule mama.
Pia biashara ya usafirishaji unapo ianza nivyeme ukaisimamia mwenyewe kwa ukamilifu na kila hatua, hii itakusaidia kupata uzowefu wa magonjwa ya magari pia jinsi ya upataji mizigo pasipo kupitia madalali.
113 na 124 ni roho ya paka. Halafu hazina mambo mengi kwenye mifumo yake kwenye injini.
 
Bima sawa, ila hapo kwenye gharama za matengenezo ndio sijakuelewa kabisa. Nilidhani 113 etc ndio zina gharama zaidi.
Kwa pesa ya kwanza nakushauri tafuta 113, 124 na kisha zifanyie maengenezo ya kutosha ndipo uweke barabarani. Tatizo la R420, R440 zinahitaji uwe na akiba walau isiyo pungua 30millions just for emergency. Pia spare zake ni ghali sana pale SubScania, na hata sisi mafundi tunawachinja sana wamiliki wa R.

Mwisho nikukumbushe tu usisahau kukata bima kubwa yasije yakajutokea kama yule mama.
Pia biashara ya usafirishaji unapo ianza nivyeme ukaisimamia mwenyewe kwa ukamilifu na kila hatua, hii itakusaidia kupata uzowefu wa magonjwa ya magari pia jinsi ya upataji mizigo pasipo kupitia madalali.
 
Scania ya 2012 ni £ 12,000 , tax ya Tanzania and a 21,000,000/=
Trailer flat bed 24,000,000/=

Yanabaki madogo madogo Kama bima na n.k
Faida inategemea unafanya Ipi?! Transit au local. Nakupa mfano: Dar to Rwanda transit cost ni 3,200usd

Wakati huo ukibeba mzigo wa local, mfano Mwanza to Dar ni 70usd kwa tani.
Faida inategemea na schedule yako ya kazi na speed yako.
 
Back
Top Bottom