Nataka kumiliki Scania R450. Je, pesa itarudi baada ya muda gani?

Nataka kumiliki Scania R450. Je, pesa itarudi baada ya muda gani?

Nimepata kama mil 100 baada ya kuvuna vanila huko Bukoba. Sasa nahitaji nijiingize kwenye biashara ya usafirishaji na wazo langu ni kununua scania kama kwenye picha.

Nimepanga kuanza na moja kutokana na kiasi nilicho nacho.

Naomba wenye uzoefu, kama biashara ikienda vizuri, kwa mwezi naweza ingiza kiasi gani?View attachment 1484199

Mkuu,

Nikupongeze sana kwa uthubutu huu.

Hii biashara ni nzuri ila ina changamoto zake za hapa na pale ila ina pesa.

Ili uweze kutoboa kwenye hii biashara jitahidi kumudu jazba zako kwa dereva wako tena hasa akiwa porini, Dereva ndiye mtu anayeweza kukufanya ufanikiwe na kukufanya ufeli mazima.

Trailer zipo za aina mbili,

Flatbed na Skelton

Kwa vile wewe ndiyo unaanza basi nakushauri uchukue flatbed kwa sababu kazi zote utabeba. Vilevile uchukue Trailer yenye (axles za BPW).

Kampuni zinazozalisha hizo trailer zipo nyingi hapo mjini, Superdoll, Simba na wengineo, Nashauri ununue trailer za mtumba.

Kikazi,
Kuna trip za local( za ndani)
Kuna trip za transit ( Nje ya nchi)

Trip za ndani sikushauri uzifanye kwasababu zinachosha gari na magurudumu. Ni bora ufanye hizo za Transit tu, tena za Dar - Lubumbashi tu.

Trip za Dar - Lubumbashi hazichoshi gari ingawa gari inachukua mwezi mzima au zaidi lakini pesa yake unaiona, Gari inaenda na mzigo na inarudi na mzigo (Copper)

Sasa ili uweze kufanya hizo trip za transit kwa mtu wa gari moja, nakushauri ufanye joint venture na mtu mwingine ambaye ana gari nyingi ili uweze kupata c28 ya TRA na hii itakusaidia kujikusanya na kujifunza mchezo.

Kwanini nasema hivyo, sijajua mfuko wako ukoje ila kuna mlolongo wa makadirio ya kodi, kukata vibali vya Zambia na mambo mengine, kwa gari moja ni story tu.

Mkuu, Magurudumu ya gari yako hakikisha umenote zile serial number na uwe mfwatiliaji wa kuyakagua kila baada ya trip.

Dereva mtaji wake ni Diseal na Magurudumu, akiishiwa huko njiani anayanywa fasta na yanauzika sana hapo Tunduma au huko Mpika.

Punguza wanawake (Mademu) magari ni kama Majini hayapendi uchafu wa mwili, na pia dereva asikuzooee sana maana wanakuwaga na vinasaba vya kiswahili unaweza kujikuta yeye ndiye kawa boss na wewe ukawa mfanyakazi wake. Zingatia Services ya gari, usifuge magonjwa kwenye gari!

Naomba niishie hapa,
Cheza na dola mkuu.

Shukrani
 
Bima sawa.. ila hapo kwenye gharama za matengenezo ndio sijakuelewa kabisa.. nilidhani 113 etc ndio zina gharama zaidi.
Kwanza spare zake ni nyingi hadi kwenye screpa unazipata.
Pili ni ngumu na roho ya paka ikiwa utazifanyia matengenezo kwa wakati.
Tatu huku mtaani sisi mafundi tunawachinja taratibu ya mazowea.
Achana na P mkuu, huo ndio ushauri wangu
 
Mimi nilianza biashara ya Usafirishaji miaka kama 10 iliyopita. Hata sasa hivi nafanya usafirishaji mizigo sana tu local ila kwakua imenibidi(Niko kwenye supply business) kwahiyo swala la kuwa na Gari linasaidia kupunguza gharama ya bidhaa nnazouza.

Ila kama ingekua ni uamuzi wangu nisingekuja kumiliki gari la mizigo tena KAMWE

Hio mil 100 tafuta biashara nyingine sio ya kuwa na gari moja.Ni Risk kubwa mno unajitafutia .Hakuna cha bima wala upuuzi wa bima. Utakufa siku sio zako

Ukiwa na magari mengi inasaidia kugawanyisha Risks. Madereva nao dahh kila siku ni kutishana na bastola mezani na kutiana lockup

Hakuna biashara pasua kichwa kama hii katika biashara zote nilizokwisha kufanya

Usione kina Usangu, Overland wanazungusha chuma tu kisauzi ila hii biashara sio mchezo.

Ungekua na mtaji wa Billion plus ningekushauri hata uanze kupambana na kina Sham Nunu na hao underdogs wengine na nisingekushauri huko kwenye Mascania. Howo anafanya vizuri sana saivi anaenda ligi za kina Daf/Volvo.
 
Wengine wanasema pengine alikuwa anatimia gear za juu kwa hiyo mzigo wote ulikuwa inategemea break. Kama angetumia gear nzito maana yake engine ingesupport sehemu ya mzigo.
Konda wa hilo lori alisema tatizo ilikuwa upepo si unajua tena malori break zake zinaendana na upepo sasa mtungi ulikuwa tupu
 
Kuna wachangiaji watatu, Zacha, geomax na nktlogistics, michango yao nimependa wana uzoefu mzuri. Nashauri soma Tena na Tena michango yao Kisha watafute personally.

Baada ya mafanikio pia usisite kuja kuleta mrejesho ili kuwatia moyo watafutaji wapya.
 
Huwezi fananisha gari mpya na used ,Howo ni gari nzuri na cost effective
Maisha yake mafupi sana pamoja na upya wake, Scania iliyotembea km lak 5 na Howo mpya kabisa probably zinaweza kaa kwenye level moja for Short time tu ila nina uhakika baada ya miaka 5, HOWO itakuwa juu ya mawe scania hata wazo hilo haina, mjukuu wako ataikuta
 
Back
Top Bottom