mjingamimi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2015
- 42,209
- 51,004
Endelea na KILIMO.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi nilianza biashara ya Usafirishaji miaka kama 10 iliyopita. Hata sasa hivi nafanya usafirishaji mizigo sana tu local ila kwakua imenibidi(Niko kwenye supply business) kwahiyo swala la kuwa na Gari linasaidia kupunguza gharama ya bidhaa nnazouza.
Ila kama ingekua ni uamuzi wangu nisingekuja kumiliki gari la mizigo tena KAMWE
Hio mil 100 tafuta biashara nyingine sio ya kuwa na gari moja.Ni Risk kubwa mno unajitafutia .Hakuna cha bima wala upuuzi wa bima .Utakufa siku sio zako
Ukiwa na magari mengi inasaidia kugawanyisha Risks. Madereva nao dahh kila siku ni kutishana na bastola mezani na kutiana lockup
Hakuna biashara pasua kichwa kama hii katika biashara zote nilizokwisha kufanya
Usione kina Usangu,Overland wanazungusha chuma tu kisauzi ila hii biashara sio mchezo.
Ungekua na mtaji wa Billion plus ningekushauri hata uanze kupambana na kina Sham Nunu na hao underdogs wengine na nisingekushauri huko kwenye Mascania. Howo anafanya vizuri sana saivi anaenda ligi za kina Daf/Volvo
Tanzania yapo magari mangapi?? yote yametumbukia ? biashara zote zina risk mkuu, na zote zina risk za kuhatarisha na kuua mtaji wote , ndio maisha yalivyo, tuna options mbili tu either tufanye au tusifanye
View attachment 1484713
Hio juu ni Fuso Tandam
View attachment 1484714
Hio juu ndio Scania kipisi ya mizigo.
Hapa umeelewekaMkuu,
Nikupongeze sana kwa uthubutu huu.
Hii biashara ni nzuri ila ina changamoto zake za hapa na pale ila ina pesa.
Ili uweze kutoboa kwenye hii biashara jitahidi kumudu jazba zako kwa dereva wako tena hasa akiwa porini , Dereva ndiye mtu anayeweza kukufanya ufanikiwe na kukufanya ufeli mazima.
Trailer zipo za aina mbili,
Flatbed na Skelton
Kwa vile wewe ndiyo unaanza basi nakushauri uchukue flatbed kwa sababu kazi zote utabeba. Vilevile uchukue Trailer yenye (axles za BPW).
Kampuni zinazozalisha hizo trailer zipo nyingi hapo mjini, Superdoll, Simba na wengineo, Nashauri ununue trailer za mtumba.
Kikazi,
Kuna trip za local( za ndani)
Kuna trip za transit ( Nje ya nchi)
Trip za ndani sikushauri uzifanye kwasababu zinachosha gari na magurudumu. Ni bora ufanye hizo za Transit tu, tena za Dar - Lubumbashi tu.
Trip za Dar - Lubumbashi hazichoshi gari ingawa gari inachukua mwezi mzima au zaidi lakini pesa yake unaiona, Gari inaenda na mzigo na inarudi na mzigo (Copper)
Sasa ili uweze kufanya hizo trip za transit kwa mtu wa gari moja, nakushauri ufanye joint venture na mtu mwingine ambaye ana gari nyingi ili uweze kupata c28 ya TRA na hii itakusaidia kujikusanya na kujifunza mchezo.
Kwanini nasema hivyo, sijajua mfuko wako ukoje ila kuna mlolongo wa makadirio ya kodi, kukata vibali vya Zambia na mambo mengine, kwa gari moja ni story tu.
Mkuu, Magurudumu ya gari yako hakikisha umenote zile serial number na uwe mfwatiliaji wa kuyakagua kila baada ya trip.
Dereva mtaji wake ni Diseal na Magurudumu, akiishiwa huko njiani anayanywa fasta na yanauzika sana hapo Tunduma au huko Mpika.
Punguza wanawake (Mademu) magari ni kama Majini hayapendi uchafu wa mwili, na pia dereva asikuzooee sana maana wanakuwaga na vinasaba vya kiswahili unaweza kujikuta yeye ndiye kawa boss na wewe ukawa mfanyakazi wake. Zingatia Services ya gari, usifuge magonjwa kwenye gari!
Naomba niishie hapa,
Cheza na dola mkuu.
Shukrani
Mkuu mie nakushauri anza na Fuso Tandam ndio utapiga pesa zaid. Ninakushauri hvo kwa kuwa hapa home tuna Scania tatu na Fuso mbili ila Fuso ndio zinapiga kazi kuliko Scania.
Na pia km ni Scania kwa wewe unaeanza sikushauri kwa kuwa ni sumbufu sana hasa ikishaanza kuchoka. Scania za kukutoa umaskini ni zile model za kizaman.
Na pia wanaokushauri kuhusu magari ya abiria naomba usiwasikilize kabisaa, maana yana changamoto nyingi sana. Mie binafsi nina Nissan Caravan mbili ila ni kichefu chefu kitupu.
NB: nimekushauri kutokana na uzoefu wangu wa kuishi na hayo magari kwa muda mrefu.
Ina maana gharama ya mafuta haizidi laki tatu?Kama unavyojua kwny utumiaje wa mafuta Fuso inatumia kidogo zaid kulinganisha na kipisi, pia Fuso Tandam inapakia had tani 16 na ikipita mizan sio shida.
Ila kipisi ukipakia tani 16 lazima upigwe faini kwny mizani, kuna kitu wanaita GVT km sikosei yaan uzito wa gari ikiwa tupu kwa Kipisi inakuwa nzito zaid. Ndio maana kwny mizan inazid
Sie sana Tandam zinapga kazi kwenda kupeleka mahindi huko kwa Usukumani. Gari inakodishwa hadi 1.6 milion kwa trip na ukitoa gharama ya kila ktu had kulipa vijana inabaki hadi 1.1 milion.
Na gari ndani ya siku mbili tu inakuwa imeshaenda na kugeuza.
Mkuu mie ni mvivu sana ku-type text ndefu ila nadhan nmejitahid kadri ya uwezo wangu
Mkuu mambo yalivyo tofauti kabisa na wewe unavyofikiria, kila biashara inarisk zake.Inategemea mkuu.
Usifanye kitu kwa kuwaiga wengine,fanya kitu pale inapobidi kufanya kutegemea na uwezo wako.
Biashara ya magari haina urafiki na mtu maskini,risks zake ni nyingi sana na zote zinahitaji pesa.
Matajiri wanaiwezea kwa sababu wanakuwa nazo nyingi so ikianguka moja wala hashtuki anajua atazitumia zingine na kupata pesa za kuiokoa iliyoanguka.
[emoji1][emoji1]mtoa mada kama kweli kilimo cha vanilla kimeweza kukupatia mil 100 nakushauri endelea tu na kilimo
kuhamia kwenye biashara ambayo huijui tena ya magari hii inaweza kuwa ndo downfall yako na baadaye kwenda kwenye uzi uleeeee wa waliowahi kushika pesa ndefu halafu gafla zikapotea
hili ni wazo tu lakini maana kuna wengine wameweza kubadili biashara pia wakafanikiwa
Kweli ndugu Tabutupu tunaomba utupe muongozo umetoboa vipi kwenye vanillaTafuta Tandam kisha ingia kwenye biashara ya kupeleka mahindi/ng'ombe/mbuzi/mchele/nyanya/viazi/ndizi/maharage Dar.
Kwa heshima na taadhima nakuomba Tabutupu uje na uzi unao eleza kwa kina hiyo vanila iliyofanikisha kukupa 100m ili tujifunze na sisi.
Upande wa services Fuso inakuwa chini kidogo, ukilinganisha na Kipisi, japokuwa Scania kipisi ukiifunga unasahau kabisa kuifungua tena hata ukichanganya na spare ambazo sio OG kabisaupande wa service je?? Tandam vs kipis.. gharama ni sawa au kuna mwenye afadhal?
Hiyo ni kutokea hapa Singida kwenda huko Musoma n.k, tena kupitia njia za vumbi (Shortcuts)Ina maana gharama ya mafuta haizidi laki tatu?
Nimepata kama mil 100 baada ya kuvuna vanila huko Bukoba. Sasa nahitaji nijiingize kwenye biashara ya usafirishaji na wazo langu ni kununua scania kama kwenye picha.
Nimepanga kuanza na moja kutokana na kiasi nilicho nacho.
Naomba wenye uzoefu, kama biashara ikienda vizuri, kwa mwezi naweza ingiza kiasi gani?View attachment 1484199