Nataka kumiliki Scania R450. Je, pesa itarudi baada ya muda gani?

Nataka kumiliki Scania R450. Je, pesa itarudi baada ya muda gani?

Wakuu,

Niseme machache.

Marehemu Rugemalila Mutahaba aliwai kusema maneno haya, naomba kumnukuu" Ukifanya biashara na haikupi changamoto basi hiyo biashara haina faida kwako achana nayo"

Akaenda mbali tena, Mjasiriamali wa kweli ni yule anayebadilika badilika huwez kukomaa na biashara ya aina moja tu kwa wakati wote, Mwisho wa nukuu.

Hii biashara ina changamoto zake lakini ina pesa, sehemu yeyote yenye changamoto pesa inapatikana hapo.

Scania 113M ni horse nzuri lakini ina mapungufu yake, hii gari haitumii umeme mwingi na ulaji wake wa diseal ni mkubwa, lakini pia haina Kitanda.

Kwa mfano trip ya Dar -Lubumbashi, halafu Lubumbashi - Dar hiyo gari inatumia diseal lita 2400 na muda mwingine mpaka 2500 wakati scania 114L, 124L inakula lita 2200.

Kwa ushauri wangu, unaweza kuanza na scania 114L yenye horse power 380 cabin ndogo. Au ukishindwa sana basi chukua DAF XF 95 manual, (camis engine)

Adjustments.jpg

Adjustments.jpg

Kama nilivyosema awali, Dereva ndiye mtu muhimu sana atakaye kutoa hapo ulipo mpaka sehemu uliyopanga wewe kufika. Tatizo kubwa kwenye hii biashara wamiliki wengi wanamchukulia dereva kama barmaid.

Dereva mzuri unampataje? Madereva wazuri siku zote wanaibwa kutoka kwenye makampuni mengine.

Tengeneza mofolojia ya kazi yako vizuri, kwa mfano kuna kampuni X inamlipa dereva mileage ya kwenda Lubumbashi na kurudi dar TSHS 1milion

Kiaje? Dereva anapewa shs 500k kwenda Lubumbashi na anavyoingia Mgodini kupakia copper unampatia dola 100, akirudi dar unampa shs 300k kama return mileage. Sasa dereva kama huyo kwanini asiheshimu kazi na kutunza gari lako vizuri..!

Kwenye hii kazi reporting ni muhimu sana, mwenye mzigo wake anataka kujua gari iko wapi na imelala wapi? Sasa ili uweze kwendana na hii ari huna budi kutengeneza Kanuni ambayo itakuwa kama katiba ya kazi ofisini kwako.

Dereva aanze safari saa moja asubuhi na ikifika saa kumi na mbili jioni apaki gari atafute guest alale na atume ujumbe kwako kukupa report. ( Kuwa mkali sana kwa dereva anayepuuzia hili)

Madhara ya kutembeza gari usiku ni makubwa sana na yanaweza kukufilisi kabisa na ukajuta kwanini uliingia kwenye hii biashara ya magari kama wanavyoelezea wadau hapo juu.

Breakdown, jitahidi sana kuepuka hitilafu za njiani, funga spare za uhakika ambazo utaweza zipata sub-scania au kwenye maduka mengine ambayo yako vizuri.

Na unapopata breakdown najua kichwa kinawaka moto na pressure inakuwa juu, jitahidi sana kujicontrol, pokea simu ya agent aliyekupakilisha mzigo au mteja mwenyewe mwambie ukweli na umpe uhakika wa usalama wa mzigo wake na uhakika wa kutoka hapo ulipo nasa.

Kutokupokea simu za hao watu kutakuharibia sana na siku nyingine utashindwa aminiwa na ukizingatia ndiyo kwanza unaanza.

Kwenye hii biashara tuna utatu mtakatifu, ambao ni Dereva, Agent / Wakala wa mizigo na Fundi wako wa gari, Hawa watu ishi nao vizuri, kuwa nao karibu kushindwa mchepuko wako.

Chonde chonde usiruhusu lori lako kubeba mkaa, (kama ni kagunia kamoja basi akamwagie maji ndiyo akabebe)

Rate za mizigo sokoni huwa zinabadilika kutoka na ari ilivyo kwa wakati huo na kabla ya kumpatia agent nyaraka zako za gari basi jiridhishe kwa kufanya utafiti kidogo wa bei maana nao ni watafutaji kama wewe.

Shukrani sana!

Muwe na jumapili njema iliyobarikiwa
 
Mkuu sorry,hiyo fuso tandem inapatikana kwa bei gani hapa tanzania ikiwa used na haijachoka?
Mkuu sina uhakika na bei ila niongelee upande wangu huwa tunanunua Fuso ya kawaida yan single diff ambayo inakuwa bado nzma kabsa kuanzia milion 22 hadi 28, halafu tunaipeleka garage Moshi kwenda kuongeza chassis na kuwa Tandam.

Pia inarembwa na kufanyiwa kila kitu hadi ikitoka hapo inakuwa km mpya. Cost zote inaweza kusimamia milion 42 hadi 50 na gari inakuwa imesimama balaa

NB: Hiyo cost ya milion 42 had 50 ni kuanzia gharama ya kununua gari hadi kufanyia kila ktu.
 
Yaani mimi kila nikimkumbuka yule mama ambaye lori lake lilitumbukia mto wami nakosa hamu kabisa ya magari
Mama alilia kaa mtoto kwa sbb alikuwa nayo moja kama dawa, ila vyuma pasua kichwa na vikikubali unapiga pesa hadi basi
 
Upande wa services Fuso inakuwa chini kidogo, ukilinganisha na Kipisi, japokuwa Scania kipisi ukiifunga unasahau kabsa kuifungua tena hata ukichanganya na spare ambazo sio OG kabsa
Shukran, kwa mtu anae anza moja kabisa unamshauri achukue ipi kati ya Tandam na kipisi?
 
Mkuu sina uhakika na bei ila niongelee upande wangu huwa tunanunua Fuso ya kawaida yan single diff ambayo inakuwa bado nzma kabsa kuanzia milion 22 hadi 28, halafu tunaipeleka garage Moshi kwenda kuongeza chassis na kuwa Tandam.

Pia inarembwa na kufanyiwa kila kitu hadi ikitoka hapo inakuwa km mpya. Cost zote inaweza kusimamia milion 42 hadi 50 na gari inakuwa imesimama balaa

NB: hyo cost ya milion 42 had 50 ni kuanzia gharama ya kununua gari hadi kufanyia kila ktu.
Ni cheaper kidogo chini ya kipisi
 
Mkuu mm sio mtaalamu wa magari wala sijawahi kufanya biashara ya magari lakini nimeukubali sana ushauri wako.
Watu wanadanganyana sana mitaani kuhusu biashara za magari wakidhani ni rahisi kama wanavyofikiria.

Ni nzuri sana na ina return tamu tu ila ni biashara ya mtaji mkubwa sana.

Fikiria ukiwa unafanya biashara ya Mil70 halafu una mzigo ndani dukani na ghalani au pengine na mzigo mwingine uko kwa wateja. Risk ni ndogo mno ya kukaanga mtaji

Ila biashara ya Magari ni kwamba Mil70 yote unaituma barabarani kwa kumuamini mtu mmoja tu(dereva) bado factors zingine hapo za madereva wengine/ubovu wa barabara/ ubovu wa gari unaweza kujikuta Mil70 yote umeikaanga kwa usiku mmoja na kesho yake unaamka na madeni ya Mil30. Ndo kilichomkuta yule mama wa Mto Wami

Hii biashara ni sawa na kilimo mtu unalima eti mtaji mil70 wote unaufukia chini halafu unategemea Mungu hela ziote na zikae miez yote labda 9 mpaka kukomaa zikuletee faida. Kuna mambo mengi sana yanaweza kutokea yaliyo nje ya uwezo wako ndomaana ni bora kufanya biashara hii ukiwa liquid kweli kweli sio kwa hela za kuunga unga
 
ooh sawa kumbe sio bei kubwa kivile
Mkuu sina uhakika na bei ila niongelee upande wangu huwa tunanunua Fuso ya kawaida yan single diff ambayo inakuwa bado nzma kabsa kuanzia milion 22 hadi 28, halafu tunaipeleka garage Moshi kwenda kuongeza chassis na kuwa Tandam.

Pia inarembwa na kufanyiwa kila kitu hadi ikitoka hapo inakuwa km mpya. Cost zote inaweza kusimamia milion 42 hadi 50 na gari inakuwa imesimama balaa

NB: hyo cost ya milion 42 had 50 ni kuanzia gharama ya kununua gari hadi kufanyia kila ktu.
 
Shukran, kwa mtu anae anza moja kabisa unamshauri achukue ipi kati ya Tandam na kipisi?

Kwa sasahivi Kipisi hakina dili na ndio maana unaona vipisi vinaisha mtaani vyote vinabadilishwa kuwa mende

Yaan mzigo unaobebwa na tandam unazid mzigo wa kipisi(Tanroads hao) ila yule wa kipisi anatumia gharama kubwa zaid. Yaan vipisi ule urefu uliowekwa na Tanroads na limit ya GVM mizani imekua inakata saivi wa Tandam anatajirika, Kipisi faida yake labda kiwe kinavuta Mtoto(Pulling) sio kipisi kavu au rudisha workshop Ongeza excel ya pili kiwe Mende ubebe mzigo mkubwa
 
Inategemea mkuu.
Usifanye kitu kwa kuwaiga wengine,fanya kitu pale inapobidi kufanya kutegemea na uwezo wako.
Biashara ya magari haina urafiki na mtu maskini,risks zake ni nyingi sana na zote zinahitaji pesa.
Matajiri wanaiwezea kwa sababu wanakuwa nazo nyingi so ikianguka moja wala hashtuki anajua atazitumia zingine na kupata pesa za kuiokoa iliyoanguka.
Mkuu , akili yako inakoishia sio kila mtu anaishia hapo hapo , endapo kila mtu angesubiri awe na uwezo wa kununua gari 5 ndio aanze leo hata kwenda kwenu isingewezekana , usafiri usingekuwepo

Watu walianza biashara na magari mengi wanahesabika , wengi ni moja mbili tena wanaanzia kwenye vi diana canter anapanda mdogodogo , wewe kama kwako ni nzito liache kwa mwenye ubavu nalo
 
Mkuu mambo yalivyo tofauti kabisa na wewe unavyofikiria,kila biashara inarisk zake.

kuna mtu anaroli moja tu ama mawili na mambo yanaenda.

Eti kwa sababu kuna ndege imeanguka ikateketea basi mwenye wazo la kuanzisha biashars ya anga ahairishe!!?
Roli limetumbukia mtoni basi watu wasifanye biashara ya maroli kisa kuna roli liliingia mtoni!!?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hii dunia ina mengi mkuu
 
Sham Nunu ni nani maana jamaa ana magari kama YOTE ya Mizigo.

Chalii tu mmoja alikua na kamtaji kidogo na proposal nzur kaongea na Sinitruck wakampa Gar 60 za kuanzia za mkopo unapeleka rejesho kila mwezi

hizi program zipo nyingi hata TATA wanazitoa kuanzia bas za abiria mpaka Trucks za mkopo unafanyia kaz kwa mkataba kwa miaka kadhaa au mwaka unalipa mdogo mdogo ndo inakua yako
80E8676C-5A28-47E3-993D-1B1AD8E17AE0.png
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Haya mkuu wewe kanunue hakuna mtu aliyekupangia matumizi ya pesa yako.
Ila humu tunapeana ushauri tu.
Kama unaona ni sahihi kubahatisha vihela na kwenda kununua lori ni hiari yako sioni sababu ya kuwa na hasira.
Chukua tu vihela vyako vya NSSF ukanunue lori ruksa.
Mkuu , akili yako inakoishia sio kila mtu anaishia hapo hapo , endapo kila mtu angesubiri awe na uwezo wa kununua gari 5 ndio aanze leo hata kwenda kwenu isingewezekana , usafiri usingekuwepo

Watu walianza biashara na magari mengi wanahesabika , wengi ni moja mbili tena wanaanzia kwenye vi diana canter anapanda mdogodogo , wewe kama kwako ni nzito liache kwa mwenye ubavu nalo
 
Kwa sasahivi Kipisi hakina dili na ndio maana unaona vipisi vinaisha mtaani vyote vinabadilishwa kuwa mende

Yaan mzigo unaobebwa na tandam unazid mzigo wa kipisi(Tanroads hao) ila yule wa kipisi anatumia gharama kubwa zaid. Yaan vipisi ule urefu uliowekwa na Tanroads na limit ya GVM mizani imekua inakata saivi wa Tandam anatajirika, Kipisi faida yake labda kiwe kinavuta Mtoto(Pulling) sio kipisi kavu au rudisha workshop Ongeza excel ya pili kiwe Mende ubebe mzigo mkubwa
sipungizi wala kuongeza kitu hapa.. acha nguvu zielekee kwenye tandam
 
Gari ya mizigo/biashara kwa beginner yeyote usijelogwa ukanunua used bongo , usijelogwa .. nunua used bongo ikiwa tayari ww Ni expert

Hahaaaa nawaonaga wastaafu wengi sana wanavyokufa mapema baada ya Fuso wanazonunua Makambako mil 11 kula mzinga halaf hana hata sent tano ndani anapaki machuma gereji vijana wanaanza kujiibia spea mdogo mdogo
 
sipungizi wala kuongeza kitu hapa.. acha nguvu zielekee kwenye tandam

Mimi hii kitu naijua nje ndani yani mkuu kuanzia kuendesha nilijipatia uzoefu najua mipigo ya madereva najua faida najua vimeo

Na ni kweli inawezekana kuanza na gari moja mie nilianza na Tani 2 ya Mazda Titan miaka Mingi nikaja Kenta 3.5 Fuso Tandam/Kipisi ambacho saiz ni Mende na nna Semi za Howo . Mungu akisaidia ntatafuta Pulling ila sio Scania
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Haya mkuu wewe kanunue hakuna mtu aliyekupangia matumizi ya pesa yako.
Ila humu tunapeana ushauri tu.
Kama unaona ni sahihi kubahatisha vihela na kwenda kununua lori ni hiari yako sioni sababu ya kuwa na hasira.
Chukua tu vihela vyako vya NSSF ukanunue lori ruksa.
I'm in my mid 20's bro , kusubiri pesa ya NSSF kama ningekua mwajiriwa probably ni miaka 30 ijayo, nimeanza tafuta pesa kama mfanya biashara, nimepata na nimepoteza sana vile vile , i know the good the bad and the ugly side of business mkuu

Ngozi nyeusi hua tunafeli sana kwenye eneo la usafiri Kwasababu moja tu kuu tunaichukulia kama "SIDE HUSTLE" and not business kama unavyo treat duka lako hapo tegeta , lazima ufeli tu , unanunua gari hujui unaenda fanyia nn. unasubiri kudra za Mwenyezi Mungu tu liwalo na liwe ..utafeli

inapofikia mtu anafika this stage kwenye vizazi vyetu hv tambua keshafanya research ya kutosha , ana uhakika wa mizigo ya kutosha probably ameshaenda sub scania akala nao kandaras wampigie service gari zake au kampuni yeyote reputable ifanye maintenance ya gazi zake , ulinzi wa gari nikiwa na maana ya GPS na vikoro koro vyake vyote etc etc etc etc mkuu..so mkuu usichukulie kiwepesi tu kama unavyo liona wewe
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Haya mkuu wewe kanunue hakuna mtu aliyekupangia matumizi ya pesa yako.
Ila humu tunapeana ushauri tu.
Kama unaona ni sahihi kubahatisha vihela na kwenda kununua lori ni hiari yako sioni sababu ya kuwa na hasira.
Chukua tu vihela vyako vya NSSF ukanunue lori ruksa.
Mimi hii kitu naijua nje ndani yani mkuu kuanzia kuendesha nilijipatia uzoefu najua mipigo ya madereva najua faida najua vimeo

Na ni kweli inawezekana kuanza na gari moja mie nilianza na Tani 2 ya Mazda Titan miaka Mingi nikaja Kenta 3.5 Fuso Tandam/Kipisi ambacho saiz ni Mende na nna Semi za Howo . Mungu akisaidia ntatafuta Pulling ila sio Scania
Soma hapo dengue
 
Back
Top Bottom