Kuna aina mbili za biashara
mosi unaweza safirisha bidhaa zako mwenyewe, mbili bidhaa za watu wengine
mfano , gari inatoka dsm kwenda mikoan huko ikifika huko wakati wa kurudi unanunua bidhaa kule unaleta huku kuja kuuza (mazao ya chakula asilimia kubwa) mfano huko moshi, unapeleka mzigo wakati wa kurudi unaenda west kule unapakia viazi (wanaviita viaz vya west Kilimanjaro) kuleta dsm
gharama za usafiri kuleta huo mzigo kutoka kule hadi hapo sokoni mabibo ni around 1.2mil hadi 1.5 mil (sina uhakika sana) hiyo unaiingiza hivyo hivyo kwenye hesabu lako la gari (gari yako ila unalipa), lakn pia kwenye viaz kuna faida kati ya lak 5 hadi 1.5 mil inategemea na soko lilivyo so unapiga Huku na Huku(hela ya usafiri umepata+faida ya mzigo uliyoleta) viaz vya west havikaagi hapo sokon, fasta tu vinaisha..gari kulala pale n mara moja moja sana , this is how you maximize your profit , ikitoka hapo inauma mzigo inarud Moshi, ikishusha inauma tena mzigo mwingine inakuja , iwe nyanya iwe karoti iwe sijui nn unapakia unakuja uza , kazi yako kubwa wewe na dereva zako/wako ni kuhakikisha mnakula vizuri na hawa wenye mizigo huku gari ikifika hamna kukaa hapa mjini na ikiwa kule hamna kukaa labda kama iko service tu
ukienda mbeya nako hvyo hvyo, Nenda uyole kule pakia zako mzigo njoo uza , sema huko kuna mizigo mingi sana ya kuja dsm(ya watu)...mingi mno na ina pesa nzuri tu, uchaguzi ni wako tu