Mimi nilianza biashara ya Usafirishaji miaka kama 10 iliyopita. Hata sasa hivi nafanya usafirishaji mizigo sana tu local ila kwakua imenibidi(Niko kwenye supply business) kwahiyo swala la kuwa na Gari linasaidia kupunguza gharama ya bidhaa nnazouza.
Ila kama ingekua ni uamuzi wangu nisingekuja kumiliki gari la mizigo tena KAMWE
Hio mil 100 tafuta biashara nyingine sio ya kuwa na gari moja.Ni Risk kubwa mno unajitafutia .Hakuna cha bima wala upuuzi wa bima .Utakufa siku sio zako
Ukiwa na magari mengi inasaidia kugawanyisha Risks. Madereva nao dahh kila siku ni kutishana na bastola mezani na kutiana lockup
Hakuna biashara pasua kichwa kama hii katika biashara zote nilizokwisha kufanya
Usione kina Usangu,Overland wanazungusha chuma tu kisauzi ila hii biashara sio mchezo.
Ungekua na mtaji wa Billion plus ningekushauri hata uanze kupambana na kina Sham Nunu na hao underdogs wengine na nisingekushauri huko kwenye Mascania. Howo anafanya vizuri sana saivi anaenda ligi za kina Daf/Volvo