Nataka kumiliki Scania R450. Je, pesa itarudi baada ya muda gani?

Nataka kumiliki Scania R450. Je, pesa itarudi baada ya muda gani?

Ahsante.
Kama ninakodisha kwako wewe sasa Danpol kutoa viazi huko west kuleta dar.
Nakulipa ndo hiyo 1.2m mpaka 1.5m.
Na ile mizigo ya kuokota njiani inaingia kwenye hesabu yangu au yako?
Na nikikodisha hiyo gari nakulipia dar nikishashusa mzigo wangu au?

Unayekodisha gari mizigo ya kuokota hakuhusuuu posho ya deree na kidogo anapelekewa tajiri kama deree anajielewa
 
Lake Oil ni mali ya Ally Awadhi , mtoto wa mmiliki wa Azania , Ridhiwan hahusiki hata kidogo, overland Carries ni mali ya ndugu wa Ally, wote watoto wa mmiliki wa Azania group
Sawa ndio watu wanavyojua hata Mali za Bakhresa wanasema zote ni zake lakini Behind the scene wenyewe wanajua mali zao!!
 
Unayekodisha gari mizigo ya kuokota hakuhusuuu posho ya deree na kidogo anapelekewa tajiri kama deree anajielewa
Hii naweza kataa naweza kubali

1.Siku ya kwanza mizigo ya njiani aliyekodi gari alilipa yeye wale madalali wa mizigo njiani na pesa tulimlipa yeye.
Na kuna siku akalalamika kwamba angekuwa na tandam angepiga sana pesa.
Maana yake ni kuwa ile pesa ni yake.

2.Hii siku tulimlipa Tanboy japo mkodishaji alikuwa anahakikisha mizigo ikishushwa.

Sasa scenarios hizo 2 zikanichanganya.

Na ni gari za mama mmoja aliyekodi na mizigo yake ni midogo mno midogo mno kiasi kwamba gari linajazwa na mizigo ya njiani (kwa kuwa mie nimepanda mara nyingi gari yake huwa ananiambia mapema tu "jumanne nitakuwa na gari fuso hapo nitapita mapema sana mizigo yako niachie mdogo wangu nipate hela ya sabuni"

Siku moja nilikuwa na mzigo mkubwa mno lile gari nililijaza mie nduyo nikaona ujinga sasa kwa nini na mie nisijipange kimtaji na nikakodi gari.
 
Kweli,Ila ni kukomaa tu lakini madereva ni pasua kichwa.anakwambia kapata tani tano kumbe ana tani saba.
Mimi najua sana hii michezo.mzee wangu alikua na maroli tisa lakini sahivi kabaki na mawili tu.
Ila yote kwa yote ukikomaa na hii biashara inakutoa,kikubwa ni kuomba mungu tu.
Kwani hamna ndugu au watoto wa ndugu zako ambao wana uwezo wa kutembea na gari au kuendesha gari?

Maana ndugu anaweza kuwa na aibu kidogo na hata kama akiiba bas ataiba kidogo.
 
Lake Oil ni mali ya Ally Awadhi , mtoto wa mmiliki wa Azania , Ridhiwan hahusiki hata kidogo, overland Carries ni mali ya ndugu wa Ally, wote watoto wa mmiliki wa Azania group

Mimi kwa Uzoef wangu sijawahi kuelewa hii habari ya kumuhusisha Riz na LakeGroup

Lake Group ni ya Omar Awadh familia nzito tu kasomeshwa USA karud bongo hakutaka kufanya kazi kampuni ya babaake

Babaake ni Edha Awadh mmiliki wa Mikoani Traders(Brand name Azania) na wana kitengo chao cha Trucking kwaajili ya bidhaa zao Mikoani Trucking. Hii Azania saiv inaendeshwa na Fuad Edha mdogo wake Omar Edha Awadh (Lake Group)

Wakati huo huo Baba Yao kabakia Overland Logistics sioni uhusiano na familia ya JK
 
Hii naweza kataa naweza kubali

1.Siku ya kwanza mizigo ya njiani aliyekodi gari alilipa yeye wale madalali wa mizigo njiani na pesa tulimlipa yeye.
Na kuna siku akalalamika kwamba angekuwa na tandam angepiga sana pesa.
Maana yake ni kuwa ile pesa ni yake.

2.Hii siku tulimlipa Tanboy japo mkodishaji alikuwa anahakikisha mizigo ikishushwa.

Sasa scenarios hizo 2 zikanichanganya.

Na ni gari za mama mmoja aliyekodi na mizigo yake ni midogo mno midogo mno kiasi kwamba gari linajazwa na mizigo ya njiani (kwa kuwa mie nimepanda mara nyingi gari yake huwa ananiambia mapema tu "jumanne nitakuwa na gari fuso hapo nitapita mapema sana mizigo yako niachie mdogo wangu nipate hela ya sabuni"

Siku moja nilikuwa na mzigo mkubwa mno lile gari nililijaza mie nduyo nikaona ujinga sasa kwa nini na mie nisijipange kimtaji na nikakodi gari.

Ngoja nijaribu kukuelezea model ya hii biashara ya Usafirishaji na Logistics kwa ujumla na faida zake zinapatikana vipi utaelewa hizo scenario zote ni KWELI ZINAWEZEKANA

nataka niandike kwa kirefu so ntakua naupdate

Hii biashara lazima ujue kwanza mtu anapokodisha gari lazima bei anayolipa ilipie gharama zoote za kwenda mzigo unakoenda, posho mafuta na kurudi gari ilipotoka hata ikiwa bodi bodi

Ila pia kuna njia nyingine inabid unamlegezea mteja kwa makubaliano maalum unaweza beba mzigo kwa mil 1.2 kwenda Dar ila unajua Dar kuna mizigo yako mingine ya laki 7 au 8 kurud nayo fasta( achana na ule ujinga wa kutega jangwani wiki mbili dalal analeta mizigo kidogo kidogo)

Sasa kama tajiri alishajua mahesabu hayo na kuona inamlipa mambo ya mizigo ya njiani hayamuhusu au anayapotezea inakua posho ya dereva

Na huwezi amini kuna safari unaweza ukalipwa vizur ya kwenda na kushusha na dereva akarud ana mil hata 2 yakwake tu ya vipeto vya kuunga unga

Sasa sijui hapo huyo mama na dereva walikua wanafanyaje biashara na tajir alikua anapataje chake
 
Kumiliki sania ni issue ndogo. Kazi ni kupata dereva mtulivu na anaeielewa gari. Pili ni nani na wapi pa kutengeneza gani lako na tatu unaifanyaje hiyo biashara. Ziko aina 4 za mfumo wa biashara ya malori hapa Tz.
1. Unaoperate kama kampuni, yaani unatafuta mzigo wewe, unantuma tu dereva na unampa mileji yake. Pesa zote unalipwa wewe tajiri.
2. Unasafirisha mizigo yako ya biashara zako. Hii ni kama una hardware etc.
3. Unakaa kushoto...unatembea na gari. Unapatana kila kitu wewe na kszi ya dereva ni kuendesha tu.
4. Hesabu. Unamkabidhi gari dereva, mnakubaliana route na unampa mtaji wa mafuta. Dereva anakuletea hesabu kwa mzunguko wa kwenda na kurudi. Wewe unabaki na matengenezo makubwa, service na tairi. Humlipi posho.

Kila moja ina faida na hadara zake.
Nimeifanya hiyo kwa miaka zaidi ya 30 sasa.

Ushauri.
Unapotaka kununua gari la biashara angalia bei za vipuri na upatikanaji wa mafundi wazuri eneo lako. Usikimbilie magari ya kisasa au ya nyuma sana au lenye milleage nyingi sana.
Scania ni chaguo zuri. Ushauri baki kwenye 124
 
No Dear, alisema alilinua kwa 15m i think kisha akalifufua hadi kufikia 83m, kwahio siku ile ndio ilikua trip yake ya kwanza tangu kulifufua na kwamba dereva alishalalamika kuwa kulikua na hitilafu..... sasa kufufua gari kwa mazingira ya kibongo bongo na huna ujuzi wa spare parts, utapewa spare yoyote ile. Ilitakiwa asiende umbali mrefu na ile gari at least ingepiga masafa ya Dar hata Chalinze ili kukagua uwezo wa kuhimili kashkash. Karibu Lunch
Kwani imezama ikiwa Tanga ?
 
Kwani hamna ndugu au watoto wa ndugu zako ambao wana uwezo wa kutembea na gari au kuendesha gari?

Maana ndugu anaweza kuwa na aibu kidogo na hata kama akiiba bas ataiba kidogo.

Ila jamaangu pia muwekee angalizo kuwa hakuna watu wabaya kama Ndugu usipokua makini. Kuna madereva wazur tunapata mtaani hatujuani na tumefanya nao kazi mpk wanazeeka wanajenga wanastaafu wananunua vyuma vyao na kuna madereva waluwalu sijapata kuona

Ila sijawahi kukutana na ndugu akafanya kazi kwangu akaondoka kwa uzuri. Wooote mishipa niliowah fanya nao kazi
 
Kumiliki sania ni issue ndogo. Kazi ni kupata dereva mtulivu na anaeielewa gari. Pili ni nani na wapi pa kutengeneza gani lako na tatu unaifanyaje hiyo biashara. Ziko aina 4 za mfumo wa biashara ya malori hapa Tz.
1. Unaoperate kama kampuni, yaani unatafuta mzigo wewe, unantuma tu dereva na unampa mileji yake. Pesa zote unalipwa wewe tajiri.
2. Unasafirisha mizigo yako ya biashara zako. Hii ni kama una hardware etc.
3. Unakaa kushoto...unatembea na gari. Unapatana kila kitu wewe na kszi ya dereva ni kuendesha tu.
4. Hesabu. Unamkabidhi gari dereva, mnakubaliana route na unampa mtaji wa mafuta. Dereva anakuletea hesabu kwa mzunguko wa kwenda na kurudi. Wewe unabaki na matengenezo makubwa, service na tairi. Humlipi posho.

Kila moja ina faida na hadara zake.
Nimeifanya hiyo kwa miaka zaidi ya 30 sasa.

Ushauri.
Unapotaka kununua gari la biashara angalia bei za vipuri na upatikanaji wa mafundi wazuri eneo lako. Usikimbilie magari ya kisasa au ya nyuma sana au lenye milleage nyingi sana.
Scania ni chaguo zuri. Ushauri baki kwenye 124

Karibu jamaa kwenye mjadala wewe kweli unaijua hii biz
 
Nimepata kama mil 100 baada ya kuvuna vanila huko Bukoba. Sasa nahitaji nijiingize kwenye biashara ya usafirishaji na wazo langu ni kununua scania kama kwenye picha.

Nimepanga kuanza na moja kutokana na kiasi nilicho nacho.

Naomba wenye uzoefu, kama biashara ikienda vizuri, kwa mwezi naweza ingiza kiasi gani?View attachment 1484199
Mkuu na kama unataka R tafuta R420 hizi spear zake ziko kila mahali lakini hizi R 450 sijui R 440 spear ya hizi zinakua mtihani ndio matoleo yameanza kuingia kwa sasa
 
Back
Top Bottom