Nataka kumuoa mdogo wa mke wangu, hii imekaaje kisheria?

Nataka kumuoa mdogo wa mke wangu, hii imekaaje kisheria?

Nondoh

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2016
Posts
298
Reaction score
478
Ndugu watanzania wenzangu hapa nilipo nipo kwenye mtihani mgumu sana wa kimaisha nashindwa nini cha kuamua, kiufupi nipo kwenye dilema.

Ki ufupi nimeishi na mke wangu karibu miaka 10 na tumebahatika kupata watoto 2. Kipindi chote cha mahusiano yetu tunaishi kwa furaha, amani na upendo.

Tatizo linalonikabili ni tabia ya kupenda kufanya mapenzi. Nimekuwa napenda sana kufanya mapenzi mara kwa mara kiasi kwamba nimekuwa kero mke wangu. Mimi hili silioni kama ni tatizo naona niko poa tu lakini yeye amekuwa akikwazika na kudai kuwa namchosha simuachi apumzike.

Kwa kipindi kirefu amekuwa na wasiwasi sana juu ya tabia yangu ya kupenda kumshughulikia mara kwa mara akihofu uwezekano wa kumsaliti ni mkubwa.

Tatizo hili nahisi amekwisha wasimulia ndugu zake na wao watakuwa wamelijadili kwa kina.

Mwaka jana Disemba tukiwa faragha alinihoji sana uwezekano wa mimi kumsaliti lakini nilimuhakikishia pamoja na uchu nilionao siwezi kumsaliti lakini bado hakuniamini. Katika mazungumzo yetu aliniomba kama nikishindwa kujizui bora nimuoe mdogo wake kuliko ikatokea nikaanza kutoka toka nje na kumletea magonjwa.

Ukweli wazo la kumuoa mdogo wake lilinistua na ilikuwa ngumu kumeza hivyo nilimkatalia katakata, lakini tangu kipindi hicho amekuwa akinisisitiza sana hadi namuonea huruma.

Kuanzia mwezi wa pili mwaka huu haupiti mwezi mdogo wake anakuja nyumbani atakaa siku mbili tatu au wiki anaondoka. Mara nyingi akija mdogo wake mimi nikiwepo dada mtu anajifanya yupo bize na vikazi na kutuacha peke yetu.

Ukweli kwa hali ilivyo uzalendo umenishinda, hata sijali jamii itasema nini mimi kuishi na ndugu wa damu sababu haya ni maisha yangu binafsi.

Kwa sasa nimekuwa najiuliza maswali mengi sana bila kupata jibu hasa suala la kisheria. Ninavyo jua mimi mtu kumuoa ndugu yake wa damu ni kosa kisheria lakini sijajua sheria inasemaje mtu kuoa ndugu au ndugu kuolewa na mtu mmoja.

Tukumbuke zamani baadhi ya makabila yalikuwa yanaruhusu mtu kuoa dada au mdogo mtu ikitokea mke kapatwa na matatizo ya kiafya eiza hawezi kuzaa au kutekeleza majukumu kama mke.

Nini maoni yenu, je kisheria imekaaje ndugu kuolea na mtu mmoja.

....................................................
K.n.y; mdau aliyeniomba ushauri
 
Kimila za kwetu huku ni ruksa mtu na ndugu yake kuolewa na mwanaume mmoja, Kuna shida ya nguvu za kike lakini mlete nimpe tiba ya kupandisha nyege ili usimuoe mdogo wake
 
Ngoja tusubiri majibu. mshana jr huyu mtu anabusara sana. Akikushauri unaweza zingatia.
Kaka uje utoe ushauri hapa 🙂
 
Hata kama umedhamiria kufanya hilo, nikushauri tu usifanye hivyo! Utaleta maafa ya zamani si ya sasa,mtunzie heshima mkeo na familia yake, onyesha ustaarabu wako Mbele ya jamii huwezi kusema hujali jamii wakati sisi sote tunaishi ndani yake! Kama uzalendo ukikushinda basi tafuta mke wa pili mbali na familia hiyo
 
kuna kitu unatafuta wewe, nguvu za kiume ni sawa na chupa ya wisk iliyoja. jinsi unavyoinywa ndiovyo inavyoisha. so kuwa makini sana na hiyo wisk yako iliyobaki mkeo wa pili akianza kutafuta kinywaji nje na nyumbani...uje hapa utuambie.

kila la kheri.
 
Back
Top Bottom