Nataka kununua Heavy Motor Bike aina ya Kawasaki ila ushauri ninaopata kwa walionizunguka ndio napata uoga

Nataka kununua Heavy Motor Bike aina ya Kawasaki ila ushauri ninaopata kwa walionizunguka ndio napata uoga

Kwa nchi zetu hizi watu wa ovyo. Vyombo vya moto ni hatari lakini pikipiki ni hatari zaidi unakua hatarini mara elfu zaidi.
Watu wetu wengi wawapo barabarani hawafuati sheria ikichangia na ujifunzaji uendeshaji vyombo kiholela basi ni hatari tupu.
Nilisababishiwa ajali na mbweha mmoja, toka hapo nikaachana na pikipiki, unakua makini weee ila inatokea mpuuzi anakusababishia ajali. Sitosahau.
 
Pascal Mayalla zungumza jambo hapa Mkuu.
Mkuu Mgibeon , asante kuni tag,
Habari zenu wadau....bila shaka ni wazima wa Afya.

Kuna jambo linanitatiza naombeni ushauri wenu. Nilipanga mwaka 2023 angalau ikifika tarehe 01 January niwe na kausafiri kangu (Gari) walau isiyozidi Mil 13.

Sasa kutokana na mambo kutokwenda sawa nimejikuta nina kama Mil 7 mkononi...sasa nikaona wazi wazo langu haliwezi kutoboa, hata nikataka kuchukua kagari mtaani katakuwa ka hovyo
emoji26.png


Wazo nikalihamishia kwenye bike off course napenda sana piki piki.

Kwa amount hiyo kwa yule mwanangu wa zanzibar sele mapikipiki napata kawasaki safi kabisa na chenchi kidogo inabaki
emoji16.png


Sasa nikasema niulize wadau wawili watatu wanipe maoni yao....kila ninaemshirikisha anasema bro naona umeyachoka maisha
emoji26.png
emoji24.png
huna muda tutakuzika achana na hayo mavitu....sasa naona ni bora nisingeulizwa nimeingiwa na hofu kubwa jambo ninaliuliza hata gari unaweza pasta ajali kikubwa ni umakini tu...

Sasa naombeni ushauri wenu nipo so confused
emoji53.png

View attachment 2450153

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
Mkuu Villky_J , mimi ni bike lover, kwanza anzia hapa Pascal Mayalla apata ajali..... kisho soma shukrani zangu Waraka wa Pascal Mayalla - Asanteni Sana!
Umezungumza vitu viwili tofauti
1. Unatafuta usafiri wa gari mzuri, bajeti yako ya 7.M haiwezi kukupatia gari nzuri ila itakupatia bike nzuri. Hivyo kwa wengi humu wanaokushauri ni usinunue bike kwa ajili ya usafiri as an alternative kwasababu huna pesa ya gari zuri, kwasababu hiyo hiyo 7M, unaagiza Passo, Vitz na IST na unalipia hadi uhuru!.
2. Kununua bike as means of transport of choice for the love of it. Huku ndiko mimi nilipo. Kama wewe ni bike lover, kiukweli bike ni very addictive!. Hiyo bike niliyopata nayo ajali ni big bike yangu ya 5!, nilianza na Honda VT 250, nikaja VFR 750, nikaja CBR 1,100, na kumalizia na Buel Fire Bolt 1,200 hii niliifuata mwenyewe US nadhani ndio Buell ya kwanza Tanzania na mpaka leo 15 years later sijawahi ona Buell nyingine yoyote kwenye street za Bongo!.

Ushauri wangu.
Kama shida yako ni usafiri, hiyo 7.M yako inakupatia gari zuri tuu.
Kama ni mpenzi wa bike, just do what you love!, usisikilize maneno ya watu!.

Nina rafiki zangu 2 walinishangaa kununua hiyo bike ya mwisho na pesa niliotumia, wao walinunua magari mazuri, tumeisha wazika kwa vifo vya ajali, magari wameyaacha!, mimi nipo nadunda, na nimepanga at 60, nastaafu rasmi na kuweka barabani Bongo Harley-Davidson CVO Tri Glide!

P
 
Hiyo ml saba unapata ractis safi kabisa ndugu ndugu hapa ninapotype mwili wote na mkono unauma vibaya mno,ni takribani wiki mbili tangu nipige mzinga mmoja matata sana wa piki piki nikaapa mimi na piki piki basi tena jichunguze tabia yako kwanza katika chombo kinahitaji uwe mwanaume na sio mvulana basi ni piki piki na kingine nilichogundua unawez kuwa makini sana lakini akatokea jamaa wa visendo na kiduku cha rasta akakusababishia ajali kwa ujinga wake ,nb kanunue gari
Balaa kama Ractis ndio hazinivutii kabisa nilikuwa nataka ka subaru impreza sasa ndio hvy mambo yamegoma

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom