Nataka kununua kiwanja, ila kwanini viwanja vya Chanika ni bei rahisi hivyo?

Toa namba
kibaha apo mwanzoni almaarufu mkoani kuna sehemu ina itwa mwanalugali mbele ya shule hiyo ya sekondari kuna mradi wa viwanja vilivyo pimwa na ni sehem ina weza kukufaa upo interested nikuunge na wahusika uka angalie hivo viwanja ukivutiwa uweze kufanya maamuzi?
 
Ni uelekeo wa geza maxmum kutoka ferr mpk kweny kiwanja main ni km 22-23 na eneo maarufu mwembe mdogo chuo cha afya cha kigamboni



kwa kifupi mwambie ni mbele ya nyumba za nssf za dege na karibu na avic town
 



namba za cm weka utafutwe
 
shukrani kwa maelezo mkuu
Kiwanja bado sijapata eneo nililoridhika nalo, wananipeleka porini wakati mimi nataka nijenge na kuhamia. Nimepandisha dau sasa hivi, milioni 20 kwa size ya 800 sqm ila isiwe porini



kigamboni mwongozo karibu na watumishi housing estate vipi? about 15km ferry ama 20km hv
 
Ukitaka kiwanja usiwe na haraka...nenda sehem unayotaka kiwanja, fika eneo hilo jichanganye piga story na wadau wa eneo hilo alafu pachika tu ka mada kuhusu viwanja...utaelekezwa kwa wanaouza bila udalali...
Jichanganye kwa mama ntilie, bodaboda, mafundi welding yaani kifupi kijiwe cha eneo hilo...usiende kishua sasa
 

Atakua anazungumzia mbondole uko uyu
 
Nmependa haya maelekezo

Hakika yatanisaidia namimi
 
Ile Chanika ni Manzese ya baadaye mkuu

Kule sio pa kununua kiwanja patakuja kuwa uswahilini hatari. Ujenzi holela kama ule kwenye ardhi iliyo tambarare mwisho wa siku mitaro ya maji machafu itazagaa kama Vingunguti.

Na ndio maana viwanja vina bei nafuu sana Chanika kwa sababu vinauzwa na waswahili.
 
Mwendo wa dakika 7 kutokea road gani, Bagamoyo road?

Anauzaje Bei ya kuanzia. Ukubwa wake?

Hivi ukitoka mapinga ndio unaingia kerege halafu Bagamoyo?
Umbali ni dakika 7 kutokea bagamoyo Road na barabara inafikika vizuri sana hata kwa gari

Ni sahihi ukitoka mapinga unaingia kerege

Anauza kuanzia 400sqmt na bei yake ni 6m yaan million sita za kitanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…