the numb 1
JF-Expert Member
- Dec 15, 2020
- 1,562
- 2,902
Mkuu hapo ni kigamboni au Mkuranga
Kigamboni mkuu karibia na chuo cha afya mwembe mdogo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu hapo ni kigamboni au Mkuranga
Nenda mikoani utapata kwa bei hiyoMi Nina milio1 napata wapi kiwanja
Wanasemaga ni kazi ya "JENGA UZA" kaka, Mfuko wa Cement unatoa tofali (biskuti) hata 60 kuendelea,aisee chanika na Chamazi kuna viwanja na nyumba za bei rahisi sana hadi kunanipa wasiwasi, yaani nyumba imekamilika kabisa inauzwa milioni 20, nataka kujua kwa nini ni bei rahisi kuliko kwingine kabla sijanunua
Akununue wewe uwe mke wakeNunua Simu tuu[emoji3][emoji3][emoji3]
Nyinyi wenye maisha magumu ndo mnanunuliwaAkununue wewe uwe mke wake
Goba kukiwa na kiwanja cha milioni 5 nistueNenda Goba, kuko poa, too modern!
Umeacha kudemka??Nyinyi wenye maisha magumu ndo mnanunuliwa
Mkuu huko bei ipojeeNna dalali ambae ndio alienitafutia Mimi kiwanja maeneo ya mapinga, ukiwa tayari ntakuunganisha nae kaka,,kule kuzuri ,upate tu mtu muhaminifu
kuanzia M.5 na kuendelea mkuu, na maeneo ya zinga piaMkuu huko bei ipojee
Hivi kuna wananchi walikimbilia hiyo fursa ya kununua viwanja Chato???Hivi wale walioenda kununua Viwanja Chato wana hali gani sasa hivi?
Mkuu huu ni uelekeo wa upande upi wa kibada au gezaulole na ni kilometa ngapi kutokea feri, ni karibia na eneo gani ambalo ni maarufu?Kigamboni mkuu karibia na chuo cha afya mwembe mdogo
mkuu hayo maeneo tokea miaka ya nyuma kuhitajika kwake hakukuwa kukubwa ukilinganisha na maeneo ya uelekeo wa barabara ya morogoro, bagamoyo maana tokea awali watu wengi walipenda kujenga uelekeo wa barabara ya morogoro na bagamoyo hivyo basi ni miaka tu hivi ya karibuni baada ya uhitaji wa ardhi kuwa mkubwa ndipo chanika ikaanza kuwa maarufu, kingine hakukuwa na lami kuelekea huko wakati uelekeo kwa mfano wa barabara ya morogoro lami ipo longtime kitambo. Kingine maji na umeme toka kitambo vipo along morogoro road na bagamoyo road wakati chanika ilikuwa ni visima tu. So hii ilipelekea watu wenye kipato kizuri kutochangamkia uelekeo wa chanika na hata mtu alikuwa akinunua kiwanja huko ilikuwa anaonekana mbona anajenga uelekeo ambao ni wa hali ya watu wa class fulani!!Wakuu nimejipanga na bajeti ya milioni 5 hadi 8 kwa ajili ya kununua kiwanja, maeneo ya DSM au Pwani kulingana na upatikanaji utakavyokuwa, bahati nzuri mimi nafanyia kazi nyumbani so hata eneo likiwa nje ya mji halitaniletea shida endapo litakuwa na intaneti
Baada ya kufanya uatafiti wangu nimeona maeno yenye viwanja vya angalau sqm 800 ni maeneo ya Kigamboni, ambapo unaweza kupata eneo la kujenga nyumba nzuri na uwanja ukbaki
Sasa kilichjonishangaza ni maeneo ya Chanika kuwa na viwanja na nyumba za bei chee sana tena maeneo yenye watu wengi tu, hi;li ni kwa nini?
Pia naomba kujua ni taratibu gani za kufuatwa ili kuepeukana na matapeli
Mkuu huu ni uelekeo wa upande upi wa kibada au gezaulole na ni kilometa ngapi kutokea feri, ni karibia na eneo gani ambalo ni maarufu?
shukrani kwa maelezo mkuumkuu hayo maeneo tokea miaka ya nyuma kuhitajika kwake hakukuwa kukubwa ukilinganisha na maeneo ya uelekeo wa barabara ya morogoro, bagamoyo maana tokea awali watu wengi walipenda kujenga uelekeo wa barabara ya morogoro na bagamoyo hivyo basi ni miaka tu hivi ya karibuni baada ya uhitaji wa ardhi kuwa mkubwa ndipo chanika ikaanza kuwa maarufu, kingine hakukuwa na lami kuelekea huko wakati uelekeo kwa mfano wa barabara ya morogoro lami ipo longtime kitambo. Kingine maji na umeme toka kitambo vipo along morogoro road na bagamoyo road wakati chanika ilikuwa ni visima tu. So hii ilipelekea watu wenye kipato kizuri kutochangamkia uelekeo wa chanika na hata mtu alikuwa akinunua kiwanja huko ilikuwa anaonekana mbona anajenga uelekeo ambao ni wa hali ya watu wa class fulani!!
Kingine ni ile kasumba ya wakazi kadhaa wa Dar wa kutoka bara kuwa anataka akae karibu na uelekeo wa njia ya kwenda kwao so watu wengi hawakuipenda chanika, kisarawe, na hata Pugu, lakini miaka ya hivi karibuni mentality hiyo imekufa kwa walio wengi maana machuma yamekaza.
Vilevile angalia umbali wa kutoka let say kimara na chanika kutokea city centre ingekuwa wewe miaka ya 80 au 90 unatafuta eneo ungetamani kuishi wapi? maana kwa mfano wakati kimara magari yalikuwepo mengi, chanika hayakuwa mengi sana na yalikuwa ni ya kusubiria yajae sasa we unataka kuwahi kazini!!!!
Hivyo basi marketi value ya chanika kuwa ndogo kwa kiasi fulani inachagizwa na historia yake kuwa tokea miaka hiyo value ya ardhi huko ni ndogo na inapanda taratibu. Angalia hata shule nzuri za private zipo uelekeo gani! angalia malls, au vijimalls vizuri vipo uelekeo gani, so hii imaana kuwa kuna watu wa class fulani hawakuwa wakiipenda chanika tokea awali. Angalia hata watu maarufu maarufu wangapi wanakaa Chanika!!
by the way kiwanja ulishapata au bado?