Mh! dunia ya Leo siyo ya kuamini mtu hivi hivi,chako kinakutoa uhai,miaka ya nyuma niliwahi kununua gunia za mpunga 500 nikaweka stoo za hawa watu wenye machine za kukoboa,chakushangaza muda uliposonga sana nikisubiri bei ipande, mwenye stoo akashikwa na tamaa za kutaka kuniua ili amiriki mpunga wangu ,nikiwa sijui hili wala lile,siku moja usiku saa sita nasikia watu wanagonga hodi kwangu nami bila kujua nikafungua mlango ,
Si kuamini macho yangu,nikapigwa chini ya ulinzi nakuambiwa tumetumwa tuje tukuue na bwana x, na ametupatia milioni moja,jamaa wakadai ili wasiniue niwape milioni moja na nusu wasiniue,nami bila hiyana ilibidi nifanye hivyo na baadae wakaniacha.
Ili kuamini ikiwa kweli wale watu walitumwa na jamaa au lah kesho yake kwenye muda wa saa nne jamaa mwenye stoo akiamini kuwa nimeshauawa nilienda mashineni na kukuta ameshaanza kukoboa mpunga wangu maana alikuwa na uhakika kuwa wameshanitoa uhai
Ogopa sana binadamu ,
Sent using
Jamii Forums mobile app