Nataka kuoa single mother wawatoto wawili, hata mimi nina watoto wawili pia

Nataka kuoa single mother wawatoto wawili, hata mimi nina watoto wawili pia

Benbulugu

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2016
Posts
852
Reaction score
1,236
Je,ni maswala gani ya msingi nihakikishe nayazingatia kabla ya kuingia kwenye ndoa ya namna hii,ndio kwanza tuna miezi mitatu ya mahusiano hatujafunga ndoa,mm nayy sotena miaka 32.sote wakristo.ushauri wenu unahitajika hapa.

Nimekua na mahusiano mengi ila najikuta kwahuyu dada kama niko SEHEMU salama hasa maswala ya heshima na utii aidha namaswala ya fedha pia,emekua mshauri mzuri hata katika maadili naona yuko vizuri.

Naona wanangu wakiwa na mamawakambo aliye mtiifu na mnyenyekevu.pamoja na changamoto zote na maoni kua tofauti tofauti ila bado najikuta kwahuyu single Maza au ndio kurogwa kwenyewe wakuu.
 
Sababu ya ninyi kuwa masingle parents ni ipi labda?
Kwa upande wangu wazazi wenzangu niliokutana nao hatukua tunaendana tabia,magomvi na mitazamo juu ya maisha haikua sawa ,isitoshe suala la utiifu na heshima halikuwepo, mwanamke wangu wa mwisho huyu hakua anafatisha maelekezo yangu,mm kama mmewe.kwa upande wake yy alitelekezwa na aliyekua baba watoto wake.
 
Je,ni maswala gani ya msingi nihakikishe nayazingatia kabla ya kuingia kwenye ndoa ya namna hii,ndio kwanza tuna miezi mitatu ya mahusiano hatujafunga ndoa,mm nayy sotena miaka 32...
Tuanzie hapo kwenye watoto wawili kila mmoja. Single mother na single father ni tofauti kidogo. Mwanaume ndie anabeba gharama za malezi ya watoto kwaiyo mwanamke akija kwako hata akikukuta tayari una watoto hataingia gharama za malezi lakini akija kwako na watoto wake maana yake wewe utaongezewa gharama za malezi ya watoto wake pia, upo tayari kulea hao watoto wote wanne bila kuwabagua mahitaji yao kuanzia shule, matibabu n.k?

Tuje kwenye muda wa mahusiano yenu, miezi mitatu ni michache sana kumfanyia surveillance mwanamke kwa lengo la kumuoa.

Kuna dhiaka ndogo ndogo za walimwengu na mateso ya kisaikolojia utayapata kuishi na mwanamke ambae anakuja kwenye mji wako na watoto wake, ndio maana hata wewe mwenyewe akili inasita ndio maana umekuja hapa kuandika uzi kujiridhisha, swali ni je utaweza kuishi na haya mateso ya kisaikolojia siku zote za ndoa yenu?

Uyo mwanamke yupo kwenye declining phase ya ubora wake, vigezo vya umri na usingle mother vinamuhukumu kwenye soko la mahusiano, karata pekee aliyobakiwa nayo ni kuwa wife material(hata kwa kuigiza). Huo mwenendo wake ambao so far umekuridhisha una uhakika ndio tabia zake au pretend tu? Katika hiki kipengere nakushauri ufatilie pia na past yake
 
Tuanzie hapo kwenye watoto wawili kila mmoja. Single mother na single father ni tofauti kidogo. Mwanaume ndie anabeba gharama za malezi ya watoto kwaiyo mwanamke...
Mleta mada, soma kwa makini sana huu ushauri kisha tafakari halafu chukua hatua,

Hapa tutakupa kila aina ya ushauri but at the end, the rest it's up to you.
 
Back
Top Bottom