Tuanzie hapo kwenye watoto wawili kila mmoja. Single mother na single father ni tofauti kidogo. Mwanaume ndie anabeba gharama za malezi ya watoto kwaiyo mwanamke akija kwako hata akikukuta tayari una watoto hataingia gharama za malezi lakini akija kwako na watoto wake maana yake wewe utaongezewa gharama za malezi ya watoto wake pia, upo tayari kulea hao watoto wote wanne bila kuwabagua mahitaji yao kuanzia shule, matibabu n.k?
Tuje kwenye muda wa mahusiano yenu, miezi mitatu ni michache sana kumfanyia surveillance mwanamke kwa lengo la kumuoa.
Kuna dhiaka ndogo ndogo za walimwengu na mateso ya kisaikolojia utayapata kuishi na mwanamke ambae anakuja kwenye mji wako na watoto wake, ndio maana hata wewe mwenyewe akili inasita ndio maana umekuja hapa kuandika uzi kujiridhisha, swali ni je utaweza kuishi na haya mateso ya kisaikolojia siku zote za ndoa yenu?
Uyo mwanamke yupo kwenye declining phase ya ubora wake, vigezo vya umri na usingle mother vinamuhukumu kwenye soko la mahusiano, karata pekee aliyobakiwa nayo ni kuwa wife material(hata kwa kuigiza). Huo mwenendo wake ambao so far umekuridhisha una uhakika ndio tabia zake au pretend tu? Katika hiki kipengere nakushauri ufatilie pia na past yake