Nataka kuolewa, ila nataka nieendelee na uhuru wangu

Waoaji tuko hapa town unaendaje huko? Piga chini, halafu tutayajenga niko hapa salasala , nitakupa uhuru wote
 
mtu mwenyewe ngumi mkononi hakuna Cha kutoa uhuru Wala nn
wee jiandae kufunguliwa kesi nachoomba isiwe tu ya mauaji😂
 
Usijali sio lazima ndoa tuta kupa mimba tu upate mtoto .uendelee na maisha yako sawa single mom
 
Ntaka niolewe lakini niendelee kuwa na uhuru wangu!

Nina mchumba wangu ambaye Mungu akipenda, mwezi huu mwishoni tunafunga ndoa. Hata hivyo, nimeshaanza kuogopa. Sio kwamba ananifanyia kitu kibaya au ni mtu mbaya, hapana, lakini kuna mambo yanatokea ambayo sijayapendi. Mchumba wangu ni daktari, anafanya kazi huko Shinyanga wilaya moja ya vijijini sana. Nilishafika huko, na kwa kweli ni sehemu ambayo siwezi kuishi kwa sababu nina maisha yangu Dar es Salaam, na marafiki zangu wengi wako huku.

Mimi ninafanya biashara, nina duka la vipodozi. Ingawa si kubwa sana, ndio linaanza, na ninaamini kuwa mbele ya safari litakuwa kubwa sana. Sasa juzi, wakati nikizungumza na mama yangu, aliniambia kwamba nikishaolewa nimwachie mdogo wangu hili duka, kwani siwezi kulisimamia nikiwa Shinyanga. Nikamuambai sshinyanga gani hiyo nani kakuambia anaenda kuishi huko aliniambia: "Unafikiri utaolewa ubaki Dar es Salaam?"

Nilimwambia mama kuwa nimeshaongea na mchumba wangu, na tumepanga nitabaki Dar, naye atahamishiwa huku. Mama alikaa kimya, na hicho kitu kilinikuna kidogo. Nikaamua kuongea na mchumba wangu na kumuuliza, "Je, unajua hatujaongea chochote kuhusu sehemu ya kuishi?" Alionekana kushangaa na kuniambia kwamba, "Si Tunakwenda Shinyanga."

Nilishtuka na kumwambia, "Mimi siwezi kuishi kijijini huko. Kwa nini usitafute uhamisho?" Akasema, "Uhamisho ni mgumu kupata, na isitoshe, sasa hivi mimi nakaimu Mganga Mkuu, nafanay mchongo ili niwe mkuu wa idara kamili. Nikihamia Dar, nitakuwa Mganga wa kawaida tu, na sipendi hilo."

Tuliendelea kugombana. Nilimwambia kuwa siwezi kuondoka mbali na Dar kwa sababu nina marafiki zangu, maisha yangu, na mipango yangu. Yeye akasema, "Siwezi kuoa mke ambaye anaishi mbali nami. Kama ni biashara, unaweza kuhamishia shinyanga."

Tumegombana, na kila mtu anaona upande wake ni sahihi. Mimi nahisi hii ndoa siwezi kuimudu. Kama mwanaume hajaniaoa tayari na anaanza kunipangia maisha, unafikiri itakuwaje nikishaolewa?

Mimi siwezi maisha ya kuendeshwa na mtu, natamani kuahirisha kila kitu kwa sababu siwezi kupangiwa maisha na mtu kisa ndoa. Naomba ushauri wako. Nikiwa hapa nyumbani hakuna anayenielewa, sasa sijui nifanye nini. Sina tena hamu ya ndoa!
kwa ushauri wangu vunja huo uchumba hiyo ndoa haitadumu
 
Ni pm nikueleze, mana mdogo wangu alipitia changamoto kama zako.
 
Bora mmegombana mapema kabla hamjafunga ndoa..

Kiufupi hapa hamna ndoa. Kila mmoja aendelee na mambo yake..
 
we jamaa si mwanaume?

juzi hapa si ulisema una mwanamke yupo mwanza?
Matraaakoo yake!!
 
Sema vizuri. Madanga yako ya dar utamwachia nani?
 
Dah maisha ya kijijini magumu nimewai shi na mume singida vj huko alikopangiwa kazi haloooo bado kidogo nikimbie ndoa,ila alhamdullilah kwa sasa tupo mjini dar.ndugu yangu usiende kijijini sijakushaur ata kidogo

we jamaa si mwanaume?

juzi hapa si ulisema una mwanamke yupo mwanza?
Labda anapiga miguu yote
 
Wewe kwa msimamo wako ndoa itakushinda, mwanaume akisimama sawasawa utaona anakutesa, matatizo yanaanzia kwa wazazi kwa kuwapa uhuru uliopitiliza, mwisho wa siku hata kuolewa mnaona ni jela. Kama baba angekunyoosha vizuri toka utotoni, shinyanga ungeenda na huyu mwanaume usingeona ni tatizo.
 
Yaani mwanaume ndio akufuate wewe
Akusikilize wewe
 
Back
Top Bottom