MKuu pikipiki yako inafika ila shida haina vifaa vinavyoisaport kufika,
Mfano unaweza kupasua tairi kama mara mbili hadi ufike, kwa tairi hizo kwa umbali wa km 300-400 kwenye lami tairi haitakuwa yenyewe,
Pia Mnyororo utazingua sana means unaweza katika hata mara tatu kama utakuwa unaunga huohuo
Pia Hiyo pikipiki ina vibration kubwa ambazo zinazidi uwezo wa spring sio nzuri kwa masafa marefu
Pia injini yake inachemka sana mkuu unaweza jikuta ikabust hata ukiwa na mapumziko must upumzishe chombo kwa takribani saa moja na nusu kabla ya safari kuanza tena
Pia sina uhakika mavazi utakayotumia kama yako sahihi sio mambo ya kukariri kuvaa sijui majaketi mazito sijui nini noo
Kuna helment nzuri sana zinazotumika kwa masafa marefu na hazitoki na hiyo pikipiki yako unanunua tu pembeni uziri wa hii helment nikwamba ni imara sana pia inakuwekea mfumo mzuri wa kupumua haikutengenezei joto kama zilizyo zingine
la hatari sina uhakika na uzoefu wa safari ndefu kwa pikpik unahitaji uzoefu kwa usalama wako
bila kupepesa macho unaweza kujikuta unalala hapo hapo juu ya chombo na bado kinatembea na ukija kuamka unajikuta upo ahera
Ushauri DONT TRY THIS MKUU
Unafamilia na Ndugu wanakutegemea na Bado Wanakuhitaji Sana
Pia Sisis Wana JF bado tunakupenda Mno