Nataka kusafiri kutoka Mwanza kwenda Morogoro kwa pikipiki sanlg 125, naomba ushauri kitaalam

Nataka kusafiri kutoka Mwanza kwenda Morogoro kwa pikipiki sanlg 125, naomba ushauri kitaalam

Ushaur wangu beba oil lita 2 kwenye beg;chukua kidumu cha lita 1 kwa ajili ya emergence,usisahau kuvaa makoti makubwa ya kuzuia upepo pamoja na buti,chukua mwamvuli njian hakutabiriki last hakikisha unapumzisha pikipiki atleast kwa kila km 300 pamoja na kuzingatia sheria za barabaran hususani site mirror
Sasa huo mwamvuli atajifunikaje
 
Nakushauri pakia hio bodaboda kwenye roli utajiletea majanga tu manake issue sio kufika issue ni uzoefu wa kuendesha mda mrefu tena highway kumbuka una pishana na heavy trucks barabarani pia uchovu utakupa tabu sana, nisha wahi endesha gari toka Arusha to Mwanza nikatubu njiani najiuliza kwa boda boda itakuaje ? Japo inawezekana lkn ujiandae kwa lolote
Nyie wanawake hamuwezi kuendesha pikipiki
 
Tembea kaka hiyo mbona haina taabu. Si sanlg tena ikiwa nyekundu ndio mwake
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Write your reply...Hivi vitu vinahitaji uzoefu wa kuendesha safari ndefu mimi nilijaribu kutoka na BAJA Dar~Tbr njiani ni very risk nashukuru mungu nilifika salama na nilirudi salama hiyo ilikuwa 2004 na sitaki tena kuendesha pkpk kindezi ndezi kama hivyo
 
Kusafiri na pikipiki ni jambo la kawaida sana na watu wanasafiri nazo kila siku bila shida yoyote, ila watu wasio na experience wanakatisha wenzao tamaa tu.
 
Ushauri wangu wakati unaanza safari waambie kule unakoenda waanze kuchonga jeneza

Halafu hao wachonga jeneza, inabidi nao waanze safari ya kulisafirisha kuelekea kule anakotokea marehemu mtarajiwa, kwa sababu wasipofanya hivyo, jeneza hilo itabidi walihifadhi kwa ajili ya mtu mwingine, mhusika hataweza tena kulitumia. Kumsubiri haiwezekani kwa sababu tayari inajulikana wazi kuwa hataweza kufika huko waliko wenye jeneza
 
ingekuwa pikpik ya timing chain kama boxer TVS hlx au SINORAY ungefika mapema kuliko bus...kuna jamaa yangu katoka dar juzi saa mbili asubuhi kumekucha na SINORAY ya timing chain kafika NJOMBE saa tisa alasiri umba ni km 700 alitumia takriban masaa 7...timing chain haitetemeshi wala hauchoki unakuwa na mwendo wako wastani kama 100kph unafika mapema kabisa
...ila hiyo sun lg utajuta utaomba kupakia njiani kwenye maroli maana full vibration hata manyoni hufiki utakuwa ushapigwa ganzi
ushauri mzuri sana wa kitaakam japo hapo mwisho umenivunja mbavu[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Watu washamba utawajua.yeye anaulizia habari za pikipiki mwingine utakuta anakuja kuleta mifano ya gari. Jamiiforums ina watu wa ajabu ajabu siku hizi. We mdada umeshindwa kumwelewa mleta hoja kabisa.

Nakushauri pakia hio bodaboda kwenye roli utajiletea majanga tu manake issue sio kufika issue ni uzoefu wa kuendesha mda mrefu tena highway kumbuka una pishana na heavy trucks barabarani pia uchovu utakupa tabu sana, nisha wahi endesha gari toka Arusha to Mwanza nikatubu njiani najiuliza kwa boda boda itakuaje ? Japo inawezekana lkn ujiandae kwa lolote
 
Kwani jamaa humu JF huwa anaanzisha nyuzi kali kali?

MKuu pikipiki yako inafika ila shida haina vifaa vinavyoisaport kufika,
Mfano unaweza kupasua tairi kama mara mbili hadi ufike, kwa tairi hizo kwa umbali wa km 300-400 kwenye lami tairi haitakuwa yenyewe,
Pia Mnyororo utazingua sana means unaweza katika hata mara tatu kama utakuwa unaunga huohuo

Pia Hiyo pikipiki ina vibration kubwa ambazo zinazidi uwezo wa spring sio nzuri kwa masafa marefu

Pia injini yake inachemka sana mkuu unaweza jikuta ikabust hata ukiwa na mapumziko must upumzishe chombo kwa takribani saa moja na nusu kabla ya safari kuanza tena

Pia sina uhakika mavazi utakayotumia kama yako sahihi sio mambo ya kukariri kuvaa sijui majaketi mazito sijui nini noo
Kuna helment nzuri sana zinazotumika kwa masafa marefu na hazitoki na hiyo pikipiki yako unanunua tu pembeni uziri wa hii helment nikwamba ni imara sana pia inakuwekea mfumo mzuri wa kupumua haikutengenezei joto kama zilizyo zingine

la hatari sina uhakika na uzoefu wa safari ndefu kwa pikpik unahitaji uzoefu kwa usalama wako
bila kupepesa macho unaweza kujikuta unalala hapo hapo juu ya chombo na bado kinatembea na ukija kuamka unajikuta upo ahera

Ushauri DONT TRY THIS MKUU
Unafamilia na Ndugu wanakutegemea na Bado Wanakuhitaji Sana
Pia Sisis Wana JF bado tunakupenda Mno
 
Hako kapikipiki hafiki nako mbali kanachemka hasa awe na pesa za kutosha kula njiani mbio asizidi kilomita 50 kwa saa .Mnyororo atembee nao mwingine mpya .Kila akienda kilomita 80 Akapumzishe walau masaa mawili akifika kilomita 160 alale aamuke nako kesho katulie kapigwe upepo na serivice
Mwanza-Moro siku 4!
 
niliwahi toka na TVs ngara mwanza 2012 km kama 490 nilifika siku hiyo hiyo lkn sitarudia tena akyanani maana ilifika sehemu nikatamani maroli yanipe tafu mabega na mgongo na kiuno viliuma siku tatu
 
Kwani ukipakia kwenye semi kuna tatizo gani?au kuna kitu unataka kugundua bro?
 
ingekuwa pikpik ya timing chain kama boxer TVS hlx au SINORAY ungefika mapema kuliko bus...kuna jamaa yangu katoka dar juzi saa mbili asubuhi kumekucha na SINORAY ya timing chain kafika NJOMBE saa tisa alasiri umba ni km 700 alitumia takriban masaa 7...timing chain haitetemeshi wala hauchoki unakuwa na mwendo wako wastani kama 100kph unafika mapema kabisa
...ila hiyo sun lg utajuta utaomba kupakia njiani kwenye maroli maana full vibration hata manyoni hufiki utakuwa ushapigwa ganzi
Mnapoandika ushuhuda wenu,punguzeni chumvi.
(Kauli taarifa)
 
Mnapoandika ushuhuda wenu,punguzeni chumvi.
(Kauli taarifa)
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji848][emoji848][emoji848]kweli mzee haumini nini hapo juu
 
Back
Top Bottom