Acha kukata tamaa, shida sisi vijana tunakata tamaa. Tafuta riziki ya halali.
Shida vijana tupata fedha tunaenda kuhonga Malaya, Kunywa pombe, kuvuta bagi na sigara unadhani ukifanya hivyo utafanikiwa ?? Jibu ni hapana huwezi kufanikiwa.
Vijana wana degree hawawezi kufanya kazi za aibu eti kisa wanaona aibu watachekwa huo ni ushamba.
Ngoja nikupe Stori yangu Fupi ambayo itakupa Fundisho.
Mimi ni Kijana wa Makao, nimezaliwa mwanzoni mwa mwaka 1997, katika kukua kwangu nimepitia changamoto nyingi sana.
Nimezaliwa Kahama Vijijin - Shinyanga, nimehitimu katika shule bora kabisa kahama enzi hizo shule hiyo ilikuwa inakimbiza sana, inaitwa MHONGOLO PROGRESSIVE SEC. SHOOL 2011 - 2014.
Mwaka 2015 nilienda Advance mkoani Kagera katika combination ya PCB, mwaka 2016 nikavunjika mkono wa upande wa kulia ambao do mkono natumia kuandika. Nilihagaika sana na mkono wangu huu takribani miezi 4.
Mwaka 2017 May nikafanya mtihani wa ACSE matokeo yakatoka nikawa na ufaulu wa Division 1 ya point 9.
Mwaka 2017 Sept. Nilihitimu mafunzo yangu ya JKT katika kambi mama hapa Tanzania (821 BULOMBORA JKT)
Mwaka 2017 Nov. Nikajiunga na chuo kikuu katika course of Bachelor in Computer Science, daah kiukweli Fani hii sikuipenda hata kidogo sababu ndoto zangu zilikuwa siku moja niwe Daktari niwahudumie na kuwatibu watanzania wenzangu, hivyo basi nilisoma ilimradi tu na wakati huo nilikuwa na mkono wangu mbovu ulikuwa unanisumbua sana.
Kipindi niko chuo nilipata BUMU tu, ila ADA nilikuwa nalipiwa na mzee, nashukuru mzee wetu ametusomesha watoto wake wote Mungu amubarikiiii sana, alijinyima sana na akauza ng'ombe wake sisi tukaenda shule.
Mwaka 2019 Nilipitia changamoto kubwa sana sitoisahau maishani mwangu, Nilitapeliwa hela na MKINGA Mmoja wa Makete Kama ml 4 ivi (hela ya bumu ya mwaka wa kwanza na wapili + ada), kidogo ni disco chuo, Mungu tu do alinipambania nikaendelea na chuo tena.
Mwaka 2020 nikamaliza chuo kikuu, huo huo mwaka nikasema sirudi nyumbani, nyumbani kuna kila kitu kuna mashamba ya maelfu ya mahekali na mifugo wa mamia na mamia, ila nilisema na nilikuwa nimejiwekea malengo yangu natafta mali yangu mwenyewe hata kama ni kidogo na sikurudi nyumbani sababu nilimkosea baba yangu, kosa lenyewe ni kutapeliwa hela ya ADA.
Mwaka 2020 Oct kipindi cha uchanguzi wa Magufuli nilipata Kibarua cha Kusoma Mita za Maji katika Mamlaka ya Majasafi na usafi wa Mazingira Mkoa X ni mamlaka kubwa sana Nchini.
Katika kibarua changu cha kusoma mita nikiwa napita mtaani daaah nilikuwa nadharauliwa kinoma, watu waliokuwa wananidharau asilimia kubwa ni wanachuo, na vijana wa mtaani, hawakujua mimi kila mwezi nilikuwa napata Milioni 1 (1,000,000) na hawakujua mimi nina elimu kubwa na nzuri, na pia hawakujua nimetoka Familia inayojiweza na kubwa tu.
Mimi katika maisha yangu huwa najifanya masikini au kujifanya mtu wa level ya chini kupitia kufanya hivo huwa naona kila aina ya tabia za watu.
Nimefanya kazi ya usomaji wa mita miaka 3, toka mwaka 2020 hadi 2023 na nilifanikisha ku save zaidi ya Milioni 15.
Mwaka 2022 July nikaoa Mke wangu wa Kibena kutoka Kidengyembe Mkoani Njombe, namshukuru Mungu na kwa rehema na baraka zake saizi nina katoto kamoja.
Mwaka 2023 August nikapata Ajira serikalini katika idara ya Tehama & Takwimu tena bonge la Taasisi kwa mshahara mkubwa namshukuru Mungu nina maisha yangu, ninakula ninachotaka.
Watu walionidharau leo hii wakiniona daah huwa nawaacha midomo wazi kwa kweli. Yule ambaye nilikuwa msomaji wa Mita za Maji leo hii nahudhuria vikao vya Wizarani.
Nimejifunza mambo Mengi sana katika maisha.
1. Maishani lanzima tuwe na subira
2. Maishani usimdharau mtu
3. Maishani lanzima uwe mwaminifu haswa makazini huko.
4. Mungu yupo na ukimuomba hutoa
Pia nimejifunza kwenye maisha haya baraka zinapitia kwa watu, Mungu alichokubariki jitaidi sana Kutoa SADAKA, siyo sadaka ya kanisani, Jitaidi sana kusaidia watu ambao hawajiwezi, saidia wazee, saidia yatima.
Narudi kwako mtoa maaada, usiende kwa waganga ili upate mali ya Haraka utakufa siku ambazo sio zako, utaishi maisha ya ajabu na yashida sanaa.
Fanyakazi ukiwa na tumaini kwamba ipo siku moja utafanikiwa tuu, kudharauliwa maisha haikupunguzii kitu.
Fanyakazi kwa Malengo, usiige watu, upe moyo wako ahadi kuwa ipo siku moja utafanikiwa.
Pambana pambana, kama umeona maisha hayaendi, gubali kurudi kijijini, nakupa baadhi ya Maeneo ambayo ukitoa aibu unafanikiwa.
Nenda:
Kahama, Mafinga, Katoro, Tunduma, Makambako, Pawaga, Ilula, Songea, Katavi.
Acha kabisa kukataa tamaa.
Usiogope kudharauliwa.
Maisha ni kutafta na sio kutaftana.
Epuka sana makundi, wanawake, pombe, sigara, bagi n.k
Kesho yako ni bora endelea kupambana.