Nataka kwenda Dubai au China kununua simu nipeni maelekezo mliowahi kwenda


Mkuu kuna swali kuhusu TRA hapo kama ungekuwa unafahamu taratibu zao na kulijibu basi hakika comment yako ingetosheleza na uzi tungeufunga
 
Mkuu hizo RMB sawa na dollar au sawa Tsh kiasi gani.
Mkuu pia hapo umesema wachina huwa hawaamini mpaka uwe wakudumu other wise unaweza ukanunua 50 return 30 kivip
Naje kwa standard nzuri ya smartphone bei hasa ikoje ya kununua kwa pesa ya kibongo au dollar ngap?
Pia faida zikoje kwa kila smartphones ukija kuuza huku bongo hizo smart kwamfano iphone,samsung
 
inatosha kabisa na kubaki
 
Tatizo kubwa bado ni TRA pale Airport maana usije leta simu ikafika hapo bei ikawa sawa na hapa Tz
 
kuna watu unaweza kuchanga nao na mkaagiza mzigo kwa bei ndgo zaidi huku ukipata mzigo mkubwa kuliko kutumia gharama kubwa kwa ajili ya ndege,malazi,chakula na kadhalika nitafte nikuunganishe 0753041742
 

mkuu rate huwa ina vary ndo mana sikutaka kuandika pesa in TSH.nimeangala sasa hivi XE convertinaonyesha ni 1RMB=325 TSH.Mara nyingi huwa inacheza kati ya hapo hadi 340 hivi.So kupata Tsh ni unazidisha hizo RMB kwa 325 (kwa sasa hivi)
kuhusu bei na inafatana na simu model gani unataka na gb ngapi,hizo ndo factor zinazo amua bei.simu zinalipa kwa ninavoona,ila pia ita depend kwako "kulipa" ni kuanzia shilini ngapi😃
 
Mkuu kuna swali kuhusu TRA hapo kama ungekuwa unafahamu taratibu zao na kulijibu basi hakika comment yako ingetosheleza na uzi tungeufunga
mkuu swala la kodi airport ni unamalizana na jamaa kibingwa.Ama unanunua mikoba ya wadada kama hata 20 hivi,utaweka simu ndani,ukifika TRA utalipia tu mikoba (itakuwa cheap).Ukilipia hawatapitisha mizigo yako kwenye scanner,so simu zitakuwa zimepita bila kulipia.Otherwise ni uwatumie jamaa wanao tuma mizigo toka huku China.Bei zao huwa ni 10$ kwa simu moja.
hope nimekusaidia kiasi
 
kuna watu unaweza kuchanga nao na mkaagiza mzigo kwa bei ndgo zaidi huku ukipata mzigo mkubwa kuliko kutumia gharama kubwa kwa ajili ya ndege,malazi,chakula na kadhalika nitafte nikuunganishe 0753041742
Tanguliza Kichwaa hapa usipigwe
 
Kama ndo unaanza biashara kuwa makini sana na maamuzi ya mwanzo maana ukikosea step pesa yote itazama. Nakupa tu ushauri hiyo 20m igawanye nusu.

Tafuta taarifa sahihi na maagent waaminifu hasa China ili uagize mzigo wa 10m.

Kuna watu wengi sana huagiza mizigo na kufika salama bila tabu kabisa.

Utaona kama kuna mafanikio kifaida katika huu mzigo then nenda mwenyewe, maana hapa utakuwa na detail za kuanzia seller range ya bei n.k na utakuwa na confidence ya kutokupoteza mtaji wako.
 
Hili wazo zuri sana na ni mbinu nzuri.
Ukiingia kichwa kichwa umeliwa na mwisho wa siku unaletwa uzi wa majuto hapa.
Kwenye biashara ukiwa na papara kupigwa ni rahisi sana.
 
Ukiwa mwoga hufanikiwi. Bora uende ukachague wewe.
Ukiletewa anayekuletea anaweza kukuzima rmb 10 hadi 100 kwa simu
 

Hapo umemaliza mkuu, barikiwa
 

Weww jamaa utafika mbali sana kwa biashara zako.unajua kutia moyo watu na inaoneka huna vinasaba vya wivu kabisa.mafanikio utayakimbia mwenyewe
 
Bos sihitaji kulala kwamtu nahitaji kufahamu badhi yagharama kama nilivyoeleza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…