Nataka kwenda Dubai au China kununua simu nipeni maelekezo mliowahi kwenda

Nataka kwenda Dubai au China kununua simu nipeni maelekezo mliowahi kwenda

20m ndo uende Dubai au china?
au unataka kwenda kutembea?
simu aina gani? kama unanua smart phone za laki mbili 20 unanunua simu ngapi?
una duka atayari au ununue ndo uanze tembeza?

Binafsi naona tafuta biashara ingine hapa ya uhakika mtaji hata 15m

5m nenda Dubai katembee ujionee na ujifunze
15 M hata Kkoo kwa wauzaji wa jumla unaweza pata faida
Sasa akienda k/koo kwa wauza ana 15m na anapata faida kwa nini asiende Duabi aate faida zaidi....Ushauru wako unakinzana wenyewe kwa wenyewe
 
Kwanza hongera sana...

Ushauri wangu kwako ni kwamba ungepata agents au wakala mwamimifu wa huko dubai au china akununulie mzigo atume au kama unaweza kuagiza mtandaoni mfano alibaba wanauza simu za jumla kwa bei nzuri mnoo ila unapaswa kuwa makini


NB;mitandaoni napo si salama wahitaji umakini ukiagiza kwa mtandao maana utapeli wizi na vitu feki ni vingi

Pia maagents nao sio waaminifu mimi sifaham hili ila nilimuona faiza aly kule insta akitumia watu mizigo yao kutoka huko china
Its best aende mwenyewe huko apate exposure
 
Watanzania wengi ni watu wawivu mno

1. Nauli kwenda na kurudi: USD 1,200

2. Chakula kwa siku: USD 22

3. Hotel Single Room: USD 50

4. Nauli ya mizunguko town: USD 49
(Taxi+Metro+Daladala)

5. Mzigo wako unaotaka kununua: (Na
hii tukupe jibu?): Minimum USD3,500
Una maanisha unaweza kwenda na kurudi china na mzigo kwa 5,000,000 [emoji853][emoji853][emoji853][emoji853]
Hapo tra inaweza kuwa hadi 8000000 huyo wa 20m aende tuuu
 
Yani kuna watu mnazingua mno kama hamna majibu tulieni wenye exposure na hiyo kitu watoe ufafanuzi kwani lazima ku"comment"

N:B imenipasa nitoe comment yangu hapa kusisitiza tuu maana majibu nimeona watu wa wawili tuu ndo wamejaribu kujibu kama mtoa mada alivyotaka.
 
Wanatakiwa watu kama wewe kuinuana na kutiana moyo
Usikatishwe tamaa na ndugu zako hapo juu.hiyo 20mil ni pesa ndefu. Wengi wao wanakupigia masimu ya 200k ambayo Kwa ujumla soko lake wewe mwenyewe unalijua, Kwa hicho kiwango ni wastan wa USD 8600. Hata ukisema utenge pesa ya mzigo Tu USD 4500 itatosha kabisa kununua mzigo. Ukisema uchukue headphone, chaja, ni zile accessories nyingine Kwa usd 1000 Tu mzigo utaukimbia mwenyewe.
 
Nimeamini JF watu hawapendi mafanikio ya wengine, in short ni upuuzi umejaa tu, mleta uzi alikuwa anahitaji mambo yafuatayo kwa uchache,
1. Nauli TZ China Tz
2. Hotel, usafiri, chakula akiwa China per day
3. Wastani wa bei za simu janja kwa kilo na gharama za wapagazi
4. Gharama ya kusafirisha mzigo China Tz
5. TRA haki bin haki hali ikoje, wacha short cut
6. Wastani wa mauzo, bei elekezi hapa Bongo
7. Ushuru na kodi yeyote wakati wa mauzo, na Neosho,
8. Mkokotoo wa mtaji wake wa 20m

Sasa majitu humu hamnazo kazi ubishi tu na comment za kipuuzipuuzi tu kukatishana tamaa mara njoo pm nyambaf

Pangu Pakavu
 
Nauza simu na accessories
Dubai kwenda kurud dollar 600 with Flydubai, dola 100 malazi getto kwangu. Andaa dola Mia nyengine ya Usafiri na kula.
Huku utawaka kwa Mguu. Upo na zaid pm me.
Unatka Mzigo NIAGIZE unataka kuja kuona jangwa linalovutia Karibu.[emoji120][emoji120]
IMG-20190820-WA0013.jpeg
 
Dubai kwenda kurud dollar 600 with Flydubai, dola 100 malazi getto kwangu. Andaa dola Mia nyengine ya Usafiri na kula.
Huku utawaka kwa Mguu. Upo na zaid pm me.
Unatka Mzigo NIAGIZE unataka kuja kuona jangwa linalovutia Karibu.[emoji120][emoji120]View attachment 1208136
Mkuu kwani akienda kulala hotelini itamgharimu dola ngapi kulala usiku mmoja?
 
Kuna uzi huku umeelezea kila kitu kuhusu kwenda China,mtaji,faida na changamoto zake,vitu gani vya kununua na wakati gani vinakua rahisi huku China kuleta Tanzania. tuombe mods wauunganishe huku
Embu copy link yake iweke hapa tuuzamie huo uzi
 
Back
Top Bottom