Nataka kwenda kuoa Zanzibar

Nataka kwenda kuoa Zanzibar

Zenji unaongea na wazee na wakubwa wa binti fasta mambo yanakuwa tayari.
 
Ingia kwenye Uislam. Jifunze nanuwe unasali sala 5 kwa siku kwa kuanzia. Nenda Zanzibar, India msikiti wowote ulio karibu na wewe, ongea na Imam.

It's as simple as that.

Ma shaa Allah, mama Samia ana mvuto.
Asante sana
 
Kwanza wale wanajua kupika vi -bites tu kama vile vibibi, sambusa, kachori, tambi, chapati na vyakufanana na hivyo.

Lakini Eti vyakula kama vya bara hivi rasmi kama vile ugali nyama, wali maharagwe n.k hawajuagi nikwambie [emoji108][emoji108]

Yaani uwe umezoea na kukulia kula vya kule vinginevyo utachokaje?!
 
Usicheze
Kama ilivyo kigezo cha kuajiriwa SMZ ni lazma uwe ni mzanzibar bc na kwa wazaz ni hivyo hivo ili uwo bint yao lazma uwe mzanzibar inagawa sio wote ile weng mno wako na mtazamo uwo ata uwe tajir kias gani hawakupiiii mtoto wao abadan.
na hela mkuu.

Nothing can take the place of money in the area where money works better
 
Habari zenu wana jamvi.

Nisiwachose sana.

Ni hivi, sauti yangu ya ndani inanishuhudia nioe mwanamke wa kizanzibari..

Kuhusu dini Mimi ni Mkristo mwenye vinasaba vya uislamu. Nipo tayari kusilimu wakati wowote ule. Kwanza I am not even a church going person.

Ukristo wangu ni ukristo wenye matege.

How? Sisi ukoo wetu wote ni waislamu. Babu yangu kizaa baba alibadili dini na kuwa mkristo wakati ana muoa bibi kizaa baba. Bibi kizaa baba kwao walikuwa wakristu. Babu yangu alikutana nae alipoenda kutafuta maisha kwenye mkoa ambao una wakristu wengi (nyumbani kwao bibi)

Hata hivyo babu yangu alikuwaga ni wale wakristu wenye kuvaa kanzu na kibaragashia. Still bado alikuwa n.a. " aura" (haiba) ya kiislamu.

Vivyo hivyo kwa Marehemu baba yangu mzazi.

Ndugu zetu karibu wote ni waislamu. Hata kwenye tumbo letu baadhi ya ndugu zangu walipewa majina ya ki islamu walipo zaliwa (sababu?) Baba alikuwa anawapa majina ya babu zake na baba zake wakubwa. Mfano kaka yangu ninae mfuata anaitwa Mohamed ingawa mkatoliki..mtaani kwetu anaitwaga Mohamed Mkristo or simply Mudi Mkristo.

Pamoja na yote Mimi mwenyewe binafsi nimekuwa exposed n.a. uislamu tangu nikiwa mdogo. Mifano nilikuwa naenda madarasa nikiwa mtoto kwa ajili ya kampani ya ndugu zangu upande wa baba (watoto wa baba wakubwa wadogo na mashangazi)

Kwetu sisi si waenda kanisani kihivyo (church goers)

Miaka ya 2000 mwanzoni tulipangishaga mashahidi wa yehova. Kuna siku walikuja na wazungu kumuhubiri baba..alicho waambia ni " nyinyi jeshi la Yehova (aliwaita Jeshi la Yehova) mnataka kusema mnaijua Biblia kuliko Mimi mkatoliki (kiukweli ni kwamba kama ilivyo kwa wakatoliki wengi duniani baba angu hakuwa anaijua biblia kihivyo). Akaendelea kuliko kujiunga na kanisa lenu si bora nirudi kwenye dini yangu ya ukoo (uislamu)

kauli hii ya baba ilipanda kitu kikubwa sana ndani ya nafsi yangu kuhusu uislamu.

Katikati ya miaka ya 2000 dada angu aliolewa na muislamu akabadili dini.

So kwangu Mimi kurejea kwenye uislamu wala hata sio tatizo.

Now kuhusu mwanamke wa kizanzibari.

Kwa muda mrefu sana nimekuwa nilipendezwa kuwa na mke wa.kizanzibari.

Nataka kwenda Zanzibar kwa ajili ya kutafuta mwanamke wa kuoa.

sifa

1. Awe mzanzibari.
2. Umri miaka.16 hadi 23 (asiwe na mtoto) Mimi umri wangu ni miaka 38.
3. Elimu darasa la saba na kuendelea (Mimi elimu yangu ni chuo kikuu nimejiajiri naishi Dar)
4. Awe mcha Mungu.
5. Akiwa mwembamba mrefu nitafurahi zaidi.

Mbinu nitakayo itumia kumpata.

Nataka kwenda Zanzibar then niende msikitini niongee na mzee au wazee niwajulishe adhma yangu.

Je, kwa mbinu hii nitafanikiwa? Wazoefu nipeni mwongozo.

Naweza kwenda hata Pemba.
Bosi wangu naona unazunguka saana lakini nikupe hints tu kuhusu wazanzibari, Mimi mwenyewe ni mzanzibari na naishi huku, naeafahamu wazanzibari in and out, kuhusu kuoa mwanamke wa kizanzibari muislamu wakati wewe sio muislamu hiyo ni ngumu Sana, ninachokushsuri kwanza kabla hujaja huku badili hiyo dini yako kwanza uwe muislamu, halafu uusome uislamu uujue, baada ya hapo Anza kutafuta mke umpendae taratibu, kwa sababu kama vigezo vyako vitakuwa vikubwa kumpata umtakae basi ujue kwenda kuposa mtoto wa kizanzibari utafuatiliwa sana life yako na historia yako na ukoo wako, kiufupi ujipange usiourupuke, na ukifanya hivyo utapata mke ambae hutojutia na utafurahia ndoa yako.
 
Bosi wangu naona unazunguka saana lakini nikupe hints tu kuhusu wazanzibari, Mimi mwenyewe ni mzanzibari na naishi huku, naeafahamu wazanzibari in and out, kuhusu kuoa mwanamke wa kizanzibari muislamu wakati wewe sio muislamu hiyo ni ngumu Sana, ninachokushsuri kwanza kabla hujaja huku badili hiyo dini yako kwanza uwe muislamu, halafu uusome uislamu uujue, baada ya hapo Anza kutafuta mke umpendae taratibu, kwa sababu kama vigezo vyako vitakuwa vikubwa kumpata umtakae basi ujue kwenda kuposa mtoto wa kizanzibari utafuatiliwa sana life yako na historia yako na ukoo wako, kiufupi ujipange usiourupuke, na ukifanya hivyo utapata mke ambae hutojutia na utafurahia ndoa yako.
Huu ndo ukwel wenyew yaani
Sio kivile usiwachukulie poa, huku watoto wa kike hawana papara la kuolewa kwa sababu wanaume wengi wao huoa mke zaidi yammoja, so ukitafuta mke wazazi huchunguza Sana hasa ukitoka nje ya Zanzibar
Wanachukulia poa san hao ila ukwel ndo huo hupewi mtt wa watu kama hujachunguzwa vya kutosha na ukionekana una makando kando yaliyokua hayaeleweki tu hupewi ata uwe na hela kias gan ila ukiwaambia wanabisha
 
Back
Top Bottom