Nataka kwenda kuoa Zanzibar

Ameshasema kwao ni waislamu isipokuwa babu yake alibadili ili amuoe bibi yake mi nadhani kuhusu yeye kubadilisha dini kwake haiwezi kuwa tatizo
Kwani kwao kuwa waislamu ndo nini? Unabadili dini kwa sababu kwenu walikuwa waislamu na kuna waislamu au unabadili dini kwa sababu umeielewa haki iko wapi?
 
Mkuu umewahi kuwa na mtoto wa kike? Sidhani kwa sababu kama ungekuwa na mtoto wa kike Usinge toa hoja ya kitoto kama hiyo
Ila tunatofautiana sana kimaisha mpaka akili.......mtoto wa kike ninaye..........ila namuomba mwenyezi mungu maana miaka 16 anakuwa form 2 sasa wewe unamuozesha au wewe ukusoma ..........? Ulivyo maliza madrasa yako basi maisha yaendelee si ndio? Ndio kuraan aitambui mwanamke kabisa ndio maana mnaona wanawake kama takataka...........yaani wewe ni mkubavu kabisa kama utambui haki ya mtoto wakike ........mwache asome aje kuwa wife material .....asije kulika ki masikhara na wahuni mkubavu tenaa wewe
 
Kwa kufuatilia maelezo yako tuu, unaonekana bila mashaka yoyote kuwa Kuna fuse flani kichwani zimekatika
 

Wewe UNAISHI dunia ipi mkuu? Miaka 16 form two? Are u serious? Mimi nimezaliwa mwaka 85 form four nimemaliza na miaka 17 halafu wewe mtoto wako anaishi karne hii form two awe na miaka 16? Mkuu siku hizi watoto wanamaliza form four sana miaka15 au 16.

Hilo tuliweke pembeni. Watoto wa kike wanaanza kupigwa miti wakiwa na miaka kumi na tatu. Huyo miaka kumi na Sita ni mzoefu kabisa wala.sio mtoto. Chaguo ni lako umuache wahuni na bodaboda wamtafune au umuoze kwa heshima
 
Tokaaaaaaaaaaa hapa jinga kabisa............zombie wa 2090 wewe.........ukizaliwa na darasa la saba ........basi na wewe unakuwa darasa la saba.........mkeo pia darasa la saba.......watoto mpaka wajukuu pia darasa la saba kisa unataka heshima .......ndio nyie mnaosema vyeo wanapeana huku shule ujaenda ........utapata wapi kazi huku ujasoma na utaki kusomesha jamii yako kwa makusudi kwa kuogopa kuliwa kimasikhara na wahuni........
Ndio nyie mnao fanya baadhi ya jamii hazina hata msomi mwenye degree katika ukoo kwa kuendesha maisha kipwagu pwagu..............elimika abunuasi wewe
 
Wewe ulie andika hapa ni msomi. Mwenye degree?
 
Wenye above 23 wataolewa na nani sasa kama wote tunataka below 😁
 
Unataka kuoa Binti muislamu au Binti mzanzibari ?
 
kuhusu kuoa mwanamke wa kizanzibari muislamu wakati wewe sio muislamu hiyo ni ngumu Sana
Halafu ongezea katoka bara! Kwa muda niliokaa huku, kuna ugumu wa kuoa mwanamke wa huku hata kama ni muislamu mwenzao kutoka bara. (Utakuwa shahidi)

Mwanaume wa huku ataoa mwanamke kutoka bara, lakini ukweli kutoka moyoni huyo mwanamke atapata sana mateso ya kisaikolojia hasa kama wanakaa huku Zanzibar! (Utakuwa shahidi)

Wanawake kutoka bara iwe muislamu au mkristo huchukuliwa kwa jicho la tofauti na ni baya.Wanaume ndiyo kabisa.(Utakuwa shahidi).

Sifa za wanawake wa huku hazitofautiani sana na wanawake wa pwani. Viburi , ujeuri na kupandisha sauti ni kawaida tu.Mwanamke wa huku hapigwi na ni nadra sana kukuta mwanamke kapigwa (Utakuwa shahidi)

Baba mkwe anakuozesha mwanae kwenye usia anamwambia "akikushinda njoo nyumbani chumba chako bado kipo".

Dini imesema ahudumiwe kwa kila kitu yeye kazi yake kukaa ndani na kuangalia nyumba, watoto na kumstarehesha mume.Wenyewe wamezoea, wewe je? Je, dunia tuliyopo inaruhusu hivyo ukilinganisha na vipato vyetu tulio wengi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…