Nataka na nina Nia ya Kuwa Tajiri Nipeni Mawaidha yenu!

Nataka na nina Nia ya Kuwa Tajiri Nipeni Mawaidha yenu!

kama
Kheri iwe pamoja nanyi ndugu zangu!
Mimi ni kijana Mwenye umri 20s nina ndoto na nia ya kuwa Tajiri(Financialy), Nahitaji kuwa Tajiri yaani kuwa na Pesa ndio Furaha yangu....sihitaji kingine zaidi ya Pesa....Nahitaji kuwa Tajiri.

katika shughuli zangu ninazozifanya mara kwa mara naambulia pesa ya kawaida ya kubadilishia mboga...Hali ambayo siridhiki nayo.

Yaani nataka kuwa Tajiri Haswa ile ukifika mtaani waseme Flani naye ni Tajiri wa Huu Mtaa.

Nimewaza sana nikafikia uamuzi wa kutumia Nguvu za Giza maana kila niliyejaribu kuzungumza naye amejaribu kunisihi kwamba ukitaka kuwa tajiri lazima shetani awe na ukaribu na wewe.

Nimejaribu kufuatilia story za Matajiri wengi nimeona wao pia wameegemea sana upande wa Nguvu za Giza sina uhakika kama wapo au hawapo ambao wanategemea nguvu za Mungu.

Sasa ndugu ambao kidogo Mna idea ziwe hizo za Nguvu za Giza au kama kuna Njia Nyingine tofauti nipeni Mawaidha yenu ili Nifanikishe lengo langu.

Asanteni.
bado hujaolewa tafuta mwanaume wa kichagga, hasa MARANGU.
 
Hii haimfanyi mtu kuwa tajiri
Work hard tu bro.. Ndo siri ya mafanikio.. Utajiri sio game kwamba kuna mbinu zake ili uwin.. Hauna formula.. Just work hard until no work is left.. Ukiwa na tamaa sana ya pesa utafeli kirahisi kwenye malengo yako.. Kuwa na tamaa zaidi ya kufanya kazi kwa bidii.. Kila tajiri ana work hard..

SOMA SANA, SALI SANA, FANYA KAZI SANA
 
Back
Top Bottom