Nataka nianze kunywa pombe bia gani ni nzuri ya kujifunzia?

Nataka nianze kunywa pombe bia gani ni nzuri ya kujifunzia?

Wana Chitchat habari ya mchana
Kama kichwa cha habari kinavyojionyesha hapo juu, nataka nianze kunywa bia,kwa maana sijawahi kunywa pombe yoyote ile, sasa naomba mnishauri ni bia gani ambayo ni rahisi ,na rahisi kwa kujifunzia kwa sisi 'beginners'
Asanteni karibuni sana wana chitchat.

Serengeti ni bia nzuri sana. Haina hang over
 
Mi naomba nijue siku utakayoanza kunywa ili nije hayo maeneo pengine naweza kupata tukio la kupost huku jamii forums
 
Nimelinda clubs na kwenye masherehe. Pombe siyo dili kama unavyofikiria. Nilikua nimeenda kulinda sherehe moja hivi Kuna jamaa alikunywa kila bia aliyoiona baadaye akaanza kulia na kupiga kelele huku anazunguka ukumbi mzima "NIPHIRENIIII, NIPHIRENIIII"

Jiangalie.
😁😄😄😄😄

Alifanikiwa alichokua anaomba hapo ukumbini ili aache kupiga kelele?
 
Mleta mada ni Kama anazifahamu aina zote za pombe.
Safari-kali sana
Balimi-yakishamba
Baltika-sio pombe
Sasa kumbe unazifahamu vizuri tu we cha kufanya agiza kitimoto 1kg ya kurost na ndizi zake iwe na rojo akikisha unakula mpaka umalize alafu agiza faru Jon.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Pombe hawafundishani.. we anza tu hata na GONGO sawa tu.
Kwa siku za mwanzo aanze kunywea mafichoni ili ajishuhudie mwenyewe kwanza akilewe anafananaje[emoji1787]
 
Hii ni Kali kwa mujibu wa wanywaji
Mkuu hizo bia kuna siku zitakuja kukutia hasara, nakushauri anza na Kvant chupa ndogo.
Zingatia: nyama/kitimoto kwa wingi kabla na wakati unakunywa.
Ukizingatia hilo haki ya Mungu nakuapia hicho kiingereza cha kilevi utakisikia kwa wanywa bia,wewe hakitakuhusu.
Karibu chamani, tunywe kwa amani.
 
Back
Top Bottom