Nataka nifanye maamuzi magumu ya kutengana na mke wangu

Nataka nifanye maamuzi magumu ya kutengana na mke wangu

Ukiangalia Au ukipitia uzi wako mmoja hivi Nazani May 2017,ulivyo elezea mlivyoishi kwa shida kutokana na Migogoro ya Wazazi ,Tena Mke Analeta Usumbufu inahuzunisha Sana .
 
KYELAMO ama TUKUYU mkuu maana mi pia nina tatizo langu moja linatokea mitaa ya SONGWE.
Ndio watu wa Mbeya walivyo, ukijitia kulalamika ukoo mzima unakugeukia halafu matoto yao ndio huwa viburi wa kutupa! Kuna limoja limeachika Toronto mapema mwaka huu. Mchizi amerudi bongo kuoa upya kamuachia yule mpuuzi watoto wawili.
Nacheka kama mazuri, sijui tulikukosea nini; bob unajua kutudiss
 
Shida ni kwamba tuna "udume" ndani yetu; ukiwa legelege imekula kwako, ukileta mfumo dume ndo dooh umeharibu kabisa hahaha. Ila mimi ni katika wale wapole sasa
Aisee kuna tatizo kubwa nalo ni KIBURI na UJUAJI, hivi kwanini watu wa kwenu ni Perfectionists?
 
Haya mambo ya ndoa haya kila mtu anaugulia kivyake

Mkuu usikurupuke kwanza kumuacha mkeo ebu kaeni chini kwanza mmalize tofauti zenu

Tatizo kwenye ndoa yenu kila mmoja yupo juu hilo ndio tatizo kubwa mwanamke ana sauti kumzidi baba
Aachane nae tu, Malaya hawezi kutulia (aliye Kula nyama ya mtu haachi)
 
Shida ni kwamba tuna "udume" ndani yetu; ukiwa legelege imekula kwako, ukileta mfumo dume ndo dooh umeharibu kabisa hahaha. Ila mimi ni katika wale wapole sasa
Mimi nimezaliwa na kukulia mbeya, nayajua makabila karibu yote ya mbeya, nilikuwa nikikuta mada inajadili juu ya ubabe wa wanawake wa kabila la mke wangu kwa waume zao nilikuwa na bisha haswaa....but nimejionea mwenyewe kwa kweli....
 
Hakuna mke hapo sepa haraka sana na pole kwa kupoteza muda wako na watoto watarajiwa.
 
Members naomba tu niandike kwa ufupi naamini mtanielewa na kama kuna ushauri nakaribisha.

Tumebahatika kupata mtoto mmoja 5yrs now, wote ni watumishi.

2013 akaomba nimsaidie kumtafutia shule mdogo wake wa kiume arudie kidato cha pili baada ya kufeli form four na kukaa nyumbani miaka karibu mitatu nikafanya hivyo, baada ya muda shemeji akaanza dharau na kiburi kwangu tena mbele ya Dada yake, nikilalamika Dada mtu anachukulia poa, nikavumilia baada ya muda mfupi kapigwa suspension akapiga magoti nimsaidie asifukuzwe shule, nilipoona habadiliki nikajitoa kumsaidia but ilikuwa ni baada ya Dada yake kusema kama naona taabu ye atalipa ninamsema sana mdogo wake.

Dogo kamaliza na division 3 point 26, wakaomba chuo cha afya government wakakosa, huruma ikanijia nikamwambia Dada mtu aende private kidato cha tano akakataa akakomalia kuwa anampeleka chuo cha afya private kama 4 million ada na mahitaji mengine nikamwambia haitawezekana hali ni ngumu kiuchumi aende advance.... nikaambulia matusi kuwa nina "gubu" na maendeleo ya mdogo wake na nisijali yeye na ndugu zake watalipa ( by this time tulikuwa tupo mbali sababu za uhamisho), mi nikaona nisiingilie ndugu.

Kumbe hakuna lolote yeye ndo mlipaji wa kila kitu, nikaja jua baadaye kuwa amekopa bank bila kunijulisha na pesa sijajua kafanyia nini kumuuliza anasema anasomesha......sijakaa sawa kumbe alikokuwa mwanzo kakopa pesa za watu million mbili kwa ajili ya jambo hilo na hajarejesha hadi sasa pamoja na riba inafika nearly 4 million.

Ametoa mimba ili aweze kujikeep busy na biashara nje ya kazi ili kuweza kugharamia masomo ya mdogo wake nilipobaini anasema maisha magumu tusubiri kwanza nilipombana anasema bahati mbaya....uwongo...

Nilisafiri nikarudi ghafla bila taarifa nakuta anaongea na mwanaume kwa simu SAA saba usiku tena anamwomba amsaidie pesa alipe ada......

Mbaya zaidi nyumbani kwangu amegoma kusaidia chochote anasema si kazi yake kufanya majukumu ya kifamilia Mimi kama baba natakiwa nitekeleze kila kitu akifanya ni huruma tu.....

Kila linaloendelea kwangu anawajulisha ndugu zake ( baba, mama na Dada zake), nikichukua hatua hata za kumzaba kidogo ili tuheshimiane basi kesho asubuhi kama ilikuwa ni usiku ntapokea simu za hao watu wakinishutumu nikiwaeleza yaliyojili inaonekana mi ndo nakosea....

Amesafir kikazi wiki ya tatu sasa simu hapokei, SMS, hajibu akipokea haongei....

Namsubir arudi niite ndugu pande zote mbili niwambie nimeshindwa....kweli wanaume tumeumbwa mateso!!

MZEE HUYU NI CHIZI KAA PEMBENI KWA MUDA KAMA MIEZI SITA KISHA ATAREJEA
 
Aisee kuna tatizo kubwa nalo ni KIBURI na UJUAJI, hivi kwanini watu wa kwenu ni Perfectionists?
Hawa raia wa pande hizo wana dharau, kiburi na ujuaji mwingi usio na maana, hawa ndiyo wale wa 50/50 ndani ya ndoa, ukijichanganya kwa hawa kwenye ndoa utapata tabu sana... Hata mke wa Le Mutuz ni wa pande hizo hizo
 
Una akili sana,hebu sogea hapo jirani kamata kinywaji bili leta PM
 
Haya ndiyo madhara ya wanaume kupiga magoti wakati wa kuwavisha pete wake zao. Unapandwa kichwani since day one.

Wewe hapo hukuoa uliolewa, fukuza haraka sana uende kanisani ukajichagulie mtoto mbichi mkali sana atakayesuuza moyo wako.
😀😀
 
Sijui kwanini wewe huna kiburi aisee, hamia chama pinzani basi kuanzia leo maana hao jinsia yako wanakudhalilisha sana Mama
[emoji23][emoji23][emoji23]...ila dah[emoji40]..i wish n8ngekuwa mnyaki na mm jaman
Hizi ID tunazoweka zinaendana na matatizo yetu. Pole kwa matatizo. Haya mambo ya kusomesha ndugu wa mwanamke wakati mwingine ndo chanzo cha matatizo kwenye family
Wanawake wana viburi aisee
 
Hivi visa vinatufanya vijana tusiingie ndoani, Pole sana mkuu
Son,

ndoa haiepukik son' hiyo ni natural call kama unavyobalehe au unapokwenda chooni kujisaidia' huamui wewe ila nafsi yako ndio itakuambia unapofika muda ( wakati) sahihi __mostly 30-45 for a man and 20-35 for a woman
Ukivuka hapo bila kuoa au kuolewa kuna % kubwa ya kubakia single ( bachela sugu) the rest of your miserably life.

Nb, ..huu ni mtazamo wangu binafsi si lazima uwe universal.
 
Usipofanya maamuzi magumu mtagawana Majengo ya serikali. Ni ama wewe utaenda JELA au Yeye Ataenda MOCHWARI. Nadhani umenielewa. Ndoa yenu imefikia Point of No return otherwise Ipo siku Mmoja atazikwa na mwingine ataozea jela.



Nakushauri Fanya maamuzi magumu.
Kumbe vichwa vya uhalisia huu vipo? Hakika ni kwa neema ya Mungu tu ndiyo tupo wanaume dizaini hii.

Maamuzi magumu hutakiwa katika maisha ili yalete maana ya hekima
 
Back
Top Bottom