Nataka nifanye maamuzi magumu ya kutengana na mke wangu

Nyumba hujengwa na Mke, Mume husimamia tu ndiyomaana hata Mungu hutukumbusha "MWANAMKE MPUMBAVU HUIBOMOA NYUMBA YAKE KWA MIKONO YAKE MWENYEWE".

Acha kushindana na Mwanaume Cariha kwa kiburi cha HAKI SAWA maana bado Mume ni kichwa cha familia katika usimamizi wa kila kitu.
Mie nimejibu kulingana na comments ya niliye mu quote mkuu. Nyie wanaume ni vinara wakujiliza hamuheshimiwi, sasa ka nyie hamujielewi mnataka nani awaheshimu sasa
 
Shida ni kwamba tuna "udume" ndani yetu; ukiwa legelege imekula kwako, ukileta mfumo dume ndo dooh umeharibu kabisa hahaha. Ila mimi ni katika wale wapole sasa
Huna lolote, asili ya mtu ni asili yake tu hata iweje hawezi kubadilika kamwe zaidi ya kupunguza ule ukakasi wake.
 
Members naomba tu niandike kwa ufupi naamini mtanielewa na kama kuna ushauri nakaribisha.

Tumebahatika kupata mtoto mmoja 5yrs now, wote ni watumishi.

2013 akaomba nimsaidie kumtafutia shule mdogo wake wa kiume arudie kidato cha pili baada ya kufeli form four na kukaa nyumbani miaka karibu mitatu nikafanya hivyo, baada ya muda shemeji akaanza dharau na kiburi kwangu tena mbele ya Dada yake, nikilalamika Dada mtu anachukulia poa, nikavumilia baada ya muda mfupi kapigwa suspension akapiga magoti nimsaidie asifukuzwe shule, nilipoona habadiliki nikajitoa kumsaidia but ilikuwa ni baada ya Dada yake kusema kama naona taabu ye atalipa ninamsema sana mdogo wake.

Dogo kamaliza na division 3 point 26, wakaomba chuo cha afya government wakakosa, huruma ikanijia nikamwambia Dada mtu aende private kidato cha tano akakataa akakomalia kuwa anampeleka chuo cha afya private kama 4 million ada na mahitaji mengine nikamwambia haitawezekana hali ni ngumu kiuchumi aende advance.... nikaambulia matusi kuwa nina "gubu" na maendeleo ya mdogo wake na nisijali yeye na ndugu zake watalipa ( by this time tulikuwa tupo mbali sababu za uhamisho), mi nikaona nisiingilie ndugu.

Kumbe hakuna lolote yeye ndo mlipaji wa kila kitu, nikaja jua baadaye kuwa amekopa bank bila kunijulisha na pesa sijajua kafanyia nini kumuuliza anasema anasomesha......sijakaa sawa kumbe alikokuwa mwanzo kakopa pesa za watu million mbili kwa ajili ya jambo hilo na hajarejesha hadi sasa pamoja na riba inafika nearly 4 million.

Ametoa mimba ili aweze kujikeep busy na biashara nje ya kazi ili kuweza kugharamia masomo ya mdogo wake nilipobaini anasema maisha magumu tusubiri kwanza nilipombana anasema bahati mbaya....uwongo...

Nilisafiri nikarudi ghafla bila taarifa nakuta anaongea na mwanaume kwa simu SAA saba usiku tena anamwomba amsaidie pesa alipe ada......

Mbaya zaidi nyumbani kwangu amegoma kusaidia chochote anasema si kazi yake kufanya majukumu ya kifamilia Mimi kama baba natakiwa nitekeleze kila kitu akifanya ni huruma tu.....

Kila linaloendelea kwangu anawajulisha ndugu zake ( baba, mama na Dada zake), nikichukua hatua hata za kumzaba kidogo ili tuheshimiane basi kesho asubuhi kama ilikuwa ni usiku ntapokea simu za hao watu wakinishutumu nikiwaeleza yaliyojili inaonekana mi ndo nakosea....

Amesafir kikazi wiki ya tatu sasa simu hapokei, SMS, hajibu akipokea haongei....

Namsubir arudi niite ndugu pande zote mbili niwambie nimeshindwa....kweli wanaume tumeumbwa mateso!!
Hadithi ya kitunga. Futilia mbali
 
Haya mambo ya ndoa haya kila mtu anaugulia kivyake

Mkuu usikurupuke kwanza kumuacha mkeo ebu kaeni chini kwanza mmalize tofauti zenu

Tatizo kwenye ndoa yenu kila mmoja yupo juu hilo ndio tatizo kubwa mwanamke ana sauti kumzidi baba
Unajua shida ya hizi ndoa ni pale mawasiliano yanapovunjika na kiburi na dharau kutawala baina ya wanandoa, hivyo kupelekea tofauti ndogo ndogo kushindwa kutatuliwa biana yao wenyewe.

Kama hawa walipofika inakuwa ngumu kwa mmoja wao au wote kujishusha maana hapo kila mmoja anataka kuonesha umwamba kwa mwenzie.
 
Kitu tall black, kono hilo, guu kama tembo; akikushushia banzi unazima mbona hahw
[emoji23][emoji23][emoji23]wamama wakinyaki rqha sana kwanza wamepanda hewan wanene..ukimsukuma tu mumeo chaliii[emoji23][emoji23][emoji23]... ni mwendo wa ndindindi tu
 
Kitu tall black, kono hilo, guu kama tembo; akikushushia banzi unazima mbona hahw
😂😂😂 i like them..khaa ..wale sio aisee😂..sasa njoo kwa wasukuma..anasemwa amepiga magoti😏😏😏..anaonewa anatazama tu kicjwa chini tena ukimaliza unashukuru kwa kutusiwa na mume😏😏😏
 
Kaka haribu Leo uishi kwa Amani kesho! Fyekelea mbali mapicha picha anayocheza huyo sio mke
 
Members naomba tu niandike kwa ufupi naamini mtanielewa na kama kuna ushauri nakaribisha.

Tumebahatika kupata mtoto mmoja 5yrs now, wote ni watumishi.

2013 akaomba nimsaidie kumtafutia shule mdogo wake wa kiume arudie kidato cha pili baada ya kufeli form four na kukaa nyumbani miaka karibu mitatu nikafanya hivyo, baada ya muda shemeji akaanza dharau na kiburi kwangu tena mbele ya Dada yake, nikilalamika Dada mtu anachukulia poa, nikavumilia baada ya muda mfupi kapigwa suspension akapiga magoti nimsaidie asifukuzwe shule, nilipoona habadiliki nikajitoa kumsaidia but ilikuwa ni baada ya Dada yake kusema kama naona taabu ye atalipa ninamsema sana mdogo wake.

Dogo kamaliza na division 3 point 26, wakaomba chuo cha afya government wakakosa, huruma ikanijia nikamwambia Dada mtu aende private kidato cha tano akakataa akakomalia kuwa anampeleka chuo cha afya private kama 4 million ada na mahitaji mengine nikamwambia haitawezekana hali ni ngumu kiuchumi aende advance.... nikaambulia matusi kuwa nina "gubu" na maendeleo ya mdogo wake na nisijali yeye na ndugu zake watalipa ( by this time tulikuwa tupo mbali sababu za uhamisho), mi nikaona nisiingilie ndugu.

Kumbe hakuna lolote yeye ndo mlipaji wa kila kitu, nikaja jua baadaye kuwa amekopa bank bila kunijulisha na pesa sijajua kafanyia nini kumuuliza anasema anasomesha......sijakaa sawa kumbe alikokuwa mwanzo kakopa pesa za watu million mbili kwa ajili ya jambo hilo na hajarejesha hadi sasa pamoja na riba inafika nearly 4 million.

Ametoa mimba ili aweze kujikeep busy na biashara nje ya kazi ili kuweza kugharamia masomo ya mdogo wake nilipobaini anasema maisha magumu tusubiri kwanza nilipombana anasema bahati mbaya....uwongo...

Nilisafiri nikarudi ghafla bila taarifa nakuta anaongea na mwanaume kwa simu SAA saba usiku tena anamwomba amsaidie pesa alipe ada......

Mbaya zaidi nyumbani kwangu amegoma kusaidia chochote anasema si kazi yake kufanya majukumu ya kifamilia Mimi kama baba natakiwa nitekeleze kila kitu akifanya ni huruma tu.....

Kila linaloendelea kwangu anawajulisha ndugu zake ( baba, mama na Dada zake), nikichukua hatua hata za kumzaba kidogo ili tuheshimiane basi kesho asubuhi kama ilikuwa ni usiku ntapokea simu za hao watu wakinishutumu nikiwaeleza yaliyojili inaonekana mi ndo nakosea....

Amesafir kikazi wiki ya tatu sasa simu hapokei, SMS, hajibu akipokea haongei....

Namsubir arudi niite ndugu pande zote mbili niwambie nimeshindwa....kweli wanaume tumeumbwa mateso!!
Mkuu tunasubiri MREJESHO
 
Back
Top Bottom