Nataka niishtaki bank kwa kutoa pesa zangu zote (dola 50,000) tokea mwaka 2017 bila idhini yangu na nimechukua bank statement

Nataka niishtaki bank kwa kutoa pesa zangu zote (dola 50,000) tokea mwaka 2017 bila idhini yangu na nimechukua bank statement

Kwanza pole sana mkuu, pili mshukuru sana Mungu umebahatika kupata dhamana na uko nje.

Tatu, hiyo kesi kwa hichi kipindi ikipelekwa inavyostahili utafungwa kwa utakatishaji wa pesa na uhujumu uchumi...
Kwa nini afungwe kwa uhujumu uchumi?naona kama unamtisha bila sababu za msingi kama fedha aliipata kihalali na kodi analipa sioni mashaka ya uhujumu uchumi
 
Ukapiga pesa nzuri ndani ya muda mchache maisha yakawa mazuri,baadhi ya wafanyakazi wa benki Wakazuia account yako.je unaweza kutaja Jina la benki?

Sijui kama jamaa atakua tofauti lakini hii michezo wanaijeria wameifanya sana. Walikua wanawatumia watu bila kujua, wanakushawishi ukafungue account uombe na POS machine, baada ya muda pesa zinaingia tu kwa account.

Na wakishaona mchezo umeshtukiwa au unataka kwenda mrama, wanapotea na kutawanyika, unaachiwa balaa peke yako.
 
Kwa nini afungwe kwa uhujumu uchumi?naona kama unamtisha bila sababu za msingi kama fedha aliipata kihalali na kodi analipa sioni mashaka ya uhujumu uchumi

Siku hizi wanaitumia sana hiyo kauli ila kimsingi hawezi kuthibitisha vyanzo vya zilikotoka hizo pesa. Ni kama money laundering. Wajanja wanacheza na system tu pesa inatumbukia kwa account.
 
Sijui kama jamaa atakua tofauti lakini hii michezo wanaijeria wameifanya sana. Walikua wanawatumia watu bila kujua, wanakushawishi ukafungue account uombe na POS machine, baada ya muda pesa zinaingia tu kwa account.

Na wakishaona mchezo umeshtukiwa au unataka kwenda mrama, wanapotea na kutawanyika, unaachiwa balaa peke yako.
Yeap hii michezo ipo watu huwa wanafanya na wale walihisi nimefanya hivyo ndio mana wakaniwekea zengwe, na kupita na pesa...sasa kwa upande wangu sikuwahi fanya hivyo na ndio mana hii case imewaelemea wao kwa sasa na wapo baadhi ya wafanya kazi pale washakimbia msala wameacha kazi kwa sababu ya hii case...
 
Nna mfano hai tena wa mwaka huu kuna mtu pesa imeshikiliwa benki.
nikuweke sawa haya mambo yapo na sio kwa POS tu hata kwa ATM watu waweza fanya, ila sio mchezo safi ukikamatwa umeisha....na wale inaonekana wameshawafanyia watu wengi then wakawakamata na kuwaweka ndani huku nje pesa wanagawana kwakuwa wanajua hauwezi toka na hata ukitoka hauwezi enda pale bank kuidai coz utaogopa msala...sasa jwa upande wangu sikufanya hivyo na ndio mana hadi sasa kuna baadhi ya wafanya kazi wameacha kazi pale bank kwakuhofia ikifika case yangu bank wao ndio wataenda ndani
 
Ni wazi wewe huna hata mwanasheria, na nasikitika kwa hilo, anyway,

1. Tafuta mwanasheria mbobezi, mwenye uzoefu wa kimahakama si chini ya miaka kumi (Makarani wa mahakama wanaweza kukusaidia).

2. Kuhusu kukutana na MD, si lazima ukakutane nae wewe, ongea na mwanasheria wako, akiona kuna umuhimu wa kumuona huyo mtu basi itakuwa hivyo.

3. Kwakuwa imeshafika kwenye hukumu, basi tusubirie hukumu, lakini pia siku ya hukumu hakikisha unakuwa na mtu wako wa karibu, incase ukifungwa (God forbid), basi waambie wakutafutie mwanasheria haraka akusaidie kukata rufaa ndani ya siku 30.

4. Unapofanya biashara za mitandao, akaunti inayoingiza hela sio ya kuhifadhia hela, unatakiwa kuwa na akaunti katika benki nyingine, kila wiki unatoa pesa cash unapeleka benki nyingine.
 
Ni wazi wewe huna hata mwanasheria, na nasikitika kwa hilo, anyway,
1. Tafuta mwanasheria mbobezi, mwenye uzoefu wa kimahakama si chini ya miaka kumi (Makarani wa mahakama wanaweza kukusaidia)
2. Kuhusu kukutana na MD, si lazima ukakutane nae wewe, ongea na mwanasheria wako, akiona kuna umuhimu wa kumuona huyo mtu basi itakuwa hivyo...
okay noted
 
Si unaona nimeanzia bilioni?.
Au tofauti ya milioni na bilioni hauijui?

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app

Oh! Hauko sahihi, wafungwa wengi waliopata msamaha wa rais na kutakiwa kukiri na kurudisha pesa kesi zao hazikufika hata milioni mia tano. (Rejea yule jamaa wa TFF)

Pia kwa mujibu wa sheria, kesi ya uhujumu uchumi isiyozidi 10 M inaweza sikilizwa na mahakama ya wilaya ikiwa DPP atashauri hivyo.

Ingekua ni kuanzia Bilioni wasingeweka hivyo vipengere.
 
Huyu hajui hata kuomba rushwa ya ngono pia ni uhujumu wa uchumi.
Kwani hiyo ni shilingi ngapi?
 
Wameachiwa sababu hela zenyewe ndogo..
Hao wafanyakazi wana tamaa tu.
Oh! Hauko sahihi, wafungwa wengi waliopata msamaha wa rais na kutakiwa kukiri na kurudisha pesa kesi zao hazikufika hata milioni mia tano. (Rejea yule jamaa wa TFF)

Pia kwa mujibu wa sheria, kesi ya uhujumu uchumi isiyozidi 10 M inaweza sikilizwa na mahakama ya wilaya ikiwa DPP atashauri hivyo.

Ingekua ni kuanzia Bilioni wasingeweka hivyo vipengere.

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
 
Namiliki lodge yakulaza wageni kisiwan znz, so nikajiingiza kwenye system ya booking.com ili niweze kurahisishia wageni kutoka angle zote za dunia kufanya booking kwa urahisi sana, nikafungua bank acc na wakanipa ile POS machine na wateja wakawa wanafanya booking from all over the world...

dah aisee hatari sana..

Jamaa yangu tafuta wakili anayejielewa, hapo unakwenda kupiga hela nyingi sana, 50K USD yako itarudishwa na bado bank husika itakulipa fidia hela nyingi sana na hao jamaa wote waliohusika watakula pingu...TAFUTA WAKILI MAKINI aka msaada wa kisheria asubuhi tu unashinda hiyo kesi..
 
Nataka niishtaki bank imetoa pesa zangu zote (dola 50,000) tokea mwaka 2017 bila idhini yangu na nimechukua bank statement kweli inaonesha pesa ilitolewa toka 2017, vipi hapo kwa wataalamu wa sheria hii case imekaaje kwenye masuala ya kunilipa na je kutakuwa na compersation yoyote kutokana na usumbufu nilioupata kipindi hiki chote toka wanichukulie pesa zangu?

Yani umepoteza $50,000 2017 umetulie leo 2020 na huwezi kulipa legal fee ya lawyer unakuja kuomba huku jamii forum?

Maajabu ya Dunia haya, wawezaje Kuwa na uwezo huo na usiwe na legal advice ya 2m per year? Huu si wetu?
 
Back
Top Bottom