Nataka nimpokonye Mwanamke Mtoto(Ni mtoto wa mdogo wangu)

Nataka nimpokonye Mwanamke Mtoto(Ni mtoto wa mdogo wangu)

Kitu pekee ambacho siwezi kufanya ni kumnyang'anya mwanamke mtoto aliyemzaa

Kwenye huduma hapo itategemea na maelekezo Yangu kama yanafuatwa.
 
Ninachokiona ni hujuma, chuki, dharau. Kwanini usimpe mtaji huyo mwanamke? Au kwasababu mtoto now anatembea anaongea hivyo unaona kaz imeisha unaweza mchukua tu ? Tulia ufikiri upya.

Ampe mtaji?😄😄😄 Kuna watu mnavituko Sana.
Huyo mtu wa kumpa mtaji yeye mwenyeewe anajitafuta😆.
 
Yote tisa kijana una dharau na majivuno sana
Ulivyomuelezea huyo binti ni kama vile wewe ndiye uliyemzalisha unataka kumkomoa kumchukua mtoto maana unaona hiyo elfu 20 unayotuma kila mwezi kama milioni

Mtoto sasa anatembea ni kama anaenda mwaka na nusu

Hata uko alipo anaachwa na bibi ndio anakaa na mtoto

Usiwe na uchungu na mtoto kuliko Mamaake.
Kama mama aliyebeba mimba Hana uchungu na mtoto wewe mwanaume unajisikiaje uchungu.

Muachie watoto. Usimnyang'anye mwanamke watoto wake.
Kama utakuwa na moyo mwema toa kiasi kadri ya ulivyojaliwa awakuze watoto wake(sio wako) kwani watoto wako ni wale unaowalea wewe mwenyewe na watakaokusikiliza na kukutii.
 
Mwenzenu azae nyie mmpokonye mtoto? Zaeni na ninyi.

Uwekwe utaratibu wa kuhudumia huyo mtoto au makubaliano ya kumchukua, kumpokonya ndio kufanyaje.
 
Tatizo ni maisha walipo, bima ya afya si kitu kama kula ni shida

Binti amesidiwa ila bado hasaidiki

Ninaposema anategemea Wanaume Nieleweke(anaacha watoto) anaenda kwa wanaume
Unamsema mpwa wangu nini wa huko Busega? Sema tofauti imekuwa kwenye kukaa kwa Bibi yao kijijini, vingine vyote copyright! Mabinti wanapitia changamoto sana! Kwenye kumpokonya watoto mkuu hutaweza, utakuwa umeingia kwenye anga za Dr. Gwajima. Serikali haiwezi kuruhusu uchukue mtoto wa chini ya miaka 7, umri huo wanapaswa kuishi na mama yao.
 
Back
Top Bottom