Nataka niwe na kampuni

Nataka niwe na kampuni

Unknown1

Member
Joined
Mar 9, 2021
Posts
70
Reaction score
45
Kama thread inavojionesha ! Kama tunavojua ,sisi sote ni ndugu!! Basi naomba tusaidiane kwa hili!! Ndoto yangu ni kufanya kazi chini ya kampuni langu, ndiyo furaha nayoiwazia saana saana kwani naimani ya kua ,nikifanikisha kua na kampuni ,basi nitaweza KUJINYIMA USINGIZI kwa ajili ya kampuni na kutengeneza fursa kwa watu wengine kupitia Mimi.

Hivyo basi ,naombeni mawazo yenu (Objectively) , bidhaa ipi itanisaidia kukuza kampuni na kupelekea kuanzisha bidha nyingine na nyingine na nyingine ? (Under the same brand)

NB! Itapendeza ukitoa wazo ambalo huenda likawa faida na kwa wasomaji wengine ;;Hivyo basi ,tujenge hoja pasipokujali Mtaji wa muanzilishi wa hii thread.

#When you get!! reach back ,then pull someone else#
 
Ukiamka usingizini tushtuane mkuu..! Mimi bado nimelala
 
Unapaswa uwe umeshajua hiyo bidhaa tayari, sisi tukushauri tu namna ya kuanzisha hiyo kampuni.
 
Kuna kampuni na kampani kwa maelezo yako unahitaji kampani(support) ili uweze kutengengeneza kampuni(Company)?????? Au sijaelewa
 
Ata ukisema bidhaa iwe kinyesi cha binadamu.. mwenendo wa bidhaa yako ndio uitaji wa kampuni utaupata.

Uza chochote unachopenda, ikifika wakati utakua na ilo kampuni
 
Kuna kampuni na kampani kwa maelezo yako unahitaji kampani(support) ili uweze kutengengeneza kampuni(Company)?????? Au sijaelewa
Nahitaji fursa Au wazo kuhusu fursa itakayokua chini ya kampuni ambayo naweza kuifanyia
 
Kuna kampuni na kampani kwa maelezo yako unahitaji kampani(support) ili uweze kutengengeneza kampuni(Company)?????? Au sijaelewa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] acha ujuaji
 
Kuanzisha kampuni ni kitu rahisi, changamoto ipo kwenye bidhaa utakayoizalisha italeta mauzo?
 
Back
Top Bottom