Nataka nizalishe kuku wa kienyeji laki moja ndani ya miaka mitatu

Nataka nizalishe kuku wa kienyeji laki moja ndani ya miaka mitatu

Ila kwenye ufugaji kuna changamoto sana.

Mimi nilianza na kuku 18 mwaka jana mwezi wa kumi. Wakawa wanaendelea vizuri tu,ila January mwaka huu wakafa 2 sikujua sababu hawakuonyesha dalili za kuumwa(dawa niliwapa na hawakuwa wakitoka nje)

Mwezi May, 2 tena wakafa, hawaonyeshi dalili ya kuumwa unamkuta asubuhi kakauka.

Muda wote hawatagi, nikachinja 2 kwa hasira. Mwezi June akafa tena mmoja wakabaki 11.

Baadaye ndio wakaanza kutaga. Matetea 4 wameshatotoa, 1 amehatamia na mwingine ameanza kutaga juzi.

Sasa hivi nina kuku 11 wakubwa, vifaranga 20 maana baadhi hawakutotoa mayai yote mengine waliyaacha.

Dawa ya mdondo mbali na antibiotics na za dukani kuna dawa nyingine ya asili inaitwa enkaka au shubiri mwitu kwa kiswahili inasaidia kuku wasife kama ukiwachanganyia kwenye maji hasa vifaranga wanapototolewa, pia glucose inasaidia vifaranga kupata nguvu (inachanganywa kwenye maji ya kunywa pia).

Huu ndio uzoefu wangu kwenye kuku, kwenye mbuzi na ng'ombe sijaona changamoto sana maana siku hizi wataalam wa mifugo wanapatikana kwa urahisi kwenye Kata zetu.
Shubili mwitu ni nini mkuu hyo? Nami naihtaji. Au nicheki mkuu unielekeze 0757386921
 
Weka business plan yako ili watu washauri sio maneno ya hisia tu.
 
Bila shaka yupo bize na shamba ndo maana ha reply

Uku laki 1 tena wa kienyeji sio mchezo
 
Back
Top Bottom