Nataka nizalishe kuku wa kienyeji laki moja ndani ya miaka mitatu

Nataka nizalishe kuku wa kienyeji laki moja ndani ya miaka mitatu

Sawa mkuu sina hata kuku mmoja. Mradi wangu ulifeli sana. Mdondo uliua kuku wote nilioanza nao. Yaani hapa nilipo napumulia mashine maana hata pa kwenda sina.

Hapo utakua umefurahi au unataka nikutumie picha za kuku waliokufa ili nikuaminishe?
Ndio mkuu nitataka kuona makaburi ya kuku wetu

Anyway, tuko pamoja mkuu, All the best
 
Ila kwenye ufugaji kuna changamoto sana.

Mimi nilianza na kuku 18 mwaka jana mwezi wa kumi. Wakawa wanaendelea vizuri tu,ila January mwaka huu wakafa 2 sikujua sababu hawakuonyesha dalili za kuumwa(dawa niliwapa na hawakuwa wakitoka nje)

Mwezi May, 2 tena wakafa, hawaonyeshi dalili ya kuumwa unamkuta asubuhi kakauka.

Muda wote hawatagi, nikachinja 2 kwa hasira. Mwezi June akafa tena mmoja wakabaki 11.

Baadaye ndio wakaanza kutaga. Matetea 4 wameshatotoa, 1 amehatamia na mwingine ameanza kutaga juzi.

Sasa hivi nina kuku 11 wakubwa, vifaranga 20 maana baadhi hawakutotoa mayai yote mengine waliyaacha.

Dawa ya mdondo mbali na antibiotics na za dukani kuna dawa nyingine ya asili inaitwa enkaka au shubiri mwitu kwa kiswahili inasaidia kuku wasife kama ukiwachanganyia kwenye maji hasa vifaranga wanapototolewa, pia glucose inasaidia vifaranga kupata nguvu (inachanganywa kwenye maji ya kunywa pia).

Huu ndio uzoefu wangu kwenye kuku, kwenye mbuzi na ng'ombe sijaona changamoto sana maana siku hizi wataalam wa mifugo wanapatikana kwa urahisi kwenye Kata zetu.
 
Ukiwa eneo lenye soko kuku wanalipa sana!
Soko la kuku wa kienyeji kwa huku kwetu ni zuri sana aisee. Kwanza tupo karibu na mjini kwahiyo inanipa urahisi wa kuuza maana ukipiga simu tu, wanakuja kama nyuki na matenga yao
 
Mipango sio matumizi.
Una maanisha nini mkuu??? Kwamba hii ipo kwenye mipango???


Kama una eneo lenye usalama kwa kuku wa kienyeji, nakupa ofa njoo nikupe somo na nikupe formula ya dawa ya mdondo na ndui....

Utajifunza bure kabisa kwa muda mfupi sana. Ila kama unalo eneo la usalama kwa kuku wa kienyeji
 
Una maanisha nini mkuu??? Kwamba hii ipo kwenye mipango???


Kama una eneo lenye usalama kwa kuku wa kienyeji, nakupa ofa njoo nikupe somo na nikupe formula ya dawa ya mdondo na ndui....

Utajifunza bure kabisa kwa muda mfupi sana. Ila kama unalo eneo la usalama kwa kuku wa kienyeji
Sio rahisi uwe na kuku laki moja ndani ya miaka mitatu.
Ni sawa na kuota unapaa.
Wewe fuga kuku wako wakifika 1000 kwa hiyo miaka 3 nenda kanisani/msikiti Katoe sadaka.
 
Sio rahisi uwe na kuku laki moja ndani ya miaka mitatu.
Ni sawa na kuota unapaa.
Wewe fuga kuku wako wakifika 1000 kwa hiyo miaka 3 nenda kanisani/msikiti Katoe sadaka.
Kuku 1000 kwa miaka 3????? Hahaaaaaa.....ndani ya mwaka mmoja nimezalisha kuku 2000 tena hapo nilipata changamoto ya vifaranga kufa kwa wingi mpaka nilichanganyikiwa. Isingekua hivyo, leo hii ningekua mbali sana.


Kwa laki moja kweli siwezi kufikisha kwawakati mmoja maana eneo lenyewe na namna ya kuwazalisha inakua ngumu maana wanachanganya sana. Ila si haba kwa hapa nilipofikia maana uhakika wa maisha tayari ninao...

Nilichojifunza kutoka kwenye ndoto kubwa ni "endapo hutaifikia, basi kuna hatua utakua umepiga"

Hebu jiulize kwa mtu alikua na wazo la kupaa?? Vipi hakuweza kutengeneza ndege??
Ambacho hawezi ni kujiotesha mabawa...

Kwahiyo, , , , , ipo siku kwa hesabu za mauzo, , nitakua nimeuza kuku laki moja
 
[emoji3][emoji3][emoji3] save your Energy brother, kwani kuna mtu alikuuliza kama unajua dawa ya MDONDO au ulisema mwenyewe kuwa unaijua?

Kwahiyo ulisema unaijua ili kuturingishia au? Kwani ungekaa kimya ungepungukiwa nini, maana ni ngumu Kwa mfugaji kuona mfugaji mwenzie anasema anajua Dawa ya ugonjwa Fulani na asiulize ndomana tunauliza

Na issue ingine, labda tu nikwambie wote tunafanya biashara au tunafuga au tunafanya shughuri yoyote iliyo halali hakuna mtu anaweza kuficha shughuri halali labda iwe na makando makando

Utaficha outcome ya biashara ila sio biashara, mtu utajua anafanya kazi gani Ila anaweza kuficha amepata nini kutoka kwenye hiyo kazi

Ungekuwa na hao Kuku, compared na watu vile walivo ku criticize kuwa huwezi Kufuga kuku laki moja, Naimani ata ungefikisha kuku 200 Tu lazima ungeleta picha ili kuprove watu wrong na usingerudi na blaaaa blaaaa kama hizi

Kuhusu Dawa ya MDONDO unasema ohhh sijui formula siwezi kutoa bure it's okay, haya kuhusu picha za kuku nazo watu wa jf wataiba au sio, kuhusu miundombinu nayo watu wa humu watakuja kuivunja au sio

Kwahiyo Kwa lugha nyepesi ni kuwa wewe hao Kuku HUNA, ila umeamua tu kurudi kufufua Uzi wako baada ya kimya kirefu
Hahahaaa!.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom