Okay....
Ipo hivi mkuu. Sehemu ninayofugia ilijengwa maalum kwaajili ya project ya zao la kahawa. Yaani eneo la kukoboa, kuloweka, kuosha, kuanika na kuhifadhi.
Eneo hili lina maghala makubwa matatu na mashimo ya kulowekea hizo kahawa. Mwenye eneo ni uncle ila alimpa mama aishi hapa yeye na familia yake. Pana fence kubwa sana na mradi wa kahawa kwa sasa, uncle ameuhamishia sehemu nyingine ambako ni makazi yake.
Hivyo, niliporudi niliiona fursa ya eneo hili ambalo lina maghala matatu, mashimo yaliyosakafiwa na fence kubwa. Fursa niliyoiona ni ufugaji wa kuku wa kienyeji maana ni nafuu kwenye kuwasimamia.
Hivyo kuku wangu nawafugia kwenye haya maghala. Yaani wanalala humo na kutagia humo ila masindo yao ni nje yaani ndani ya fence.
Vifaranga nawalelea kwenye mafactory ya kusindikia kahawa ambayo hayatumiki. Nawaweka pamoja na mama zao kwaajili ya kuzalisha joto mwezi mmoja.
Nawapa broiler starter ndani ya mwezi mmoja wanakua wanaweza kujitegemea.
Kuhusu dawa, hapo pana ukakasi maana ni sawa na kutoa formula ya kitengeneza soda, bia na vitu kibao. Hata nikikutajia, inaweza niletea shida kubwa. Ingekua physical mimi na wewe, ningekuonyesha