Nataka nizalishe kuku wa kienyeji laki moja ndani ya miaka mitatu

Nataka nizalishe kuku wa kienyeji laki moja ndani ya miaka mitatu

Hahahahaha, eti Kenya yote!
Kuna graduate dropper yaani mhitimu msaka ajira zikabuma, leo ni milionea alianza na kuku 3 tena alipewa na shangazi yake alifaulu kuwamanage wakaazaana na kuongezeka ana supply mayai na kuku Kenya yote.
 
Kuzalisga sawa ila kuwalisha ndo utakwama hapo. Labda uwe na pori lakufikia eka 5 hadi 10 then fuga kwa kuwaachia wajilishe wenyewe
Hata eka 10 haitoshi kwa kuku laki moja. Afanye jaribio tu kuku 500 awaweke kwenye eneo la ekari 5 aone wanavyotawanyika na kusambaa shamba lote. Kumbuka kuku wa kienyeji kama hauna mazingira ya wao kujilisha kwenye nyasi na wadudu huko nje kama unategemea mfuko wako lazima ulie.

Tatizo ni muda mrefu wa kuwahudumia kabla hawajaanza kukurudishia hela na hapo uombe magonjwa yasiwapitie.

Hilo eneo la shamba hata iwe kubwa kiasi gani, watakula siku ya kwanza na ya pili baada ya muda itabaki ardhi isiyo na hata jani moja, hapo sijasemea msimu wa kiangazi ambapo hakuna majani
 
Kila jambo kabla ujalianzisha utatakiwa uwe na way out na way forward , pili strategic plan iki ni kitu muhimu sana maana utajiona wapi unakwenda , tatu technical know how (ujuzi wa fani husika) mleta Uzi alisema waliokuja kupata huduma mashineni walileta magonjwa kuku wakafa Moja Kwa moja akujua kuhusu biosecurity measure, nne kwakuwa alishafuga kidogo Kuna vitu alishanote some details hivyo Kwa sasa akianza tena na vifaranga 300-500 hataweza fikia malengo yake .Dunia Ina fursa za kumtosha Kila mtu.
 
Yaani bana watu Kama wewe yaani wewe kushindwa kwako Basi unajua naye Ni Kama wewe. Tunatofautiana mkuu. Motivation yako sio ya kaangu
Ila ndyo ukweli kuku 15 kufika 1000 cio leo na sio kimahesabu ya kichwa tu
 
Endelea kujifurahisha na kufurahisha wengine, ila kiuhalisia ni kwamba Huwezi kuwa na kuku laki moja

Unawajua kuku laki 1 au unawaskia tu? Hiyo mashine unayosema ipo ya kusaga haina uwezo wa kuhudumia kuku laki 1 Kwa siku

Ni vizuri kama umeamua kukimbia Dar na kurudisha mpira Kwa goal kipa ila kama ndo umerudi na mawazo hayo basi muda sio mrefu utarudi Dar pamoja na kuku wa Mama

Kuanza na kuku 15 saizi unawaza kuwa na kuku laki 1, unadhani wafugaji wenzio walio kwenye tasnia kabla yako hawajui hayo madawa na chanjo?

Huwajui kuku vizuri wewe, Kwa sasa we furahia tu hao vifaranga 70 Kwa sababu wapo ndani ya uwezo wako na ata wafike 500 still wanaweza wakawa ndani ya uwezo wako

ila ukitaka kujua kuwa inawezekana unawaza ukiwa umeshiba sana au Una njaa sana basi Piga hesabu ya gharama ya kulisha kuku 5000 tu ndio utajua kuwa unaota ndoto ukiwa ndani ya Maji

Anyway, All the best mkuu
Nimecheka sana.Vijana wanatoka shule wakiwa na motivated na mitandao.Mwambie ajaribu kuku 100 kwanza,ndiyo ataelewa Somo ni kwa nini watu hatufugi Kuku wa kienyeji kwa idadi ya broiler
 
Nimefikisha kuku 2000 mpaka sasa. Japo nilipata changamoto hapo kati, ila safari ndo imeiva hivi sasa. Nimetenga tray 10 kila siku za kuhudumia kuku wote. Mpaka ndoto yangu itimie.

Karibu tule vijogoo vya kuchoma na mayai ya kuchemsha kwa mama mkuu
 
Back
Top Bottom