Nataka nizalishe kuku wa kienyeji laki moja ndani ya miaka mitatu

Nataka nizalishe kuku wa kienyeji laki moja ndani ya miaka mitatu

Ngoja nikupe mchanganuo wa mradi wangu wa broilers

Hapa sijaweka eneo ambalo nilinunua milioni 20 kiasi cha Sqm 5900

Nilijenga mabanda mawili ambayo yana capacity ya kuingiza kuku 5000 kila moja kwa kiasi cha sh 22m. Mabanda hayo yana sehemu ya stoo za kuhifadhia chakula ukiwa unaingia

Nilizungushia fensi ya nguzo za namba saba na waya wa mfumo wa wavu mkubwa katika eneo lote pamoja na geti na kibanda cha mlinzi chenye choo ndani ambayo ilikula kama 8 to 9m. Pia nimejenga kijumba simple cha vyumba viwili kwa ajili ya wafanyakazi cha bati za upande mmoja na choo kilitumia kama 6m.
Kisima cha maji na umeme vilikuwa kama 3m. Nilisakafia sehemu ya kuhifadhi mbolea na kununua Simtank moja la lita elfu 10 zilighalimu kama 3m hivi. Vifaa vya chakula na maji kama 1M. Kilichobaki ndio nilianzia kuingizia kuku 5000 na kuwatunza na akiba kidogo ilikuwep. Kwa sasa nina kuku 8000 na mwisho wa mwaka huu nataka niwe na kuku 10,000 wa broiler.

Nimenunua eneo kubwa jipya mitaa ya Kibaha ambako ninategemea kufanya mradi mkubwa zaidi huko maana eneo ni kubwa na nita expand vizuri sana kutokana na business plan yangu.. Ninategemea kuchukua mkopo maana nimepata soko Zanzibar nataka niwe na constant supply.

Biashara hii ina changamoto sana ila Allahamdulilah life goes on
Kiongozi,
Mungu akutangulie kwenye plan zako,
 
Mim nimeanza kufuga kuku mwez8 nimeanza na kuk 30 mixer na kanga target yangu mpka 2023 niwe angalau na kuku 1000
 
Kuna kitu mkuu unakosea sana, hakuna aliekataa mazingira ya kijijini kuwa hayako favourable Kwa ajili ya ufugaji wa kuku na hasa free range system....
Mkuu nilibahatika kuanza mradi wa kuku wa kienyeji katika eneo la eka 3 ila nilichukua sehemu ndogo ya eneo kwa kuanzia.

Walifika mpaka 100 na nilikuwa nawala ila siuzi
Mayai ni kugawa kwa familia tu

Nilikuwa na biashara zangu zingine kwa hiyo hapo nilikuwa napenda tu kuona wakizunguka kwenye machine za Unga

Chakula nilikuwa nawapa dagaa na virutubisho kwa kuchanganya ila nilikuja kusoma jamaa USA wanavyoweka rundo la mchnganyiko wa mboga na matunda pamoja na brown staff.

Hiyo ilinipunguzia sana kununua chakula kwani soko la mboga lipo karibu sana na Gari la kubeba lipo
Kazi ni kukusanya mabaki ya mboga na matunda na kubeba bure kutoka sokoni

Mradi niliufunga baada ya kuku kuingiliwa na ugonjwa ulioletwa na wasagaji wa mahindi na mradi ukafa ila sasa nataka kukaa mbali kidogo na kufanya mradi wa kibiashara zaidi na nitahitaji wataalamu wa kuwalipa vizuri

Compost-Corner-Cover.jpg
Browns-and-Greens.jpg
compost-jpg-1.jpg
green-waste-513609_1280.jpg
 
Kuvuka katika project kama hii utahitaji kuku wazazi wanaokaribia 260 mwaka wa kwanza
Wanaotaga mayai angalau 75%
Incubator yenye ufanisi usiopungua 85%
Vifo vya vifaranga/kkuku visizidi 7%
Ukuaji wa project usipungue 30% kwa mwaka....


Najaribu kufikiria jambo gumu kwa rahisi
 
Sio kumkatisha tamaa ni kuelezana ukweli tu. Kuku laki moja wanahitaji mtaji mkubwa sana zaidi ya milioni 500. Sasa hiyo time aliyojiwekea kufikia hiyo idadi si sahihi unless awe na mtaji kama milioni 250 kwa sasa awekeze ili akizalisha afikie hilo lengo...
Ana wazo zuri jamani.

Huwenda akaja kumudu kuku 2000.

Hatokuwa alipo lakini pia kuku wanataga mayai ambayo ni pesa kwenye kuku 2000 huwezi kosa kuku 300

wanaotaga kila siku hiyo yote ni pesa ambayo inasaidia uendeshaji

mtu anaweza kuwa na kuku hata milioni 1 achilia mbali hiyo laki moja
 
Ila mkuu kuwa na kuku mil 1 n Jambo linalowezekana k ila utekelezaji wake n balaa anahtaj kujitoa haswaa
Nikupe mfano mm hapa kwangu vjana wangu wanapassion ya ufugaji niliwanunulia kuku 10 jike 8!jogoo 2 asee wale kuku walianza.kutaga Kama mzaha Sasa hivi wanakuku 180 wa kienyeji ufugaj huu ulianza mwaka Jana mwez 1

Kiukwel wamekuwa msaada hapa nyumban

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Ila mkuu kuwa na kuku mil 1 n Jambo linalowezekana k ila utekelezaji wake n balaa anahtaj kujitoa haswaa
Nikupe mfano mm hapa kwangu vjana wangu wanapassion ya ufugaji niliwanunulia kuku 10 jike 8!jogoo 2 asee wale kuku walianza.kutaga Kama mzaha Sasa hivi wanakuku 180 wa kienyeji ufugaj huu ulianza mwaka Jana mwez 1

Kiukwel wamekuwa msaada hapa nyumban

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Hapo tunaongelea kampuni sasa ambapo una wafanyakazi hata elfu1 na mashamba hata kumi ya kuku lakini ukiwaza kwa udogo kwamba nyumba na ist ndiyo umeshapatia maisha basi kuku elfu mbili ni wengi sana kwako
 
Endelea kujifurahisha na kufurahisha wengine, ila kiuhalisia ni kwamba Huwezi kuwa na kuku laki moja

Unawajua kuku laki 1 au unawaskia tu? Hiyo mashine unayosema ipo ya kusaga haina uwezo wa kuhudumia kuku laki 1 Kwa siku...
[emoji849][emoji849][emoji849][emoji849]
 
Back
Top Bottom