Nataka nizalishe kuku wa kienyeji laki moja ndani ya miaka mitatu

Nataka nizalishe kuku wa kienyeji laki moja ndani ya miaka mitatu

Duuh mkuu usifanye masihala kutunza kuku laki moja ni mziki sana labda uwe na eneo kubwa na mtaji wa kutosha.
 
Mipango yake co yako uckatishe tamaa jaama
Ata kama mipango ni yake na sio yangu, ila kuna vitu vingine sio vya kumjaza mtu ujinga kisa nisimkatishe tamaa

Hebu tuwe serious, hivi wewe unawajua kuku laki 1 lakini au unataka tu kwenda na beat la mtoa mada umfurahishe?

Yani ulishe kuku laki 1 Kwa kutegemea mashine ya kusaga? Hebu acheni masikhara kwenye vitu vya msingi Aisee
 
Simamia kwenye chanjo kuna ugonjwa unaitwa mdondo huo ukipita bandani kama kuku wako hawajachanjwa wanapukutisha banda nzima.
Huwezi kuamini hata doctors wa mifugo huwa wanasababisha kusambaza magonjwa wanapotoka kwenye kuku wagonjwa
Lazima uwe na makoti na Wellington boots kwa ajili yao wanapokuja kwako
Inasaidia kupunguza maradhi
Sio wote lakini ila baadhi hawajali
 
Nauza Asali Ya Jumla Na Rejareja
Ipo Ya Nyuki Wadogo Na Nyuki Wakubwa.

Tunafunga Kwa Vipimo Tofauti Tofautii

Bei Ya Rejareja
Lita1 - 10,000 (Nyuki Wa Kubwa)
Lita1 - 25,000 (Nyuko Wa Dogo)

Bei Ya Jumla
Tuwasiliane Maana Kuna Ofa Zaidi

0658 357537
Tabora

[emoji625] [emoji593] Tunafanya Delivery Nchi Nzima.
Screenshot_20220702-233234.jpg
 
Endelea kujifurahisha na kufurahisha wengine, ila kiuhalisia ni kwamba Huwezi kuwa na kuku laki moja

Unawajua kuku laki 1 au unawaskia tu? Hiyo mashine unayosema ipo ya kusaga haina uwezo wa kuhudumia kuku laki 1 Kwa siku

Ni vizuri kama umeamua kukimbia Dar na kurudisha mpira Kwa goal kipa ila kama ndo umerudi na mawazo hayo basi muda sio mrefu utarudi Dar pamoja na kuku wa Mama

Kuanza na kuku 15 saizi unawaza kuwa na kuku laki 1, unadhani wafugaji wenzio walio kwenye tasnia kabla yako hawajui hayo madawa na chanjo?

Huwajui kuku vizuri wewe, Kwa sasa we furahia tu hao vifaranga 70 Kwa sababu wapo ndani ya uwezo wako na ata wafike 500 still wanaweza wakawa ndani ya uwezo wako

ila ukitaka kujua kuwa inawezekana unawaza ukiwa umeshiba sana au Una njaa sana basi Piga hesabu ya gharama ya kulisha kuku 5000 tu ndio utajua kuwa unaota ndoto ukiwa ndani ya Maji

Anyway, All the best mkuu
Mkuu umesomea kuwatisha watu wenye ndoto zao nini, mana sio kwa 'mitisho' ya namna hii!
 
Namaanisha kibiashara. Kuku wa kienyeji anatumia miezi sita kuwa mkubwa wa kulika wakati chotara anatumia miezi mitatu hadi minne. Kibiashara ilo gape la muda lina maana kubwa sana.

Kuku wa kienyeji ukiwafuga kibiashara (sio free range) wana gharama sana halafu soko lake ni gumu kutokana na bei ambayo inajumuisha gharama za kuwatunza

Kuku wa mayai wana faida sana ila unapaswa kuwa na mtaji wa kutosha kuwalisha miezi sita kabla hawajaanza kutaga

Wanyama wana mzunguko mzuri kwa wawekezaji wanaotaka faida ya haraka maana wakifika kuanzia wiki nne wanakuwa tayari kuuzwa ingawa faida yao si kubwa sana

Kwa ushauri wangu kama mdau wa sekta hii kufuga kuku laki moja wa kienyeji sio jambo zuri unless uwe na soko zuri la kimkataba kabisa. Ngumu sana kukuta watu wanaonunua kuku kwa wingi kama wale wa mikutano au harusi kutumia kuku wa kienyeji. Wa nyama wanamzunguko mkubwa sana na ni nafuu. Kienyeji tunakula kwenye matukio muhimu tu
Nmekaa kijijini kidogo, nmegundua watu wa mjini ukipiga nao story kuhusu kijiji hua wanakitazama kijiji kwa jicho la mjini hivyo ideas zao hua wanadhan kinachoendelea town bas unaweza ukahamishia kijiji na ika work... No, no, si hivyo mkuu. Iko hivi..
Mtoa mada amesema yuko kijiji right? Kwanza choice yake ya kuamua kufuga kuku wa kienyej it's the perfect choice kulingana na MAZINGIRA aliyopo sababu kuu ikiwa eneo, (km analo au atanunua, even one acre or more than that) it's ok maeneo vijijini yapo, mpaka ukitaka pori upasue msitu ww mwenyewe sawa tu hivyo idadi ya kuku 100k inawezekana tu kikubwa MANAGEMENT.
Pili upatkanaji wa chakula ni rahisi kdg, hasa materials km pumba na mashudu akitaka kufuga boilers au chotara kupata chakula chake itamsumbua sn na kwanza kule hawana soko, utajipa headache bure kikubwa afuge kwa kuzingatia anabana cost of production as well as he can. Tena kwa ushauri afuge free range akitaka kuwaweka ndani cost of production lazma zitapanda.
 
Dawa za kinga na chanjo nazijua, chakula ni uhakika kwakua kuna mashine ya kukoboa na kusaga unga wa mahindi. Eneo lipo la kutosha na maji ya kumwaga.

Mtaji ni kuku 15 niliowakuta hapahapa kwa mama. Hakika nataka niwe milionea kwa ufugaji wa kuku wa kienyeji. Hakika huu mradi nauheshimu maana mpaka sasa nimefanikiwa kuzalisha vifaranga 70 na kuna kuku wanataga na wengine wameatamia.

Hakika najuta kupoteza muda dar miaka yote hiyo. Japo siwezi sema nilipoteza muda kutokana na elimu niliyoipata isiyo rasmi
Ndoto za alinacha
 
Nmekaa kijijini kidogo, nmegundua watu wa mjini ukipiga nao story kuhusu kijiji hua wanakitazama kijiji kwa jicho la mjini hivyo ideas zao hua wanadhan kinachoendelea town bas unaweza ukahamishia kijiji na ika work... No, no, si hivyo mkuu. Iko hivi..
Mtoa mada amesema yuko kijiji right? Kwanza choice yake ya kuamua kufuga kuku wa kienyej it's the perfect choice kulingana na MAZINGIRA aliyopo sababu kuu ikiwa eneo, (km analo au atanunua, even one acre or more than that) it's ok maeneo vijijini yapo, mpaka ukitaka pori upasue msitu ww mwenyewe sawa tu hivyo idadi ya kuku 100k inawezekana tu kikubwa MANAGEMENT.
Pili upatkanaji wa chakula ni rahisi kdg, hasa materials km pumba na mashudu akitaka kufuga boilers au chotara kupata chakula chake itamsumbua sn na kwanza kule hawana soko, utajipa headache bure kikubwa afuge kwa kuzingatia anabana cost of production as well as he can. Tena kwa ushauri afuge free range akitaka kuwaweka ndani cost of production lazma zitapanda.
Free range kuku laki moja
 
Nipo sana, sema tunapishana tu.
Bado unaendelea na ufugaji? Mpe uzoefu wako mleta mada
😂😂 bado nafuga, tena mambo yamepamba moto kwa sasa...inabidi anitafte sasa tena aje shambani kabisa.
 
Nmekaa kijijini kidogo, nmegundua watu wa mjini ukipiga nao story kuhusu kijiji hua wanakitazama kijiji kwa jicho la mjini hivyo ideas zao hua wanadhan kinachoendelea town bas unaweza ukahamishia kijiji na ika work... No, no, si hivyo mkuu. Iko hivi..
Mtoa mada amesema yuko kijiji right? Kwanza choice yake ya kuamua kufuga kuku wa kienyej it's the perfect choice kulingana na MAZINGIRA aliyopo sababu kuu ikiwa eneo, (km analo au atanunua, even one acre or more than that) it's ok maeneo vijijini yapo, mpaka ukitaka pori upasue msitu ww mwenyewe sawa tu hivyo idadi ya kuku 100k inawezekana tu kikubwa MANAGEMENT.
Pili upatkanaji wa chakula ni rahisi kdg, hasa materials km pumba na mashudu akitaka kufuga boilers au chotara kupata chakula chake itamsumbua sn na kwanza kule hawana soko, utajipa headache bure kikubwa afuge kwa kuzingatia anabana cost of production as well as he can. Tena kwa ushauri afuge free range akitaka kuwaweka ndani cost of production lazma zitapanda.
Kuna kitu mkuu unakosea sana, hakuna aliekataa mazingira ya kijijini kuwa hayako favourable Kwa ajili ya ufugaji wa kuku na hasa free range system

Hakuna aliekataa kuwa huko materials ya ujenzi upatikanaji ni rahisi, hakuna aliekataa kuwa huko materials ya chakula ni rahisi,hakuna aliekataa kuwa ukiwa na eneo kubwa linaweza kukuwezesha kufuga kuku wengi na kupunguza gharama za uendeshaji

Shida inakuja kwenye number ya hao kuku, hivi ukiskia kuku laki 1 unapata picha gani kichwani? Unahisi ni rahisi tu kwakuwa inatajwa kijijini? Ushawahi kuona mradi wa free range wenye kuku wengi kabisa wangapi labda tuanzie hapo

Wengine tunaongea by experience na msidhani tunaongea Kwa kufata mkumbo au kukatisha watu tamaa,me nimewahi kushuhudia mradi wa kuku elf 6, rudia tena kusoma sijamaanisha kuku elf 60 ni kuku 6000, ambao walikuwa wanafugwa free range kwenye heka 5

Hivi unajua kama vyakula waga vinaisha na inakulazimu uanze kutafuta means ya kuwahudumia? Walikula chakula chote kinachopatikana katika hizo heka 5, au nyie mnazani Ardhi inazaa tu hivyo vyakula kwahiyo kila siku vinakuepo?

Baada ya chakula kuisha ikabidi jamaa aanze kuwapa chakula mwenyewe, mwanzo alikuwa anawapa chakula vifaranga tu ila kuku wakubwa walikuwa wanajitafutia wenyewe kwenye hiyo Ardhi ya ukubwa wa heka 5

Ikafkia hatua Hao kuku elfu 6 pamoja na kuwa walikuwa free range Ila ilifkia hatua wanakula 500kg kila siku, haya wewe uliekazana kusema kuwa vijijini vyakula bei rahisi jikadilie bei ya pumba/chakula alafu zidisha Kwa hizo kilo 500 kila siku tuone utaweza kulisha Kwa siku ngapi

Sasa hao ni kuku elf 6 ambao walikuwa wapo kwenye heka 5 free range na kufikia Kula kilo 500 per day, tupigie hesabu hao kuku laki 1 hiyo free range watakaa kwenye ukubwa gani wa eneno ili wasimalize chakula, na kama wakimaliza pia utupe hesabu watakula kilo ngapi per day..! Tunasubiri
 
Back
Top Bottom