Nataka nizalishe kuku wa kienyeji laki moja ndani ya miaka mitatu

Nataka nizalishe kuku wa kienyeji laki moja ndani ya miaka mitatu

Namaanisha kibiashara. Kuku wa kienyeji anatumia miezi sita kuwa mkubwa wa kulika wakati chotara anatumia miezi mitatu hadi minne. Kibiashara ilo gape la muda lina maana kubwa sana...
Sawa mawazo mazur, vipi we ni mfugaji? Nataka nikuje PM
 
umempa ukweli mchungu kulisha kuku laki1 kisa kuna mashine ya kukoboa karibu kijana analeta masikhara uyu
Wewe ni bora ana hilo lengo na ameanza, mwisho wasiku akifeli kufikisha laki moja huenda anaweza kuwa na hata elfu thelathini sio mbaya
 
Mkuu unawazo zuri sana tena hadi nimependa arif,hizo ndio target za kiume unapoingia kufanya kitu unawaza mambo ambayo wengine wanaona Huwezi au unajitekenya mwenyewe...
Umeongea vizuri sana. Lazima awe na business plan iliyoshiba. Ameongea tu na kuweka time frame ambayo siyo realistic.

Niko kwenye sekta ya ufugaji kuku muda mrefu naelewa sana mwenendo wa hii biashara. Inahitaji mtaji mkubwa sana na umakini.

Mtoa mada anatakuwa kuchanganua yafuatayo:
1. Miundo mbinu . Mabanda, ofisi, machinjio, visima, uzio, machine za kutotoleshea, standby generator nk

2. Chakula na madawa.

3. Wafanyakazi

4. Usafiri

5. Machine za kuzalishia chakula

6. Masoko

7. Mtaji
 
Anaweza akawa ndio mtu wa kwanza kufanya hivyo, kwanini ishindikane kama ana rasilimali za kufanyia hiyo kazi. Kuku laki moja si wengi kushindwa kuwafikia idadi hiyo kwa miaka 3.

Anahitaji kuwa na speed ya uzalishaji kubwa.
Angekuwa na hizo rasilimali asingeenda Kijijini "kwa Mama".
Anyway ni ruksa kuota
 
Elfu tatu mia tano. Nina mpango wa ku expand nimenunua eneo kubwa Kibaha ndio naliweka sawa kimiundombinu nihamishie nguvu zote huko
Khy apo unatrei 115 ivii kwa siku sem mm natak niupe mchanganuo wa kuku mayai mia tatu yaan kuwalisha had watage
 
Haiwezekani hiyo hesabu.
Trust me
Mimi ni mfugaji wa kuku wa kienyeji.
Chanjo nawapa na msosi nawapa.
Pesa kwenye kuku ipo ila si kirahisi hivyo
 
Time frame aliyojiwekea ni ndogo sana na pia hana mtaji zaidi ya hao kuku alionao. Angewekeza say milioni 200 kwa hiyo miaka mitatu angeweza kufikisha kuku laki moja ingawa bado ni ngumu. Ukiingia kwenye hii biashara ndio utaelewa
Anaweza kufika but there is alot of work to be done and he need the at most and undivided attention kwenye project without any distractions.

Mimi huwa naamini katika kufanikiwa zaidi ukiamua kufanya jambo lako kwa namna yako tofauti na kuiga au kucopy wengine muhimu ni uwe na enough energy na drive plus stamina ya kusimamia jambo lako plus kutoruhusu hali ya kuzima akili yako pale mambo yanapokuwa hayaendi kinyume na matarajio yako.

Kwa hili linawezekana kabisa ila inahitajika kazi na sapoti kubwa sana kulifanikisha.
 
Sio kumkatisha tamaa ni kuelezana ukweli tu. Kuku laki moja wanahitaji mtaji mkubwa sana zaidi ya milioni 500. Sasa hiyo time aliyojiwekea kufikia hiyo idadi si sahihi unless awe na mtaji kama milioni 250 kwa sasa awekeze ili akizalisha afikie hilo lengo....
Mkuu yawezekana hiki ulichosema hapa ni ukweli kabisa kutokana na mazingira uliyopo na namna ambavyo unaichukulia pesa, watu tunatofautiana kabisa.

Ila kuendesha mradi wa kuku 8000 kwa 60M, nilitaka nijue kama hiyo fedha imejumlisha na ununuaji wa eneo la ufugaji. Nauliza kwasababu 60M kwa kuku 8000 ni kubwa kidogo.
 
Ni gharama za mradi mzima kutoa ununuzi wa eneo
 
Inawezekana hata kuku milioni moja ni wewe tu, soko la uhakika lipo linataka kuku milioni 10.
Kuna mgodi kanda ya ziwa wanataka kuku wa kienyeji tu, piga Kazi nikupe soko.
 
Kuna graduate dropper yaani mhitimu msaka ajira zikabuma, leo ni milionea alianza na kuku 3 tena alipewa na shangazi yake alifaulu kuwamanage wakaazaana na kuongezeka ana supply mayai na kuku Kenya yote.
 
Mkuu yawezekana hiki ulichosema hapa ni ukweli kabisa kutokana na mazingira uliyopo na namna ambavyo unaichukulia pesa, watu tunatofautiana kabisa.

Ila kuendesha mradi wa kuku 8000 kwa 60M, nilitaka nijue kama hiyo fedha imejumlisha na ununuaji wa eneo la ufugaji. Nauliza kwasababu 60M kwa kuku 8000 ni kubwa kidogo.
Ngoja nikupe mchanganuo wa mradi wangu wa broilers

Hapa sijaweka eneo ambalo nilinunua milioni 20 kiasi cha Sqm 5900

Nilijenga mabanda mawili ambayo yana capacity ya kuingiza kuku 5000 kila moja kwa kiasi cha sh 22m. Mabanda hayo yana sehemu ya stoo za kuhifadhia chakula ukiwa unaingia

Nilizungushia fensi ya nguzo za namba saba na waya wa mfumo wa wavu mkubwa katika eneo lote pamoja na geti na kibanda cha mlinzi chenye choo ndani ambayo ilikula kama 8 to 9m. Pia nimejenga kijumba simple cha vyumba viwili kwa ajili ya wafanyakazi cha bati za upande mmoja na choo kilitumia kama 6m.

Kisima cha maji na umeme vilikuwa kama 3m. Nilisakafia sehemu ya kuhifadhi mbolea na kununua Simtank moja la lita elfu 10 zilighalimu kama 3m hivi. Vifaa vya chakula na maji kama 1M. Kilichobaki ndio nilianzia kuingizia kuku 5000 na kuwatunza na akiba kidogo ilikuwep. Kwa sasa nina kuku 8000 na mwisho wa mwaka huu nataka niwe na kuku 10,000 wa broiler.

Nimenunua eneo kubwa jipya mitaa ya Kibaha ambako ninategemea kufanya mradi mkubwa zaidi huko maana eneo ni kubwa na nita expand vizuri sana kutokana na business plan yangu.. Ninategemea kuchukua mkopo maana nimepata soko Zanzibar nataka niwe na constant supply.

Biashara hii ina changamoto sana ila Allahamdulilah life goes on
 
Nakutakia kila lakheri katika ufugaji ila anza nao taratibu ujue mbivu na mbichi za hiyo biashara. Mimi ni mfugaji wa kuku wa nyama na mayai. Nionavyo mie kwenye mazao ya ufugaji kuku, wenye faida sana ni kuku wa mayai wanafuatia broiler lisha hawa kuku chotora kisha wa mwisho wa kienyeji
Chotara ni dili sana
 
Mkuu unawazo zuri sana tena hadi nimependa arif,hizo ndio target za kiume unapoingia kufanya kitu unawaza mambo ambayo wengine wanaona Huwezi au unajitekenya mwenyewe...
Nlivyokuona tu umetia timu kwny huu uzi, nkajua tu hapa lazima tutakula madini.

Asante!
 
Chotara ni dili sana
Kuku wanaolika kwa wingi ni broiler ingawa faida yake si kubwa sana. Hao ndio wanaoliwa vyuoni, mitaani, harusini, mikutanoni n.k

Chotara kuna rafiki yangu alifuga 30,000 Morogoro na alikuja kuchemsha kwenye masoko. Fanya research utajua au uliza waliofanya hiyo biashara. Kuku dili ni wa mayai kama ukiwawezea faida ipo kubwa
 
Mayai wa kienyeji au kisasa
 
Back
Top Bottom