Mkuu with all due respect kwa ndugu yangu hapo, kwa Akili tu ya kuvukia barabara unahisi kuna mwenye kuku 2000 hapo?
Unapofuga kuku it means hiyo ni biashara, na biashara yoyote ile mwenzie ni matangazo ili biashara/product zako ziweze kusambaa eneo kubwa na hatimae kuongeza income
anasema anauza mayai, anauza na kuku kipi kinafanya afanye Siri utadhani anafuga MAJINI? labda kama utakuwa mgeni wa watu tuliopo humu na majigambo yao nyuma ya keyboard
Kupitia picha atapata wateja wa mayai kutoka mikoa yote,atapata wateja wa mitetea kutoka mikoa yote,atapata wateja wa majogoo kutoka mikoa yote, sasa kuna mfanya biashara asie taka Ku expand empire yake?
Kwahiyo ukikuta mfanya biashara analazimishwa kuonesha/kutangaza bidhaa zake na hataki Usijipe tabu, jibu jepesi ni kuwa HANA
Ata mie naweza kuanzisha Uzi au kutoa comment kuwa kwa sasa nina mbuzi 200 na nilianza na majike wawili na beberu moja mwaka Juzi, wakutoa pongezi atatoa na kukosoa atakosoa
ila kuna wenye curiosity ya kutaka kujua nimefanikiwa vipi watataka kujua kupitia picha za hao Mifugo, pia picha za miundombinu nayotumia katika ufugaji wangu ili itumike kama elimu Kwa wengine lakini pia kujitangaza
Sasa kama nafuga kimya kimya sitaki kuonesha picha za hao mbuzi wala mabanda yao wala mbinu nazotumia kukabiriana na magonjwa sasa m nilianzisha wa nataka kuwa na mbuzi 5000 ndani ya miaka 5 wa nini?