Natamani kila mpangaji angekuwa kama nilivyokuwa mimi

Mkuu huwezi kuwa hujaelewa tunacholalamikia, ni kutotimiza wajibu bila sababu za msingi. Unasema kuhusu dereva wa lori ambaye ni mgonjwa sasa hapo unahitaji sababu zipi? Hivi kuwa na shida ya uchumi ambazo sio kila mtu anaziona, inakupa kibali cha kutowasiliana na mwenye nyumba?

Tunazungumzia mpangaji asiyetimiza wajibu wake bila sababu za msingi. Usipoteze uelekeo wa hoja.
 
Hata mimi sina kikubwa, hata ningekuwa zero kabisa, kukosa sio sababu ya kutotimiza wajibu wako. Usijifichie kukosa kwako kama sababu ya kutolipa kodi ya watu. Huna jisalimishe.
 
Watu ni kama vidole.
 
Shikamoo kaka...
 
1. Kulipa kodi ya mwaka mmoja siyo kuwa mpangaji mzuri. Kodi inatakiwa kulipwa kila mwezi, tarehe za mwanzoni. Huu utaratibu wa kulipa kodi ya miezi mitatu, sita au mwaka, ni kumuumiza mpangaji.
2. Kurekebisha nyumba ni kazi ya mwenye nyumba na huwa inapigiwa mahesabu kwenye kodi. Kama wewe ulikuwa unafanya basi hukujua na ulikuwa unajiumiza mwenyewe.
 
Muhasibu umesema kweli kuna mama mmoja hm ameharbu nyumba kabisa yani kumekua kama jalalani, mwezi uliopita niliweka mazingira fresh nikajua atajifunza lakini wapi. Kuna watu uchafu ni asili yao wakikaa bila kuvuruga vitu wanahisi kuumwa.
Tatizo la wenye nyumba Tanzania wanadai kodi ya muda mrefu. Kodi inatakiwa ilipwe kila mwezi, mwanzoni, na kunakuwa na fedha za deposit eg kiasi cha kodi ya miezi miwili ili mpangaji akiharibu chochote, zile fedha za deposit zinatumika kulipia.
 
[emoji1317]
 
...Mkuu, umehamia Kwako 2016, lakini Leo Miaka Saba baadae ndio umeona Utujulshe jinsi Ulivyokuwa Mpangaji Mzuri ??? [emoji846]...

Sent from my TECNO BD4j using JamiiForums mobile app
 


Wacha kiburi kijana, bado u mdogo, haya maisha hayana adabu. Usiongelee mambo ya mtu kama huyajui.

Kuna watu wanahudumia Wazazi wao huko kijijini na wanaunga unga, haya maisha, wewe acha tu, kuna wazembe sio wote.

Usione watu wanatabasamu, wengine wana shida nyingi sana na hawazisemi, waache tu, kama unayo wewe shukuru Mungu.
 
Hakuna baya aliloongea hapo.. umeamua tu kucatch feelings, busara ya kukosa kadi ni kumpa taarifa muhusika kabla muda haujafika, magumu ni sehemu ya maisha na kama kabla ya magumu ulikua mlipaji mzuri landlord muelewa hawezi kukuharass
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…