BEZO
JF-Expert Member
- Jul 15, 2023
- 1,770
- 4,449
MKUU,ndo maana amesisitiza kuwa atoe taarifa kwa mwenye nyumba siyo kukaa kimya.Kamwe sitamteta mtu au kumsimanga ambaye sijui ana shida gani.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
MKUU,ndo maana amesisitiza kuwa atoe taarifa kwa mwenye nyumba siyo kukaa kimya.Kamwe sitamteta mtu au kumsimanga ambaye sijui ana shida gani.
Hahaa! Wapangaji watukutu ujumbe uwafikie haraka sana.Shekhe hizo za kulipa kodi zaidi ni kujiwekeza security deposit tu Ila jambo la msingi ni kutimizi wajibu wako kulipa kodi inayotakiwa kwa wakati na kuweka mazingira ya nyumba safi na salama
Aina hii ya mpangaji ni kumpiga notisi tu arudi nyumbani kwa mama yake!!Kwa nini yeye asiseme hiyo shida, ana wajibu wa kufanya hivyo, kama hawezi alipe kodi. Kukaa kimya maana yake kiburi. Kwa post zako inaonyesha wewe ni mpangaji pasua kichwa
Umeongea pointi sanaUjaongelea usafi peke yake, umeongelea kulipa mwaka mzima etc, andiko lazo zuri, ila lina element ya kiburi.
Kuna watu wema wengi sana ila wanapitia wakati mgumu sana, hawawezi kuwa kama wewe kwa sababu hawana fursa.
Na wewe ulivyo ni vyema, ila ni kwa sababu una afya ambayo amekupa Mungu, ungekuwa huna pengine usingewe, kuwa ulivyo.
Siku zote ukiongelea mafanikio, kwanza mshukuru Mungu, then endelea na mengine, nafikiri bado u mdogo ki umri, haya maisha hayana adabu.
Kuna jamaa alikuwa kijana wangu anaendesha lory la mchanga, nilimpenda sana, mstaarabu, analipa lodi kwa wakati etc, mtu mwema sana sana.
Siku moja alikuwa anashuka na lory Ngorongoro, akapata ajali, akaparalyse nusu, anahudumiwa na mke kila kitu, hata ngoma haisimami kabisa.
Kakaa ndani mda sana, akaanza uza vitu, baada ya mda sababu ya kukaa sana, akapata Kisukari, just imagine maisha yake.
Mshukuru Mungu ulivyo, ondoa neno kama mimi, nakupongeza, ila sio kwamba wote ambao hawako kama wewe ni wabaya.