Natamani kuipinga Taarifa ya awali juu ya sababu za kudondoka kwa lift ya Millenium Tower

Natamani kuipinga Taarifa ya awali juu ya sababu za kudondoka kwa lift ya Millenium Tower

Kuja jamaa yangu alikwama nusu saa tu alitoka kununua maandazi na vitumbua alipookolewa akadai amekaa siku tatu. Hiyo mwaka 2003. Huwa nikimkumbusha anacheka sana. Maana ndo alikuja Dar kwa mara ya kwanza Chuo akitokea Kishimundu Moshi
Sasa siku moja alfajiri, kuna jamaa aliingia na taulo kwenye lift floor za juu kwenda kuoga floor za chini pale hall 5, na wakati huo ana UE saa 2 asubuhi. Kaingia kwenye lift, si ikawa haisimami, inatoka floor ya mwisho juu, ikifika ya mwisho chini inageuza, na mchezo uliendelea hivyo kama roundi mbili. Ikaja kusimama floor ya nane (kama sijakosea) ikiwa imesimama chini kidogo ya usawa wa floor, imetengeneza kama ngazi moja hivi. Jamaa alitoka anatweta hatari. Bahati yake aliwahi UE
 
Umesema kweli kabisa. Hawa ni vilaza tu wasiojua kitu. Ila kwa Tanzania litapita na kesho tutakuwa tumeshasahau. Kuna kipindi mtu mmoja alifariki kwenye ajali ya lift tena hapo hapo Dar. Unajua ilikuwaje? Walikuwa wanafanya service, lift iko ghorofa ya chini na ghorofa ya juu kabisa wamefungua mlango lift wa hiyo floor. Akaja mtu bila kujua, akaingia kwenye ule mlango na kudondoka mpaka chini.
Kwamba wanafanya matengenezo huku hawajaweka baricades..!! (warning tapes au kufunga kabisa..!)
 
Je ingekuta Ni Yale majengo gorofa 50 ,60 had 100 za new York mnk Ni kwamba ngoma ingeua wote

Si kweli.

Hata kama ikianguka haiwezi kuwa na madhara makubwa kwa kiwango hicho, kwa sababu lift ina shock absorber kwenye case kama ya free fall inapotokea.

Katoka jengo la NSSF Kaloleni Plaza ilianguka kutoka ghorofa ya saba ikiwa na watu ndani na ilikuwa hakuna hata majeruhi mmoja, wote walikuwa salama.
 
Watanzania tunapendaga na kuendekeza sana anasa. Sasa lifti ya nini? Yani unakuta ghorofa ya kumi na nne hadi 20 huko eti watu wanatumia lifti. Unabaki tu kujiuliza are we really serious with our wellbeing 😡😡😡😡😡
Aise! Ghorofa 14 sio makalio aise.....hivi umewahi kujaribu kupanda hata flow 10 tu?
 
Poleni sana wakazi wa Dar na wahanga wa ajali, nimeona kwenye mitandao hii habari nikatamani kujua vingi, na ningekuwa Dar ningefika hata eneo la tukio for physical observation.

Nimeona Mtu kutoka jeshi la Zimamoto na Uokoaji akisema kuwa Sababu kuu za kudondoka kwa lift ya jengo la Millenium Tower ni wingi wa watu. BADO KICHWA CHANGU HAKIJAAFIKI. Na hoja ni hizi:

1. Limitation ya Lift haipo kwenye idadi ya watu, ila ipo kwenye uzito. Idadi ya watu huwekwa tu kama makadirio kwamba kila mtu anaweza kuwa na uzito wa wastani kilo 75. Hivyo ikiwa limit ni kilo 750 itaandikwa ni watu 10 kwa maana ya 75 x 10. Sasa Jeshi limehakikisha vipi kuwa idadi ya watu iliyokuwepo imezidi limitation ya uzito?

2. Mechanism ya Lift ilivyo, uzito ukizidi huwa inatoa notification na haiendi, sasa iliendaje? Je haikutoa hata notification? Jeshi hakukuwa na any notification au lift kugoma kufanya kazi? Na kwanini ishuke kama jiwe?

Ifike wakati nadharia zetu ziwe zinachanganua mambo vizuri ili tujue tatizo ni nini, kulikubali tatizo kwa nadharia tu haiwezi kusaidia kuepuka majanga. Lazima tuzishughulishe akili zetu zifanye kazi kitaalamu na tuwe na Majibu ya kitaalamu. SIo yale yatakayokubalika na jamii kwa haraka.

idadi ya watu kuzidi/uzito kuzidi jambo dogo sana kwenye lift kuanguka.

Tunaomba majibu sahihi ili na sehemu zingine waweze kuchukua tahadhari.
Video Haina content zozote ila Ina mb 22
 
Back
Top Bottom