Natamani kuipinga Taarifa ya awali juu ya sababu za kudondoka kwa lift ya Millenium Tower

Siwalaumu sana polisi, huwa wanalazimika kuelezea mambo ambayo hawana utaalamu nayo.

Tunacho chombo kinachokagua mejengo, walipswa watoe taarifa ya awali na polisi.
 
Kuja jamaa yangu alikwama nusu saa tu alitoka kununua maandazi na vitumbua alipookolewa akadai amekaa siku tatu. Hiyo mwaka 2003. Huwa nikimkumbusha anacheka sana. Maana ndo alikuja Dar kwa mara ya kwanza Chuo akitokea Kishimundu Moshi
Sasa siku moja alfajiri, kuna jamaa aliingia na taulo kwenye lift floor za juu kwenda kuoga floor za chini pale hall 5, na wakati huo ana UE saa 2 asubuhi. Kaingia kwenye lift, si ikawa haisimami, inatoka floor ya mwisho juu, ikifika ya mwisho chini inageuza, na mchezo uliendelea hivyo kama roundi mbili. Ikaja kusimama floor ya nane (kama sijakosea) ikiwa imesimama chini kidogo ya usawa wa floor, imetengeneza kama ngazi moja hivi. Jamaa alitoka anatweta hatari. Bahati yake aliwahi UE
 
Kwamba wanafanya matengenezo huku hawajaweka baricades..!! (warning tapes au kufunga kabisa..!)
 
Je ingekuta Ni Yale majengo gorofa 50 ,60 had 100 za new York mnk Ni kwamba ngoma ingeua wote

Si kweli.

Hata kama ikianguka haiwezi kuwa na madhara makubwa kwa kiwango hicho, kwa sababu lift ina shock absorber kwenye case kama ya free fall inapotokea.

Katoka jengo la NSSF Kaloleni Plaza ilianguka kutoka ghorofa ya saba ikiwa na watu ndani na ilikuwa hakuna hata majeruhi mmoja, wote walikuwa salama.
 
Watanzania tunapendaga na kuendekeza sana anasa. Sasa lifti ya nini? Yani unakuta ghorofa ya kumi na nne hadi 20 huko eti watu wanatumia lifti. Unabaki tu kujiuliza are we really serious with our wellbeing 😑😑😑😑😑
Aise! Ghorofa 14 sio makalio aise.....hivi umewahi kujaribu kupanda hata flow 10 tu?
 
Video Haina content zozote ila Ina mb 22
 
Hivi pale Chamwino kuna lift?, kama ipo nijibuni haraka kesho tufurahi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…